singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
TANGU Rais Dk John Magufuli aapishwe na kuingia Ikulu mapema mwezi Novemba 2015 ameonesha dhamira ya kweli ya kutaka kuwatumikia Watanzania kwa kuzingatia hali halisi aliyoikuta: Kisiasa, kiuchumi, kijamii na kimazingira.
Baada ya Dk Magufuli kuingia madarakani alikuta changamoto nyingi katika sekta mbalimbali ambazo kwa namna moja au nyingine wananchi wanaamini zitafanyiwa kazi ipasavyo. Miongoni mwa changamoto zilizoko katika jamii ni pamoja na kukithiri vitendo viovu kama ufisadi, rushwa karibu katika sekta zote; uzembe serikalini katika kutoa huduma za kijamii kama afya, elimu, maji, miundombinu, kukithiri kwa biashara ya mihadarati na mengineyo mengi.
Kutokana na hali hiyo, Dk Magufuli anafahamu fika kuwa akilegea hawezi kusonga mbele ili aweze kutimiza azma yake ambayo amekuwa akiisema hata wakati alipokuwa akiomba kura huku akisisitiza kaulimbiu ya “Hapa Kazi Tu chagua Magufuli”. Katika harakati za kampeni pia akaonesha kuwa akichaguliwa nguvu ya kufanyakazi anayo kwa kuingiza vibwagizo vya “pushups”.
Baada ya kuingia Ikulu akawaonesha Watanzania kuwa kazi aliyoiomba na akabahatika kuipata kweli anaiweza. Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki mstaafu, Dk Felician Kilahama anasema ndani ya miezi mitatu Rais amefanya mengi na anapaswa kuungwa mkono na wote wanaomtakia mema pamoja na kujiweka tayari kwenda na kasi yake ili kuleta mabadiliko ya kweli katika kuendeleza taifa.
Huduma katika Hospitali Kuu ya Taifa Muhimbili zimeimarika mfano, mashine muhimu za vipimo zinafanya kazi na duka la kuuza dawa kwa wagonjwa kupitia wakala wa Serikali wa Dawa (MSD) kuanzishwa na wagonjwa kupata dawa kwa bei nafuu. Hata kama dawa au huduma Muhimbili hazijatosheleza kulingana na mahitaji lakini mwelekeo ulivyo unaridhisha huku hospitali nyingine, vituo vya afya na zahanati sehemu nyingine nchini zikiiga mfano huo kwa kujitahidi kuboresha huduma wanazozitoa kwa wagonjwa.
Sasa Serikali ya Awamu ya Tano hata kama ni ya CCM imeingia madarakani kwa kufahamu fika kuwa Watanzania hawataki mchezo wamechoshwa na ubadhirifu wa mali za umma hivyo wanataka mabadiliko kifikra na kimatendo. Inakuwaje, “milango ya nyumba iwe wazi (yaani haijafungwa) lakini baadhi ya watu wakiwemo wageni waingie ndani kwa kupitia madirishani tena kwa kusukumana na kelele zikiwa nyingi ndani ya nyumba?”
Kwa hali kama hiyo kuna tatizo la msingi ambalo Rais wa Awamu ya Tano anajitahidi kupambana nalo ili kurudisha maadili kwa viongozi na watendaji wa serikali. Pamoja na jitihada zote anazozifanya Rais tena kwa muda wa kipindi kifupi sana (miezi mitatu tu) kuna baadhi ya watu wanaombeza na kudai kuwa hakuna la maana analolifanya bali anavunja sheria, taratibu na kanuni.
Watu wanaodhani kuwa rais anavunja sheria wanapaswa kutafakari juu ya madai yao ili waweze kuondokana na dhana hiyo potofu na badala yake wajenge mawazo chanya na kumuunga mkono rais ili kutimiza lengo lake la kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye viwanda na yenye uchumi wa kundi la kati. Baadhi ya wafanyabiashara wanaokwepa kulipa kodi wanaotakiwa kulipa ili kuongeza ufanisi wa serikali katika kutoa huduma za kijamii kwa wananchi wake.
Watanzania tumshukuru Mungu kwa kutuwezesha kumpata Rais huyo ambaye anaonesha dhamira ya kweli ya kutaka kuinua hali za maisha kwa Watanzania wengi na masikini na ukweli unabaki palepale kwamba “mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni,” anasema . Ikubalike kuwa muda mfupi Magufuli ameonesha kuwa anaweza na kama ni kuvunja sheria, taratibu na kanuni hayo ni mapito tu ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuleta mabadiliko yaliyokusudiwa.
Kuubadilisha mfumo wa kiutawala ambao umekuwepo kwa muda mrefu siyo kazi ndogo ni kubwa na ngumu sana na kadhalika tumwombe Mungu amtie nguvu na kumjaza hekima na busara. Iwapo kuna baadhi ya wasiopenda kuona mabadiliko ya kweli nchini Tanzania kupitia serikali iliyopo madarakani, ni vizuri kusubiri maana miaka mitano siyo kipindi kirefu sana. Tabia kama hizo zinajitokeza kutokana na kumomonyoka maadili na baadhi kuwa na ubinafsi ulioshamiri kuliko kuwepo hali ya utaifa na uzalendo kwa nchi .
Ihakikishwe kuwa hatokatishwa tamaa Rais bali aungwe mkono ili wote kwa pamoja tuweze kuyafaidi matunda yatokanayo ra rasilimali zilizopo nchini kwa kuwa wengi wamechoka na vitendo vya kifisadi, rushwa, wizi, ubadhirifu wa mali za umma na kero nyingi katika huduma za kijamii. Rais Magufuli aungwe mkono katika vita hiyo ngumu ili kwa pamoja tupate mafanikio mazuri. Kimsingi kinachotakiwa ni suala zima la maslahi mapana ya taifa na watu wake ambapo kinachotakiwa ni kuona dhana hiyo inajengeka zaidi ndani ya fikra za viongozi.
Marehemu Baba wa Taifa; Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kutuasa kwamba “ili Taifa liweze kuwa na maendeleo endelevu tunatakiwa tuwe na vitu vinne ambavyo ni ardhi (ambayo tunayo); watu (ambao wapo); siasa safi na uongozi bora”. Vilevile, marehemu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kusema kwamba “kuongoza ni kuonesha njia” na “kupanga ni kuchagua”.
Sasa ilifika wakati viongozi wa taifa wakapanga na kuchagua njia ya kwenda kwenye maslahi binafsi na kuachana kabisa na maslahi mapana ya taifa. Vilevile, jitihada za makusudi zilifanyika za kuachana na misingi mahususi ya utaifa likiwemo suala zima la Maadili na Uwajibikaji wa viongozi kwa umma wakati marehemu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kuasa kwamba “hakuna taifa ambalo halina maadili na miiko yake,” hata kama ni taifa lililoendelea lazima lizingatie sana masuala muhimu ya kimaadili na miiko.
Jitihada za Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano zinalenga kuwezesha kuelekea kuwa na taifa lenye maadili na miiko ya kazi katika sekta za umma na binafsi. Kwa mfano, suala la kulipa kodi ni sehemu ya kuwa na maadili mazuri na uwajibikaji ndani ya taifa letu. Baadhi ya wawekezaji toka nje nao wamejikuta wanatumbukia katika hitilafu hiyo mbaya sana na wakawa wanakwepa kulipa kodi, iwapo kodi haikusanywi ipasavyo na kuwasilishwa Hazina Serikali itawezaje kuboresha huduma za kijamii?
Magufuli anafanya mambo mengi kwa nia njema ya kuiwezesha serikali yake kuweza kujenga uwezo wa kujitegemea kama taifa na kwenye shughuli binafsi za familia zetu na jamii kwa ujumla. Pamoja na mambo mengine, moja ya maamuzi yake ni kupunguza matumizi makubwa kwa sekta ya umma ikiwemo kudhibiti safari za nje ya nchi. Baadhi wanalaumu kwa nini hajasafiri kwenda nje ya nchi kwa misingi ya maslahi ya taifa, ukiangalia kwa undani zaidi utaona bado ni mapema sana kwa yeye kufanya safari za nje.
Kipindi cha miezi mitatu ni kifupi sana kuweza kuleta hofu ya kwa nini Rais hataki kusafiri nje ya nchi. Kusema kweli hali ilivyokuwa inamlazimu aliweke taifa kwenye misingi thabiti na kuhakikisha tunarudi kwenye njia ya kuleta maslahi mapana ya taifa na watu wake badala ya kuangalia maslahi binafsi. Kufanikisha kazi hiyo siyo lelemama ni kujitolea kwa nafsi, nguvu pamoja na utayari wa kuwatumikia Watanzania, masuala ya nje yenye maslahi kwa taifa anayafahamu na wakati utawadia atakwenda kusiwe na wasiwasi juu ya hilo.
Kwa uhalisia ikiwemo hali mbaya ya mapato na madeni makubwa; mafuriko pamoja na ukame vikiwa ni athari za tabianchi; mimi naona yuko sahihi kwa kutokwenda nje ya nchi kwa lengo la kuimarisha misingi thabiti ya kuiendesha serikali yenye mwelekeo wa kuleta maslahi mapana kwa taifa na watu wake.
Masuala ya kwenda kuhemea huko nje yatafuata baadaye na pia misaada yenye masharti kama kuingiza “ushoga” ndani ya maadili isipewe nafasi hata kidogo. Hivyo, shime Watanzania kumuombea Rais Dk John Magufuli kwa sababu kazi aliyoianza ni ngumu sana imejaa lawama nyingi na changamoto nyingi akihitaji ulinzi kutoka kwa Mungu, amjaalie afya njema, busara na hekima.