Watanzania wanataka mabadiliko, watanzania wamechoka na rushwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania wanataka mabadiliko, watanzania wamechoka na rushwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sifongo, Sep 27, 2012.

 1. sifongo

  sifongo JF-Expert Member

  #1
  Sep 27, 2012
  Joined: Jun 5, 2011
  Messages: 4,598
  Likes Received: 2,408
  Trophy Points: 280
  Kikao cha CCM kilichokwisha muda si mwingi huko Dodoma kimenikumbusha mambo mazito sana aliyowahi kuyasema Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere mwaka 1995 katika moja ya vikao vya chama hicho, na ni moja katika ya HOTUBA ambayo sikumuona mwalimu akicheka wala kuleta mzaha, Mwalimu alikuwa serious kabisa na hapa tujikumbushe machache.

  Allisema.....Watanzania wanataka mabadiliko, wasipoyapata mabadiliko ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM, Watanzania kuna mambo mengi wanataka serikali ijayo iwafanyie. 1: Watanzania wamechoka na rushwa, tunatakiwa tumpate mgombea ambaye atapiga vita rushwa si kwa mdomo tu bali kwa vitendo na dhamira safi kabisa toka moyoni.

  2: CCM bado ni chama cha masikini kwa maana ya wakulima na wafanyakazi hivo tunataka tuendelee kushughulika na watu wetu, tushughulike kwa dhati na matatizo ya wananchi wetu katika hali yao ya uchumi.
  Mwalimu alitaka wajumbe wa halmashauri kuu wachague viongozi wanaojali matatizo ya watanzania, wanaojua umaskini wa watanzania na wanaokerwa na umaskini wa Watanzania.

  3: Lingine alizungumzia udini, akikemea kabisa suala la udini katika Nchi hii.

  Swali ninalojiuliza na wanajamvi mnisaidie, katika viongozi wa CCM waliochaguliwa huko dodoma jana ni nani hasa mwenye hizo sifa alizozitaja mwalimu? kama wao wanahonga ili kupata uongozi dhamira ya kweli itatoka wapi katika kukemea rushwa, kama wanahusika na ufisadi dhamira ya kweli ya kumtetea Mtanzania maskini ipo wapi ilhali wanatapanya kodi zetu kwa anasa na kujilimbikizia mali, CCM ya leo inaubavu gani wakujitapa kwamba ni chama cha mkulima na mfanyakazi na kinawajali.......Binafsi sijaona.

  Udini ndio usiseme, maana imekuwa kama ni fashion sasa kujuana dini, uvumilivu hakuna tena, kama watu wanadiriki kuchoma nyumba za ibada nini kingine kimebaki? tafakari.

  WITO WANGU KWA CCM: KAENI CHINI MJITAFAKARI UPYA, MLIPOTOKA, MLIPO NA MNAPOKWENDA, JE BADO MNASTAHILI KUIONGOZA HII NCHI? NA WAKATI MNAJITAFAKARI TAFADHALI WAACHENI WATANZANIA WATAFUTE MABADILIKO KWINGINE.
   
 2. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  riziwani kikwete.
  salma kikwete.
  ...........kikwete
  ..........kikwete.
  jakaya mrisho kikwete.

  this is my hero family 2012.
   
 3. m

  multmandalin JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 8, 2012
  Messages: 1,951
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Yeeees! Hayo maneno ndo Ring tone yangu, kwa taarifa yale maneno ya Mwalimu yaliishia palepale siku ile, kwani sasa watanzania wamekikosa ndani ya CCM wamegunduwa kipo nje ya CCM.
   
 4. Root

  Root JF-Expert Member

  #4
  Sep 27, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,326
  Likes Received: 13,032
  Trophy Points: 280
  jf ilinisababisha nidownload speech za Nyerere za kule mbeya
  ukizisikiliza ziko na sense
   
Loading...