Watanzania wanangoja kwa hamu kitabu cha Rais John Pombe Magufuli baada ya kustahafu!

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
5,031
2,000
Baada ya uzinduzi wa Kitabu cha Rais mstahafu Mzee Ben Mkapa cha,''My Life, My Purpose.''na kujaribu kuweka hadharani changamoto alizokutano nazo wakti wa kipindi chake kuna shauku kubwa ya watu kuja kuona kitabu cha Rais Magufuli baada ya kustahafu ifikapo 2025.

Mzee Mkapa ameandika kwa lugha ya kigeni yaani Kiingereza(Sijui ni kwanini). Kwa Magufli sina hakika kitabu chske atatumia lugha gani kati ya Kiswahili au Kiingerereza. Kutakuwa na shauku kubwa ya kuona Rais Magufuli ataandika nini katika Mafanikio na Mapungufu yake wakti wa kipindi chake cha Urahisi kwa akiweka bayana. Every Leader must have his/her own traits.His Strengths and Weaknesses in Leadership.

Katika miaka hii 4 ya Utawala wa Magufuli Watanzania wameshuhudia matukio makubwa ya kisiasa, kiuchumi na kiutawala. Kwa ujumla Watanzania katika awamu hii wameshuhudia kipindi chenye changamoto za kimaisha ambazo hawakuwahi kuzipitia wakti wa wamu zilizopita.

Utawala wa Magufuli umegusa maisha ya kila mmoja kwa namna moja au nyingine. Lakini pia nyanja karibu zote kuanzia Wafanya biashara, Watumishi wa Umma, Wanajeshi na Askari wa kawaida. Wakti Magufuli anaingia madarakani kuna watu walikuwa wakiishi kama Malaika walioko peponi na alipoingia tu akatangaza vita dhidi yao kwamba atawashusha toka peponi awafanye kuishi kama Mashetani na kwa hakika amefanikiwa.

Kwa sasa kuna Wafanyabiashara wachache sana wanaoweza kutengeneza faida kwenye biashara zao kutokana na mazingira kuwa magumu. Kuna Wafanyibiashara wamefunga biashara zao mazima. Kwa ujumla sekta binafsi imeathirika kwa sehemu kubwa maana karibu biashara zote ambazo zilikuwa zikifanywa na Sekta binafsi zimechukuliwa na Serikali yenyewe. Kwa ujumla sekta binafsi imepokwa biashara zake na kuchukuliwa na Serikali.

Kinachofanyika kwa sasa ni biashara kati ya Taasisi na Taasisi za Serikali. Kwa mfano kama kuna Mradi wa kujenga Jengo la Serikali kama Hospitali au Wizara hiyo kazi atapewa NHC au TBA badala ya kupewa Wakandarasi na hivo kupelekea Wakandarasi Wazalendo kukosa miradi ya kufanya hivo kubakia kupiga miayo mtaani bila ya kazi yoyote ya kufanya.

Je, JPM atayaweka haya wazi na mengineyo katika kitabu chake cha ''His Life, His Purpose'' mara atakapostahafu?
Ni swala la kusubiri.
 

lukindo

JF-Expert Member
Mar 20, 2010
8,487
2,000
Mzee Mkapa kwa upande mmoja amefanya vizuri sana lakini upande mwingine wa shiling ni msala kwa wengine.
Hii ni nchi ya amani na hata Mwalimu alitubu mambo mengi na kuweka wazi kuwa hawakuwa malaika.
Hopefully Mungu akipenda tutawekewa wazi huu uzushi wa sandarusi za escrow, trillion 1.5, utekaji nk kama mzee alivyoweka bayana issues za EPA, Pemba nk.
Mungu ibariki Tanzania
 

ostrichegg

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
8,117
2,000
Ili uweze kuandika wahitaji kuwa na uwezo wa kutulia na kutuliza akili. Upende kujisomea ili kupanua uelewa uwezo wa kuchanganua na kuchambua. HUYU wa sasa Inabidi asaidiwe sana awe 'counselled' ili aanze mapema kukusanya na kutunza kumbukumbu ili asijee akaendeleza kukumbuka visasi na ukomoaji tu.
 
Top Bottom