Watanzania wanachagua viongozi wabovu au tume ya uchaguzi inawachagulia Watanzania viongozi wabovu?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Nikitolea mfano wa uchaguzi wa serikali za mitaa, je Watanzania ndio waliochagua viongozi waliopo au tume na wenye mamlaka ndio waliamua Nani atawale wapi na wapi?

Tukirudi kwenye uchaguzi mkuu, hivi Watanzania ndio wanaochagua wabunge, madiwani na Rais au tume ndiyo inachagua Nani awe Mbunge, rais na Diwani?

Kama tume ndiyo inaamua Nani atuongoze, upo umuhimu wa kuipa kazi tume ya uchaguzi kufanya manunuzi na maandaliz ya vifaa vya uchaguzi? Kwanini tusipige kura ya kupendekeza kila Jimbo bajeti yake ya uchaguzi utumike kununua madawati, kununua dawa na kujenge vituo vya kutolea huduma Kama hospitali?

Tukiamua Leo tuseme waliopo madarakani waendelee hadi 2025 lakini fedha za uchaguzi zitumike kwenye miradi inayoathiri jamii moja kwa moja nadhani tutaweka historia Duniani.

Ajitokeze Mbunge awasilishe hoja binafsi tukusanye maoni ya wanaotaka uchaguzi na wasiotaka uchaguzi then tusiotaka uchaguzi tukishinda tupewe fedha tukafanye maendeleo kusubiri 2025.

Kama mzee Mangula na umri wake bado ahamini kwenye uchaguzi huru bali anaamini kwenye kufuta vyama unategemea nani zaidi anaweza kumtangaza mtu wa chama kingine?

Kama polepole anaamrisha vyombo vya dola na wananchi wasimguse Mbunge au kiongozi yeyote wa chama tawala hata akikosea unategemea Nini?

Kufanya uchaguzi ni matumizi mabaya ya rasilimali fedha, tutumie fedha za uchaguzi kujenga vituo vya afya, kujenga shule, kuboresha miradi ya maji, kujenga barabara wakati tunasubiri hawa wazee wasiopenda kuona watu wengine wanatawala wanapumzika na kutuachia nchi yetu.
 
Wewe mwenyewe ulijionea kuwa watawala ndiyo "waliowasimika" kibabe viongozi wa serikali za mitaa wa chama cha CCM na haukufanyika uchaguzi wowote ulio huru na wa haki
 
Vyama vya siasa ndio wamekuwa wakileta wagombea wabovu waliotanguliza njaa zao mbele, wasiojua wajibu wao kwa jamii.

Ndio maana watu wanaenda kwenye chaguzi kuchagua vyama zaidi bila kujali ubora wa wagombea.

Pia ikumbukwe kuwa ili uwe kiongozi nchii hii kuanzia ngazi za chini hadi juu lazima utokane chama cha siasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom