Watanzania wanahisi suala la kuitetea nchi haliwahusu bali ni la wanasiasa pekee

Nsam

JF-Expert Member
Oct 25, 2018
212
286
Narudia tena; tukidhani wanasiasa pekee ndio wenye jukumu lakujenga nchi yetu, basi TUTAHARIBIKIWA.

NI wajibu wa kila mmoja wetu kusimamia maendeleo ya nchi yetu. Tupigane kuilinda nchi yetu, wanasiasa wanatuchezea sana! Maisha yamekuwa magumu tukisema wanasema tunalalamika.
 
1. Maisha ni siasa.
2. Hakuna kufanya siasa hadi kipindi cha kampeni.

Kwani unateseka?
 
NI wajibu wa kila mmoja wetu kusimamia maendeleo ya nchi yetu. Tupigane kuilinda nchi yetu, wanasiasa wanatuchezea sana! Maisha yamekuwa magumu tukisema wanasema tunalalamika.

Ulianza kuhitimisha vizuri kuwa kila mmoja apambane, nadhani ungeishia hapo ila sio hapo mwisho unalaumu wanasiasa kukuhadaa.... labda kama uliamini ipo siku watakuletea ugali mezani.
 
Watanzania wanaridhika na utenda kazi wa Rais Magufuli

Wapo busy na shughuli za uchumi
Hawana muda wa kupiga porojo
 
Watanzania wana akili sana..wanajua wanasiasa wote siku hizi ni wasaka tonge...
 
Misingi ya hili ilibomolewa na siasa hadaa za vyama vingi. Hatukua tayari kisiasa kuingia kwenye mfumo huu. Enzi za mfumo wa chama kimoja watu walikua na uzalendo uliotukuka kwa nchi yao

Sasa hivi mapenzi ya vyama yamechua nafasi ya uzalendo. Maadhali mtu anatetea chama chake yuko tayari kuiuza nchi iwe kwa mabeberu au wakoloni mamboleo wengine
 
Back
Top Bottom