Watanzania wanataka Serikali ifanye nini zaidi ya kuwatahadharisha kuhusu COVID-19?

Nalazimika kuandika mada hii kwa uchungu na hasira kwa sababu mitandao ya kijamii, ikiwemo hii yetu ya JF, imejaa bandiko kuhusu korona (CIVID-19), zikiishutumu Serikali ati kwa kutokuchukua hatua stahiki za kupunguza, kama siyo kukomesha maambukizi.

Nani anahusika na uzembe huo kama siyo sisi wenyewe, wakiwemo waandishi hao wanaoshutumu Serikali na kutia hofu jamii.

Je, tumejiuliza ugonjwa wa UKIMWI, usiokuwa na tiba au chanjo, umeisha? Je, watu hawafi kwa UKIMWI? Je, nani anamsimamia mtu kutumia kinga dhidi ya maambukizi? Je, kuna sheria imetungwa inayolazimisha mtu kutumia kinga wakati wa tendo la ngono?

Serikali, kupitia Wizara ya Afya, imekuwa ikitoa tahadhari na maelekezo dhidi ya magonjwa yanayo ambukiza na yasiyo ambukiza. Wewe na mimi ni kwa kiasi gani tunafuata hayo? Au tunajali tiba kuliko kinga?

JF doctor tusaidie elimu ya kujikinga na magonjwa mbalimbali tuondokane na ujinga huu.

La sivyo, Wajinga ndio waliwao na wataondoka kwa ujinga wao wakidhani wao ni werevu.
Fala
 
Mbona serikali inatoa takwimu za maambukizi ya ugonjwa wa ukimmwi na inatoa tahadhari watu kuepuka ngono zembe na serilikali imekubali matumizi ya ARV's na condom ambazo zimetoka kwa Wazungu?

Je,Mwananchi wa kawaida anaweza kutoa tamko mipaka ya nchi ifungwe ili kuzuia kusambaa kwa Corona?

Ligi kuu Tanzania bara isimamishwe tuu au mechi zichezwe bila mashabiki maana itafika kipindi mnyororo wa maambukizi utaku mkubwa Sana kiasi kwamba kutakua hakuna sehemu ya kukimbilia,hapa serikali ndo yenye uwezo wa kufanya hili Mwananchi wa kawaida hawezi kutoa tamko ligi isimame au mechi zichezwe bila mashabiki

Mgonjwa wa Corona anatibiwa na familia 😂 hapa Napo Kuna hatari kubwa ya huu ugonjwa kusambaa kwa Kasi

Tunataka serikali ipambane na gonjwa hili la Corona Kama inavyopambana kuwapata wakwepa Kodi.
 
Ni wajinga wachache wa pale chadema mkuu! Alafu kumbe mwenyekiti wao nae kakimbilia dubai
 
Back
Top Bottom