Watanzania wanafanyakazi nje ya nchi WALIPISHWE KODI pindi warudipo nchini

kupe

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
1,035
326
na hii inafanyika katika nchi nyingi mojawapo ni PHILIPINES mara warudipo katika nchi yao (HATA LIKIZO) wanapigiwa mahesabu pale airpot au border then wanalipishwa kodi ..... Na hii inawezekana hata Tanzania . Mtu yeyote anayefanyakazi anawajibika kuchangia uchumi wa nchi yake kwa kulipa kodi. Baadala ya kuwa tunalalamika tu kuwa nchi haina maendeleo.
 
na hii inafanyika katika nchi nyingi mojawapo ni PHILIPINES mara warudipo katika nchi yao (HATA LIKIZO) wanapigiwa mahesabu pale airpot au border then wanalipishwa kodi ..... Na hii inawezekana hata Tanzania . Mtu yeyote anayefanyakazi anawajibika kuchangia uchumi wa nchi yake kwa kulipa kodi. Baadala ya kuwa tunalalamika tu kuwa nchi haina maendeleo.
Watachukua Uraia wa nchi wanazoishi ili kukwepa kulipa kodi mara mbili.
 
na hii inafanyika katika nchi nyingi mojawapo ni PHILIPINES mara warudipo katika nchi yao (HATA LIKIZO) wanapigiwa mahesabu pale airpot au border then wanalipishwa kodi ..... Na hii inawezekana hata Tanzania . Mtu yeyote anayefanyakazi anawajibika kuchangia uchumi wa nchi yake kwa kulipa kodi. Baadala ya kuwa tunalalamika tu kuwa nchi haina maendeleo.

Pumba, unalipa kodi unakofanya kazi i.e. pale unapochuma ... ..... mbona hii nchi inapata kigugumizi kuwalipisha kodi wageni ambao wanapata mishahara ya kufuru wakati wafanyakazi wanaolipwa fedha za kuhesabu wanalipishwa kodi kubwa? Tanzania inachotakiwa kufanya ni kuto-renew work permits za wageni hadi pale watakapoonyesha wamelipa kodi kiasi gani na wananufaisha vipi pato la kodi kwa Tanzania vinginevyo wasiongezewe muda, hatuwezi kuwa na wageni wanaojilimbikizia faida kubwa bila kulipa kodi na hii isiwe kigezo cha kuona Watanzania walio nje ndio njia ya ku-balance umburukenge.


NB. Kwa waajiriwa wa serikali wanaopelekwa nje unaweza kufanya hivyo.
 
kama wewe ni mtanzania na unajiingizia kipato au umejiingizia kipato kutoka nje ya nchi basi unawajibika kulipa kodi kwa kipato ulichojiingizia. Kama wanavyolipa kodi watanzania wenzako wanaofanyakazi hapa nchini.
 
kama wewe ni mtanzania na unajiingizia kipato au umejiingizia kipato kutoka nje ya nchi basi unawajibika kulipa kodi kwa kipato ulichojiingizia. Kama wanavyolipa kodi watanzania wenzako wanaofanyakazi hapa nchini.

Serikali ina utitiri wa kusamehe kodi kwa wawekezaji, halafu mje kubanana kwenye hela yangu ninayohangaikia huku bila aibu wakati nakuja kujenga nyumbani kwendeni huko.
 
Hii ni sawa ila mleta mada umekurupuka mkuu......kwa nchi za wenzetu unalipa kodi ila sasa mwisho wa mwaka huwa kuna calculation ambazo zinfanyika unarudishiwa kiasi flan which they call tax return kwa kuwa may be hukukaa nchini more that I month consequently . Kwa tanzani nilimsikia membe akisema kitu kama hicho ila utekelezaji wake inabidi kuwa na system nzuri ya tracking za watanzania waishi nje na kufanya kazi.
 
hiyo kodi ni ya mizigo ninayoingia nayo au ni ya muda niliokaa huku? una uhakika gani kuwa nafanya kazi huku na nalipwa sh ngapi? will i tell the truth? najua una lengo zuri na nchi yako but tafuta mbinu nyingine. naona bora tutumie michango yao kimawazo na pia kuwapa post za maana kikazi wanaporudi nchini hii kidogo inaweza kuwavutia na sio kuwaibia hicho kidogo wanachopata huko. we unasubir fulan aende marekan akirudi umdai kodi ili mwanao asome? mtanzania amka!!
 
kwani wakija huku wanakuja na kila kitu kutoka nje? Kuanzia airport kila watakacho nunua, kuanzia vocha, teksi, gazeti, juice, maji, chakula watakacho kula, kila kitu, tayari wanakua wamelipa kodi ndugu yangu. Kama ameingiza mzigo wowote kutoka nje, lazima alipie kodi ispokua bidhaa zilizo samehewa kodi kama kumputers kamili n.k.

Au unataka turudishe kodi ya kichwa?
 
Ndio walipie kodi kipato wanachopata au walichopata. Mbona huku mama nitilie, wauza magenge, wafanyakazi kima cha chini wanalipa kodi kwa kipato walichochuma...... Why hao wasilipe? Wakiwa nje utawasikia wanalalamika eti nchi haina maendeleo..... Au wanapiga simu au email kuulizia eti vipi bongo siku hizi imeendelea eeh. Kulipa kodi ili kuijenga nchi hawataki
 
upuuzi mtupu. mnashindwa kukusanya mapato: bandarini, madini, gesi nk. alafu mnaleta uppuzi hapa.
 
Mleta hoja kwanini asijiendee Milembe mapema akapima maana inaonekana kama ni kichaa hiki ni babu kubwa. Kama viongozi wetu wataacha kuombaomba wakatulia nchini na kukuza uchumi na maisha yakawa na maana basi tutalipa. Ulipe kodi ili watu wachache waibe kutumia siyo? Huna adabu we kijana.
 
Tanzania inaokotwa kodi kibao tena bila mpangilio. Je hiyo kodi inakwenda wapi? Nchi haina shule, mahospitali, barabara, na mengine ya muhimu ambao ndiyo matunda ya kodi. Huko hao watanzania waliko wanalipa kodi na wanapewa huduma muhimu za kijamii. Hapa Tanzania watakuja kulipa kodi ya kitu gani wakati hakuna huduma hata moja muhimu ya kijamii iliyonyooka?
Ama kweli mtanzania ni mjinga wa kutupwa anayejilinganisha na mfilipino. Je unaujua mfuma mzima wa jamii ya kifilipino? Mashule yao yako wapi? Vyuo vyao vikuu vinatoa huduma na elimu ya aina gani ukilinganisha na shule za kata zinazoendeshwa kwa kodi hapa Tanzania. Wamama wanapoenda kujifungua wanalundikana kwenye chumba kimoja na kulazwa chini kama ilivyo mhimbili na hospitali nyingine zinazoendeshwa kwa kodi za watanzania? Je barabara za philipins zimepindika kama ilivyo barabara ya Rombo iliyofunguliwa na raisi juzi?
Je madaktari na waalimu wa huko ufilipino wanagoma kila siku kwa kusosa vitendea kazi? Ni wapi tuanzie kwa kujilinganisha na mataifa mengine hata hapa Africa tu kwa upende wa malipo na matumizi ya kodi?
 
Wailete tu tuanze kuzilipa halafu tuweze kuwauliza vizuri wamezifanyia nini na mchanganua wake, maana huko Bongo hawaulizigi kodi zao zinafanya nini.. wao ni kuchanga tu kila siku na kutokuuliza ndio kunakochangia ufisadi maana watu hawajui michango ya kodi zao zinafanya nini...inabidi wajue mgawanyo wa kodi zote katika huduma za afya, barabara..elimu. defence, na kila seheme ...sio kuchanga kila siku na kuendeleza ufisadi bila kujua matumizi yake kwenye safari za abunuasi...
 
Hata wakilipa zitaliwa na wajanja na hazitachangia kwenye maendeleo ya nchi hii so its no use!
upuuzi mtupu. mnashindwa kukusanya mapato: bandarini, madini, gesi nk. alafu mnaleta uppuzi hapa.
 
Ninavyoelewa mimi unalipia kodi sababu ya services the government offer you, why will I pay tax to a government ambayo hainipi chochote!
 
Naungana na wadau wengine kwamba inaweza ikawa ni moja ya njia ya kuiongezea serikali mapato; lakini jamani hivi serikali itakusanya shilingi ngapi kutoka kwa hao watanzania wanaofanya kazi nje? Kwa nchi yenye vyanzo vingi vya mapato vilivyofumbiwa macho kama Tanzania itakua ni uonevu kuwadai kodi watu walikwenda kujichanga changa huko ughaibuni na kurudi kufanya maendeleo nyumbani ilhali kuna wageni kibao hapa nyumbani wanafanyakazi bila vibali, na wenye vibali hawalipi kodi? Kwanza wangeongeza asilimia 1 tu kwenye kwenye ile 3% ya mrahaba (mrabaha???) hata wasingehitaji kudai hivi vikodi vidogo vidogo. Kama mwalimu alivyokwishawahi kusema kwamba nchi iliyofilisika hudai vikodi vidogo vidogo na kufumbia macho kodi kubwa na ndipo tulipo sasa.
Binafsi suing mkono hili kwani nikiangalia mfumo wa kodi wan chi hii unatia hasira sana. Mie mshahara wangu (serikalini) ni kama milioni saba kwa mwaka kabla ya makato, lakini nalipia kodi karibu laki 6 wakati kuna wafanya biashara ambao wana mitaji mikubwa tu wanalipa pengine chini hata ya nusu ya kiwango ninacholipa.
Pia kukosekana kwa uwazi na uaminifu miongoni mwa maafisa wa kodi pale uwanga wa ndege na mahali pengine ni kikwazo kikubwa. Kwa ndugu mliwahi kupita hasa huu uwanja wa DAR ni kero tupu jamaa wanakomaa wapewe pesa za rushwa hata kwenye vitu ambavyo c magendo. Sasa ukianzisha hiyo kodi c watatutia umasikini hawa?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom