Carlos The Jackal
JF-Expert Member
- Feb 6, 2017
- 24,036
- 71,268
FalaNalazimika kuandika mada hii kwa uchungu na hasira kwa sababu mitandao ya kijamii, ikiwemo hii yetu ya JF, imejaa bandiko kuhusu korona (CIVID-19), zikiishutumu Serikali ati kwa kutokuchukua hatua stahiki za kupunguza, kama siyo kukomesha maambukizi.
Nani anahusika na uzembe huo kama siyo sisi wenyewe, wakiwemo waandishi hao wanaoshutumu Serikali na kutia hofu jamii.
Je, tumejiuliza ugonjwa wa UKIMWI, usiokuwa na tiba au chanjo, umeisha? Je, watu hawafi kwa UKIMWI? Je, nani anamsimamia mtu kutumia kinga dhidi ya maambukizi? Je, kuna sheria imetungwa inayolazimisha mtu kutumia kinga wakati wa tendo la ngono?
Serikali, kupitia Wizara ya Afya, imekuwa ikitoa tahadhari na maelekezo dhidi ya magonjwa yanayo ambukiza na yasiyo ambukiza. Wewe na mimi ni kwa kiasi gani tunafuata hayo? Au tunajali tiba kuliko kinga?
JF doctor tusaidie elimu ya kujikinga na magonjwa mbalimbali tuondokane na ujinga huu.
La sivyo, Wajinga ndio waliwao na wataondoka kwa ujinga wao wakidhani wao ni werevu.