BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,005
Mimi siwezi kuupigia kelele ufisadi. Na wala sijaneemeka na ufisadi. Mwenyezi mungu amenibariki kwa namna moja au nyingine kuweza kupata kipato cha halali kinachotokana na jasho langu
.
Na nimebahatika kusafiri nchi kadhaa na kuishi nchi kadhaa (sio kama najidai, maana mtaanza hizo) na nimeona karibu kila nchi ufisadi upo kwenye siasa tena wa hali ya juu.
Nipo states sasa hivi na ukisikia ufisadi uliopo jeshini la marekani, with evidence unaweza shangaa, ufisadi uliopo wall street, ufisadi unaofanywa na serikali za uingereza, China n.k ni humungous!!... but hey, it is what it is.
Kama wewe BAK ukiiba bilioni mia moja na ukaanzisha shirika lako la reli na kupatia wananchi usafiri wa maana toka Dar mpaka mwanza, mpanda, kigoma etc... mimi wala sitakumind, ni wapuuzi wanaoiba halafu hamna cha maana kinachoendelea ndio labda nitawamind, ila hiyo siyo kazi yangu.
Kama unataka research papers kuhusu democracy and opposition in Tanzania, unaweza kula nondo hii hapa chini, kutoka Georgetown University (kama mvivu wa kusoma just scroll to page 5, halafu nenda kwenye conclussion).
Tanzania's Missing Opposition ---
Utawezaje kuupigia kelele ufisadi na ilhali wewe ni mamluki/fisadi/anayeemeka kupitia migongo ya mafisadi? Huna mapenzi ya kweli na nchi yetu ndio maana madudu yanayofanywa na Serikali ya magamba inayoongozwa na Kikwete huyaoni.
Bahati mbaya sina jadi ya wizi hivyo wazo lako hilo chafu kwamba mimi nitaiba liondoe kichwani mwako. Nakula nguvu yangu na wala sijawahi kumdhulumu mtu au kufanya ufisadi na wala sifikirii kufanya hivyo na nashukuru Mungu kwa kunijaalia maisha mazuri.
Sihitaji kula nondo ya mtu yeyote yule mi Mtanzania banaa!!! Naifahamu vizuri sana nchi yangu. Naona unajibaraguza baraguza tu lakini maswali yangu kuhusu huu utafiti uchwara unayapiga chenga, kama huna majibu ni bora tu useme kwamba sina majibu badala ya kuendelea kuyakwepa.