Watanzania wanaofanya PHD ujerumani hali zao mbaya sana na wanahitaji msaada haraka

europe yote...watanzania wana compllicate wenyewe elimu yao.

taratibu mazee,usilete zileee za o-level/form six tulikuwa tunaongopeana eti elimu ya bongo form six sawa na ya chuo kikuu ulaya,mweh!
babu kuna shule zinatoa dozi mpaka utajuta kwanini uli enroll
 
  • Thanks
Reactions: Obi
taratibu mazee,usilete zileee za o-level/form six tulikuwa tunaongopeana eti elimu ya bongo form six sawa na ya chuo kikuu ulaya,mweh!
babu kuna shule zinatoa dozi mpaka utajuta kwanini uli enroll

ugumu wa kitu una depend na kichwa chako mwenyewe,elimu ya bongo unasoam huku maprofesa wanakutishia kukufelisha.
you cant compare it with ED europe
 
Hivi tunaye kiongozi ambaye hakusomeshwa na serikali?

Just curious...
 
Nchi isiyo na vipaumbele warudi nyumbani tushirikiane kubadilisha uongozi nchini hakuna njia mbadala hata wakipewa leo zitabaki za kuunga unga na wataendelea kuishi kwa kudhalilika
 
ugumu wa kitu una depend na kichwa chako mwenyewe

hapana mkuu,siyo kichwa chako tu.Inategemea pia mazingira ya shule,walimu,vitendea kazi,kozi unayosomea,muda nk ndiyo maana ukasema wewe mwenyewe kuwa elimu ya ulaya ni rahisi sana kuliko ya bongo
wewe ulisomea kozi gani,nchi gani na kwa lugha zipi?nway acha niache ubishi,maybe ur right,inawezekana kweli shule yako ilikuwa rahisi sana
 
Mkuu Ivuga, labda nikung'ate sikio kidogo maana nina kauzoefu kwenye hizo anga.
Kama Kiwewe alivyosema box siyo tatizo.. ila shule imesimama!! Nilimwelewa zaidi.
Maprofesa wengi kule hawana longolongo katika taaluma..na usipokuwa mjanja utajikuta unalala maabara mara nyingi tu.
Nilikuwa level za chini hivyo tuliweza kuibia muda na kuingia mtaani kubeba box maana allowance ilikuwa kiduchu..
Kwa bahati mbaya chuoni wakagundua hilo. Ilibidi atafutwe mtu maalum ambaye kazi yake ni kutumonitor waswahili kutwa nzima!!. na ikawa ndiyo mwisho wa box!!
Wadochi wanachukia sana mambo ya box, kwao ni wastage of precious time!! muda ambao unatakiwa kuutumia zaidi kufikiria tafiti zako especially kwa wanaofanya level za juu kama PhD.
Hivyo mtu kugeneralize kuwa jamaa wanacomplicate elimu yao anakuwa hajawatendea haki kabisa maana mazingira ni tofauti kati ya nchi na nchi, au hata eneo kwa eneo.
Isitoshe, mbongo afanye complication dhidi ya nani huko ujerumani? Wanachohitaji ni survival!
Complication zipo sana hapa hapa nyumbani..
 
Poleni sana kwa mateso ya kucheleweshewa allowances zenu. Kuna la kujifunza hapo, ukizingatia nyie ni lecturers back home. Mateso mnayoyaona huko, na mishahara yenu inaendelea kuingia bank, walau na yale mashamba yenu mnakofuga vitimoto yanaendelezwa yanasikitisha. Wafikirieni sasa watoto wa wakulima wanaocheleweshewa allowances zao na bodi kwa sababu hizo hizo za kizembe. Natumaini Drs mkirudi nyumbani, mtakuwa na uelewa zaidi wa migomo ya wanafunzi na hivyo kutonuia kuwakamata pindi wakiwa kwenye 'crush programmes'
Poleni sana wakuu.
 
Poleni sana.

Nina ndugu yangu anafanya PhD kwa mpango huo pia mbona hajatwambia?

Mimi sina hizo degree lakini naweza kusema kwa ujasiri HAMJUI kujenga hoja. Lugha ya watu mmetumia huku makosa sarufi na muundo mengi tu.
Ni wazi hii barua imendikwa na mtu mmoja, unajaribu kutumia misamiati ya kwenye `ripoti`.

Ndani ya miaka miwili mtarudi na PhD zenu kwa ujengaji hoja duni kama huu....dalili ya mvua....

Samahani nia sio kuwakwaza lakini

RealMan tunashukuru kwa kutukosoa. Kwanza napenda nikueleze hatujaja kusomea lugha, kama ni lugha wengine tunafanya masomo yetu kwa Kijerumani. Pili tulitaka ujumbe ufike kwa wakuu wetu sehemu za kazi. Sidhani kama wao hawataelewa kama ilivyotokea kwako. Huyu msamaria mwema aliyeiweka humu alifanya hivyo ili kuhalalisha taarifa yake, lakini haikuwa maalumu kwa JF members. Nakutakia kila laheri ndiugu yangu.
 
Wanafunzi wengi wa phd wakiwa ulaya wanadharau kazi za box wakidhani wao ni high class hasa watanzania.....haiwezekani mtu ukae hapo nchini mwaka mzima au miezi sita ushindwe hata kutafuta kazi ya gazeti ya kufanya jumapili au siku za katikati hata tatu tu.......ndo hvo mvumilie tu hadi serikali itakapowasikiliza!! poleni

Siyo kweli Mrembo by Nature. Tungepata hiyo nyfasi tungefanya. Naomba tusipende kulinganisha mambo yasiyolinganishika. Ungelifahamu nature ya hii program ungekuwa na mwanga mzuri na wala usingetukosoa kwa hili.
 
mimi ninavyojua elimu ya ulaya ni rahisi mara 100 kuliko ya Tanzania ..ulaya kila kitu kipo simple and clear..huyu jamaa labda anafikiri kuwa wote humu JF ni wanafunzi ama wote tupo tz

Nikweli elimu ya Tz inaweza ikawa ngumu zaidi ya mara 100 kwaajili ya kukosa facilities na access ya materials. Ila urahisi huo siyo kwenye substance ya shule. We need to publish in higher impact journal paper kadhaa ili turuhusiwe kuandika kitabu cha kukamilisha masomo. Nafikiri kwa ufahamu wako mkubwa unaelewa kazi iliyopo, maana hapo anayesimamia PhD yako si supervisor wako tu bali hata pannel ya reviwers wa different journals katika hizo paper kulingana na research studies ulizofanya.
 
europe yote...watanzania wana compllicate wenyewe elimu yao.

Hongera sana Saint Ivunga, inaelekea wewe PhD yako uliisomea nchi zote za Europe mpaka ukapata uzoefu huo mkubwa wa kujua kuwa Watanzania wanacomplicate wenyewe. Tunashukuru kwa kutukosoa.....
 
wacha kuwapa pole walio dar wasiolipwa ukawape pole wa nje ya nchinani kawatuma waende huko kwa ni PHD udsm Muzmbe azipowaachen wafu wazike wafu wao jamani
 
mimi ninavyojua elimu ya ulaya ni rahisi mara 100 kuliko ya Tanzania ..ulaya kila kitu kipo simple and clear..huyu jamaa labda anafikiri kuwa wote humu JF ni wanafunzi ama wote tupo tz
Mkuu umenichekesha kweli kweli. Ni Ulaya ipi unayosema shule ni rahisi mara 100 ya Tanzania? Au unazungumzia Ulaya iliyopo Morogoro mkuu?
 
title nimeona wanasoma PHD lakini habari yenyewe naona UZAMILI..phd=uzamivu
 
wacha kuwapa pole walio dar wasiolipwa ukawape pole wa nje ya nchinani kawatuma waende huko kwa ni phd udsm muzmbe azipowaachen wafu wazike wafu wao jamani

nahisi hujasoma mada na kuelewa ndiyo maana unatoa comment hiyo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom