Watanzania wanaoishi nje wasakwa kuchangia uchumi wa nchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania wanaoishi nje wasakwa kuchangia uchumi wa nchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MkamaP, Oct 16, 2012.

 1. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #1
  Oct 16, 2012
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Silima Pereira (kulia), akipeana mikono na Balozi wa Jumuiya ya Ulaya hapa nchini, Filberto Ceriani Sebregondi, wakati wa mapumziko ya chai, kwenye ufunguzi wa warsha ya siku mbili kujadili njia bora za kutunza kumbukumbu na Sera ya Uhamiaji jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mwakilishi kutoka Shirika la Kimataifa linaloshughlika na masuala ya Uhamiaji (IOM), Damien Thuriaux na Balozi wa Uswis nchini, Olivier Cheve.

  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Idara ya Uhamiaji imeandaa mpango wa kupata idadi ya Watanzania waishio nje, idadi ya wahamiaji nchini pamoja na mchango wao katika kuinua uchumi wa nchi.

  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima, alisema jana kuwa mkakati uliopo sasa ni kujua idadi ya Watanzania waishio nje ya nchi wanachangiaje kuongeza uchumi wa chini kwa kuleta fedha za kigeni nchini.

  Alisema kuna Watanzania wengi wanaishi nje ya nchi huku wakihudumia familia zao nchini kwa kuwatumia fedha za kigeni na mahitaji mengine kila siku.

  "Lazima tujue wahamiaji wanaichangia katika nchi yetu kwa kiasi gani, kuna mapato mengi yatokanayo na Uhamiaji hivyo yatupasa kufahamu ni kwa kiasi gani," alisema Silima.

  Alisema, waandishi wa habari pamoja na wanasiasa wanapaswa kupewa elimu juu ya masuala ya uhamiaji na uhamaji kwa kuwa wengi wao hawafahamu faida zake.

  Naye Kamishna wa Fedha na Utawala Idara ya Uhamiaji, Piniel Mgonja, alisema wataalam kuna waliokwenda nje ya nchi kujifunza masuala mbalimbali kuhusu uhamiaji na uhamaji. Aidha, alisema wataalamu wa takwimu wanafuatilia kujua idadi ya Watanzania walioko nje.


  CHANZO: NIPASHE
   
 2. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #2
  Oct 16, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,187
  Likes Received: 704
  Trophy Points: 280
  Visa zao zinatusumbua,lazima tuwe matajiri ndio watupe au wasomi,wakati wao hata ma homeless wanakuja tz kutembea kuishi,kuomba ajira,kwa nini sisi watz tuwe na vikwazo ? Wakati EU na Amerika wameweka vitega uchumi vyao katika migozi na URENIAM,wanatunyonyaaa lakini kwenda kwao ni big deal ? HEE ETItunaenda kushangaa mijumba mirefuu,sio ivyoo bongo ajira hakuna,hata kama msomi,ukiwa msomi huna kitu mfukoni,ajira mpaka uwe na ndugu katika kampuni au serikalini,au ujiajiri mwenyewe uuuze njugu au mitumba,mashamba serikali wanatupokonya na kujimbakizia wao.

  Umasikini ni viongozi wetu ambao wanatuzalilisha kwa wageni,na pia ubinafsi.
   
 3. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #3
  Oct 16, 2012
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Mkuu
  Kama hakuna ajira kwanini Tanzania isiwatafutie wasomi/ wanafunzi iwa export ulaya ili wawe na wa Tanzania wengi wanaoleta fwedha za kigeni. Nchi zingine za hasa za asia ndo zinafanya hivyo.

  Harafu wawasake je, huko waliko kama hawana uraia wa nchi husika ni ngumu kupata kazi nzuri ya kiwango cha mhusika. Wakitaka fwedha za kigeni wawaruhusu uraia wachukue kazi nzuri. Wao wanataka tu fwedha ila hawataki kumjengea hata mazingira basics ya mhusika kwa kumruhusu kukamata uraia mwingine.
   
 4. M

  Mazindu Msambule JF-Expert Member

  #4
  Oct 16, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 4,317
  Likes Received: 1,494
  Trophy Points: 280
  Wazee kwa Ku-copy na ku-paste, hivi hii siimetolewa Rwanda kwa Kagame? mara baada ya Kagame kunyimwa misaada na nchi zilizoendelea aliwaomba Wanyarwanda waishio nje ya nchi kuchangia bajeti ya nchi yao, waliitikia mwito huo na Rwanda imekusanya pesa nyingi tu za kuendeshea nchi yao.

  Naomba nitoe changamoto kwa hawa viongozi wetu, WanyaRwanda wame respond kwasababu wanajua serikali yao ina nidhamu ya matumizi ya pesa za nchi, pesa nyingi inaelekezwa kwenye maendeleo na yote ni kwaajili ya wananchi, hapa kwetu sisi kama ni matumizi ya maana basi ni kulipana posho tu za vikao ambavyo hata havina tija, nawashauri enyi Watanzania mlioko nje msitoe ushirikiano kwa hili, angalia safari za mweshimiwa, hazina tija yeyote, Hospitali ni issue, hivi tunavyo ongea, kuna Hospitali za serikali hazina hata sindano, vitu vinavyo uzwa just Tsh 50/= tu, madaktari waligoma ili wapewe vifaa vya kazi, wakaishia kuwa Ulimboka, leo tunaambiwa spika wa Bunge yupo India kwa ajili ya ku-check afya yake, what kind of shame is this?

  Nina uhakika, kama pesa tulizo nazo tukizitumia kwa matumizi yenye tija, wala serikali haiwezi kuzitolea macho pesa za hao Diaspora au hata za NSSF/PPF.
   
 5. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #5
  Oct 16, 2012
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Mkuu
  Nafikiri unajua hata unapotuma fwedha kwa kaka/dada tayari umeshangia uchumi wa nchi. Hivyo ningewashauri serikali badala ya kulia lia na hawa watanzania kiduchu. Inge export watanzania wengine wengii wa kutosha.
  Serikali ni rahisi sana ku export watu, mkisha wa export mnawapa mwongonzo. Mfano,
  A. kwa kipindi cha masomo yako hakikisha unaji legalize na system husika
  B.Hakikisha shule unamaliza
  Nk NK
  Harafu watoe uraia wa nchi mbili, baada ya miaka 5 tu fwedha za kigeni zitakuwa zinamiminika zenyewe, wala haitahitaji kuwasaka.
   
 6. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #6
  Oct 20, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Hao washenzi kweli. Yaani wamepewa nchi yenye maziwa na asali wakaigawa kwa mafisadi wa kigeni halafu eti wanataka walioko nje wachangie ili wao wale siyo? Ukitaka kusafiri nje kama siyo mwenzao wanakuwekea kila vikwazo kupata pasi ya kusafiria. Ukishapenya ukafanikiwa hao hao waliokutilia mtima nyongo eti wanataka uwekeze Bongo wahomole kama wanavyofanya madini na kodi za makapuku. Mwenzenu simo baba yenu.
   
 7. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #7
  Oct 20, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Orwellian orangutans and obscene Ottoman-like ombudsmen.

  Watu wamekimbia upuuzi wa serikali, bado mnataka kuwafuatilia ili iweje?

  Wengine hatutaki kufuatiliwa na serikali dhalimu kwani hatuna imani nayo. Kama msaada si washasema unatolewa moja kwa moja kwa ndugu jamaa na marafiki? Sasa serikali inataka nini?

  Na waende wanaotaka kujiandikisha, mie naona uchu na uchuro tu.
   
Loading...