Watanzania Wanaongea Sana Kuliko Wakenya Na Waganda?

Haika

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,348
559
Kila mahali utakia watanzania tunasemana
'Mswahili bwana, maneno meeengi'
Je ni kweli, ina maana watanzania tuna maelezo mengi kuliko wenzetu?
Au tunaongea kuliko matendo?
Au ni msemo tu wa kiwahili.
 
Waswahili siyo domain ya Watanzania tu, Mombasa na Lamu kuna Waswahili pia.

Kihistoria kuna swala la Kiswahili ambacho kimewaunganisha Watanzania na kujenga camaraderie ambayo haipo katika nchi nyingine yoyote ya East Africa.Kwa hiyo ni rahisi kwa watu kujichanganya na kuongea bila hata haja ya ku break the ice.Kenya na Uganda to an extent bado kuna mambo ya ukabila, hawajui Kiswahili (a unifying language) vizuri, na hata kiingereza chenyewe hawakijui kama wengi tunavyofikiri kwa hiyo wanakuwa wamegawanyika zaidi.

Pia kuna element ya kupikwa kisiasa, wakati wenzetu wanasoma au kufanya biashara sana, Watanzania watu wa kupelekwa pelekwa kisiasa sana, kuanzia hotuba za mchonga mpaka usanii wa wanasiasa wetu wa leo.Kenya na Uganda interest katika siasa haikuwa kama Tanzania, ironically katika kipindi hiki cha mageuzi Kenya wanatupita katika kuleta mabadiliko, probably kwa sababu "hawakupikwa" kisiasa na KANU kama watanzania "walivyopikwa"
na TANU/CCM.

Wakati Waingereza wanaandaa Kenya kuwa "The Australia of Africa" Watanzania walishajua kuwa wao walikuwa "watoto wa kambo" kutoka kwa Mjerumani, hili lilifanya Watanganyika then na Watanzania baadaye ku focus inward and hence bonding with each other under Nyerere wakati kina Kenyatta wanajenga a classic market oriented outward looking society.The proverbial gift and the curse.

Halafu tanzania ni nchi kubwa yenye makabila zaidi ya 120 bila ya kuwa na tatizo la tribal dominance.Ni kama nyumba yenye watoto wengi, naturally watoto wa nyumba yenye watoto wengi watakuwa wachangamfu/ waongeaji zaidi kuliko watoto wa nyumba yenye watoto wachache.
 
Kweli sisi ni wachangamfu katika maneno.

Ona blog yetu ya jamii ilivyoshamiri maoni na mapendekezo na hisia.

Ni kweli Pundit, sisi tunaongea kwanza kabila linajulikana baadae sana, na wala si ishu ya kusimulia,
Ila jamani jamani siasa!!!, mpira!!!

ata kazini kujieleza kwanini kazi haijafanyika, hakuna mtu wa kutupiku,

Si unaona wanasiasa wetu? au raisi wa sasa na aliemtangulia, anageuza hadithi mnabaki mnamtazama, anaondoka bila kutupa tunachotaka.

Angalia pepa zetu kwa mahirika ya kimataifa, zote bomba, mpaka wakielezwa jinzi tunavyoshughulikia mafisadi wanaelewa kabisa na kuridhika bila kujijua ni changa macho.

Mungu atupe nini???
 
Angalia pepa zetu kwa mahirika ya kimataifa, zote bomba, mpaka wakielezwa jinzi tunavyoshughulikia mafisadi wanaelewa kabisa na kuridhika bila kujijua ni changa macho.

Haika umezibuka!
 
Kila mahali utakia watanzania tunasemana
'Mswahili bwana, maneno meeengi'
je ni kweli, ina maana watanzania tuna maelezo mengi kuliko wenzetu?
au tunaongea kuliko matendo?
Au ni msemo tu wa kiwahili.

Very interesting fact!!....., lakini thats the fact, nipo ktk instution flani within maziwa makuu, ila wabongo utatujua tuu kwa kuongea sana, uchangamfu, ushirikiano na umoja flani!!

Of coz in comparison sisi tuko juu zaidi ya wenzetu, ingawa in other side ina side effect yake lakini is good as far as national sovereignity is concerned!!
 
Sikubaliani na hili, waganda nao wanaongea sana, hata Wakenya pia.
 
Sikubaliani na hili, waganda nao wanaongea sana, hata Wakenya pia.

Not really kaka!!

Kama nilivyoanisha hapo juu, nipo inst. ambayo tuko na kila ina ya taifa esp from across the region, lakini wabongo bwana ni nomaaaa!!
 
We are very articulate and charming as compared to our neighbours....:) Ndiyo maana tunaongea sana kuliko wao.
 
Not really kaka!!

Kama nilivyoanisha hapo juu, nipo inst. ambayo tuko na kila ina ya taifa esp from across the region, lakini wabongo bwana ni nomaaaa!!

Sifa kubwa ya wabongo sisi ni uvivu, sidhani kama ni kuongea. Sikukatalii kuwa watanzania wanaongea, lakini sidhani kama we the loudest people in the region.
 
Sifa kubwa ya wabongo sisi ni uvivu, sidhani kama ni kuongea. Sikukatalii kuwa watanzania wanaongea, lakini sidhani kama we the loudest people in the region.

Fisadi Mkapa alikuwa anapenda sana kututukana Watanzania kwamba ni wavivu. Kuanzia katikati kukazuka mtindo wa Watanzania wengi kutafuta kazi nchi za nje hasa katika nchi za magharibi. Watanzania hao walionekana ni wachapa kazi hodari hawana malalamiko na kujijengea sifa kubwa katika nchi hizo za magharini na hata waajiri kuanza kuulizia kama kuna Watanzania wengine wenye qulaifications kama hizo wawachukue ili wakachape mzigo.

Sifa hizo za Watanzania waliozaliwa, kulelewa na kusoma Tanzania elimu yao ya msingi hadi undergraduate degree zilipofika serikalini. Watanzania wakaanza kuhoji kama Watanzania ni wavivu inakuwaje hawa walio nje wanamwagiwa sifa kem kem tena toka katika nchi za dunia ya kwanza ambazo watu huchapa kazi mtindo mmoja? Je, kulikoni? Hapo ndio fisadi Mkapa akaacha kututukana kwa kutuita Watanzania wavivu maana kulikuwa na ushahidi unaonyesha kwamba Watanzania si wavivu kama wakipewa mazingara mazuri ya kufanyia kazi na mishahara mizuri inayoendana na gharama halisi za maisha.

Watanzania siyo wavivu hilo nitalikataa siku zote, ila wanakatishwa tamaa na viongozi wezi, mafisadi walioweka mbele maslahi yao binafsi badala ya yale ya Taifa. Viongozi hawa wako tayari kumlipa mzungu mshahara hata wa $4,000 kwa mwezi kwa kuwa tu ni mzungu pamoja na kuwa hana qualifications kama za Mtanzania au uzoefu kama wa Mtanzania, mfano ni TANESCO ambapo fisadi Mkapa baada ya kuwaondoa wabongo ambao waliokuwa na qualifications za hali ya juu na uzoefu wa muda mrefu katika kuendesha shirika la umeme, aliwaweka makaburu ambao walikuwa hawana qualifications zozote katika umeme lakini wakalipwa mishahara na marupurup manono na waliyoyafanya pale TANESCO wote tunayajua. WATANZANIA SIYO WAVIVU TUSIPENDE KUJIDHALILISHA!!!
 
Fisadi Mkapa alikuwa anapenda sana kututukana Watanzania kwamba ni wavivu. Kuanzia katikati kukazuka mtindo wa Watanzania wengi kutafuta kazi nchi za nje hasa katika nchi za magharibi. Watanzania hao walionekana ni wachapa kazi hodari hawana malalamiko na kujijengea sifa kubwa katika nchi hizo za magharini na hata waajiri kuanza kuulizia kama kuna Watanzania wengine wenye qulaifications kama hizo wawachukue ili wakachape mzigo.

Sifa hizo za Watanzania waliozaliwa, kulelewa na kusoma Tanzania elimu yao ya msingi hadi undergraduate degree zilipofika serikalini. Watanzania wakaanza kuhoji kama Watanzania ni wavivu inakuwaje hawa walio nje wanamwagiwa sifa kem kem tena toka katika nchi za dunia ya kwanza ambazo watu huchapa kazi mtindo mmoja? Je, kulikoni? Hapo ndio fisadi Mkapa akaacha kututukana kwa kutuita Watanzania wavivu maana kulikuwa na ushahidi unaonyesha kwamba Watanzania si wavivu kama wakipewa mazingara mazuri ya kufanyia kazi na mishahara mizuri inayoendana na gharama halisi za maisha.

Watanzania siyo wavivu hilo nitalikataa siku zote, ila wanakatishwa tamaa na viongozi wezi, mafisadi walioweka mbele maslahi yao binafsi badala ya yale ya Taifa. Viongozi hawa wako tayari kumlipa mzungu mshahara hata wa $4,000 kwa mwezi kwa kuwa tu ni mzungu pamoja na kuwa hana qualifications kama za Mtanzania au uzoefu kama wa Mtanzania, mfano ni TANESCO ambapo fisadi Mkapa baada ya kuwaondoa wabongo ambao walikuwa na qualifications za hali ya juu na uzoefu wa muda mrefu katika kuendesha shirika la umeme, aliwaweka makaburu ambao walikuwa hawana qualifications zozote katika umeme lakini wakalipwa mishahara na marupurup manono na waliyoyafanya pale TANESCO wote tunayajua. WATANZANIA SIYO WAVIVU TUSIPENDE KUJIDHALILISHA!!!

Bubu naomba niondoe hiyo statement ya uvivu! I agree with your analysis kuwa uvivu wetu unachangiwa na kipato kidogo. Lakini ukweli unabaki kuwa ukiingia kwenye ofisi hasa za umma utasikitika jinsi ambavyo kazi hazifanyiki. Ukimwagiza mtu kufanya kazi ambayo ni ya nusu saa ataifanya baada ya wiki moja na sababu nyingi ambazo hazina miguu wala kichwa! that is exactly what I meant. Na manifestation ya uvivu ni kuwa na maneno meengi, hasa wakati wa kazi.
 
Kwanza naomba niulize hivi mswahili ni mtanzania? kwa muono wangu hakuna mtanzania ambaye ni mswahili ila kiswahili ni lugha yetu wote bwana. Hivyo statement sahihi ilitakiwa kuwa 'watanzania bwana wana porojo nyingi (lol).
Pili ninaungana na wale wanaosema kwamba maslahi ni set back ya watu wengi kufanya kazi kwa sababu hakuna mtu ambaye yuko tayari kuona ana toil na wengine wanafaidi. Hii inakatisha tamaa sana.
Sijui kama umeshawahi kugundua kuwa ni hapa Tz tu ambako mtu huwa nafanya kazi kweli kweli tena katika professio yake lakini malipo yake kwa mwezi tu hayakidhi hata kulipia house rent. Sasa tuseme ukweli ni nani atakuwa na hamu ya kufanya kazi?
Angalia wanasiasa jinsi wanavyolipwa a lot of money na kwa sababu hiyo wanafanya kazi usiku na mchana ili wasiondoke katika post zao. Wako tayari hata kutumia ndumba ili waendelee kuwapo katika post hizo. Na hii imesababisha watu wote wafikiri kuingia katika siasa na kuacha taaluma zao. Kwa hiyo hata hao wanaosema sisi tuna kiswahili murefu ni wale wale walio na ka element ka siasa tu ndani. We mpe mtanzania pesa nzuri uone anavyochapa kazi. Msiwatuhumu bure wakati hawalipwi kipato poa.
 
Mkuu hebu fafanua hao wabongo unaosema noma hapo kazini kwenu,hawafanyi kazi au wanakuja kazini saa sita,niambie wanafanya nini hasa!!!! Kama wanaongea sana na tija inapatikana basi waache waongee mpaka wachoke.
 
Wakuu,

Naomba nitofautiane na maelezo mengi yaliyotolewa na wenzangu, kuhusu hii dhana ya kuwa Watanzania wanaongea sana kuliko Wakenya na Waganda. Dhana hii ni ya zamani sana na ilisikika ikisemwa na wenzetu wa Kenya hususan askari polisi wao.

Askari polisi wa Kenya, wakati huo walikuwa wanapenda sana kuhongwa na dau la hongo yao kwa kawaida ilikuwa Shilingi 20/- (ishirini). Makosa makubwa yaliyokuwa yakiviziwa nao yalikuwa ya uvunjwaji wa sheria za uendeshaji magari barabarani na ya wale waliokuwa wakienda haja ndogo kando kando ya barabara au vichochoroni.

Hii ilikwenda mpaka watu wakawa wanatembea na noti za shilingi 20/- mifukoni au wanazipachika kabisa katika leseni zao. Sasa wenyewe kwa wenyewe wa Kenya, walikwisha zoeana. Wakikamatwa tu, kama ni yule wakukojoa anatoa pesa mara moja na shauri linakwisha. Kama ni dereva, akiulizwa leseni yake akimpa polisi. polisi anaifungua, anatoa ile shilingi 20/- iliyopkunjiwa humo ndani ya leseni, mashauri yanajiishia.

Sasa basi, inapokuja zamu ya kukamatwa mtu wa Tanzania, awe aliyekuwa na kosa la kukojoa au dereva, anakuwa na maelezo mengi sana ya kujitetea. Nao hao polisi wa Kenya wanakuwa hawana muda wa kusikiliza utetezi. Wanachotaka ni kuiona noti ya shilingi 20/- inatolewa. Wakaja na huu msemo, "hii mitu ya Tanganyika ina midomo mireefu sana." Na maanake ni kwamba, "unasema sana, bila kitendo (cha kutoa hongo)." Unapoteza muda. Kwa kukusikiliza wewe, yeye angeshakusanya shilingi ishirini, ishirini zaidi ya moja.

Hali hii imeifikisha dhana hii hapa tulipo, "tunasema sana kuliko tunavyotenda." Dhana hii si suala la uchangamfu, ukabila au kujua sana lugha ya Kiswahili. Tumeburuzwa sana na TANU/CCM na tunaendelea kuburuzwa hadi hii leo. Tunafanya nini katika kuirekebisha au kuiondoa kabisa hali hiyo zaidi ya kusema sema tu?

TANU/CCM imetufikisha kwenye mikasa yote hii, sijui Richmond, BoT, EPA na mingine mingi sana tuijuayo na tusioijua. Tunafanya nini zaidi ya kusema sema tu? Mpaka sasa tumepewa sifa nyingine mpya. "Watanzania wagumu wa kuelewa na wepesi wa kusahau."
 
Kuongea kwa WA TZ tusikubeze. Kumbukeni kwa wale waliopitia JKT ni hayo hayo maongezi na stories nyingi zilitufanya tuwe kitu kimoja na kumaliza salama ambapo mwisho wa yote tumejenga 'social network' kali sana.

Nimefanikiwa kukaa na Wakenya huko ughaibuni, wao wakikutana kama sio kabila moja mahusiano yanaishia hapo hapo. Wa tz, mpaka ujue kule mwenzako anakoishi na ikiwezekana mnasaidiana kutatua yale yanayowakwaza. Ebu tujivunie hili. Mtaniunga mkono kwa wale ambao wamekaa nje ya tz na kuona hali inakuwaje kwa mfano, Muha kukutana na Mmakonde pale Dussedorff, urafiki utaanzia hapo hapo mpaka nyumbani na familia zao kupitia kwao wenyewe zinakuwa na uhusiano mzuri tu. Hii ni zawadi Mungu aliyotujalia tusiige eti Waganda na Wakenya wanavyofanya acha wafanye hayo wanayoyafanya. Kumbukeni Wakenya wanatamani sana mshikamano wetu, utasikia wakisema kwa nini tusiwe na mshikamano thabiti kama wa watz? ukitembelea tovuti yao ya 'kazi afrika' utakuta kuna maneno ya kutamani watz tulivyo.

Kuhusu kiingereza' si waganda si wakenya au watz wanaongea kwa ufasaha lugha hiyo. Lakini wote tukiongea tunawasiliana vizuri tu bila matatizo.Labda yale tunayoyaona ni mazuri kutoka kwa majirani wetu hawa tuyachukue lakini sio life style yao tuilete kwetu tutakuwa tumefanya makosa.

Watz nawafagilia wawawawawawa.
 
Kwa wa Tz waio nje uongeaji ni jambo zuri la kuiga,
je kwa walio kazini, wenye maneno mengi kama wanasiasa wetu lakini utekelezaji hakuna?
na ukimuuliza anamaneno mengi tu ya kukujibu, kwa nini hajatekeleza.
Kama Hawa mafisadi, hebu kumbukeni shairi zuri la kusisimua la lowasa kuhusu viongozi jasiri na thabiti.
hadi inafika wakati ukiambiwa kitu na mwenzio huwezi kuamini kabisa hadi ushuhudie mwenyewe au uhakikishe mwenyewe kwa kushika mkononi ulichoahidiwa.
Hebu someni pepa za watanzania, na ziko nyingi sana, za kuombea misaada, well put together, lakini ukwli hapo utakuta ni asilimia 15 tu. nyingine ni upambaji tu.
Hotuba za ukimwi, wakati wakitoka majukwaani wanaanzana wenyewe.
NGO, zilizoko Dar, zinapata ripoti nzuri kabisa za mikoani na wafadhili wanakubaliana nazo.
 
Wether or not there are truths in stereotypes is debatable, but let me say i know a few tanzanians, maasais here in kenya and they are some of the most hardworking people ive met. They are not that educated but they make more than some of the educated kenyans
 
Kuongea saana kwetu kumetusaidia pia kuepuka KUTWANGANA kirahisi kama ilivyo kwa WENZETU. Ni WAANCHARI, WARENCHOKA na WAKIRA kule Tarime ndio wanaotuangusha ambao wana uhusiano wa karibu sana na WAKENYA. Kuongea sana kunaepusha mengi na kunaimarisha sana MAHUSIANO. Hatupaswi kulionea HAYA hili.
 

...FACT; hata humu kwenye hii mada kuna watu wana "mineno mireeeeeeeefu!"


:D
 
Back
Top Bottom