Watanzania wana kiu kikubwa cha kuitoa CCM, Je tatizo ni nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania wana kiu kikubwa cha kuitoa CCM, Je tatizo ni nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zawadi Ngoda, Nov 23, 2011.

 1. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #1
  Nov 23, 2011
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Watanzania wana uchu mkubwa wa kuiona CCM inahama IKULU, na kukipisha chama kingine kuingia Ikulu. Haya ni majibu ya utafiti wa kile kikundi chetu binafsi "SONGAMBELE" amabacho kina wanachama na wataalam wake toka vyuo vikuu mbali mbali Tanzania.

  Aidha katika taarifa hiyo imeonyesha kuwa 70% kati ya watanzania walioshiriki katika utafiti huo ( 1 milioni) wanahitaji chama kingine zaidi ya CCM Kuingia Ikulu. Lakini walipoulizwa ni chama gani kati ya vyama pinzani walipenda kukiona kinaingia Ikulu, 65% walijibu "hakuna". Hii inaonyesha wazi jinsi vyama vya upinzani vilivyowakatisha tamaa watanzania toka katika ndoto yao ya kukiona chama cha upinzani kuingia ikulu.

  Nilipomhoji Prof Safari kuhusu matokeo hayo alisema yafuatayo "Sishangazwi wala kushitushwa na taarifa hiyo, angalia kampeni zao ni za kubabaisha tu, hakuna chama kinachokidhi matakwa ya wananchi. Hakuna chama cha upinzani katika vyama vikuu kilichoweza kuonyesha kuliweka wazi swala la umoja wa kitaifa. Vyama hivi aidha vimelaumiwa kwa kuendekeza ukabila au udini, na wameshindwa kujibu tuhuma hizo kwa kiwango ambacho watanzania watawaelewa. Kuwa na viongozi wa vyama ambao walishiriki au wanashiriki katika nyadhifa za taasisi za kidini ni kosa kubwa kwa kipindi hiki, watanzania hawako tayari kwa hilo japokuwa kisheria inakubalika."

  Katika utafiti huo CHADEMA iliongoza kati ya vyama pinzani kuingia IKULU kwa kuwa na 16% ikifuatiwa na CUF 14%. Cha kushangaza hata maeneo yale ambayo huhesabika kama ngome yaCHADEMA, ilifanya vibaya. Kwa mfano Arusha ni 35% na Moshi 40% tu ndio waliohitaji kuiona CHADEMA yaingia IKULU. Kwa Arusha wengi walikatishwa tamaa na viongozi wao hasa kwa tukio la hivi karibuni la kuwapeleka wanachama kuandamana bila mipango maalum.

  Mh Slaa nilipompigia simu alikataa kusema lolote na kukata simu. Mh Zitto Kabwe, alicheka na kusema "sina uhakika kama hizo namba zinawakilisha hali halisi. Hata hivyo kuwaeleza watu mpaka wakuelewe inachukua muda, chama hakina haraka. Tunachojua sisi ni kuwa tukilinganisha na tulikotoka tunajivuna kuwa chama kinapiga hatua"

  Nilipomhoji Julius Mtatiro alisema yafuatayo: "Watanzania wanapenda propaganda, chama chetu hatukujiandaa kwa hilo na wala hatuamini hilo. Namba si tatizo kwa chama chetu, tutaendelea kuwaambia ukweli watanzania na tuna program nzuri inayokwenda hatua kwa hatua. Tumetatua mgogoro wa Zanzibar kwa amani, sasa nguvu yote tunaielekeza Tanzania bara. Utajionea mwenyewe matokeo ya uchaguzi ujao."

  Hali ya vyama vya upinzani ni mbaya, kwani kama haitasikiliza matakwa ya watanzania kuna hatari kwa vyama hivyo kufa. Wakati ni huu, asiyesikia la mkuu huvunjika guu.
   
 2. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #2
  Nov 23, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Niliwahi kusema zamani kuwa 54% ya watanzania mwaka 2010 hawakupiga kura. From 46% ya wapiga kura only 62% ya wapiga kura walikuwa wameipigia kura CCM na Chadema kilipata asilimia 27% huku CUF ikiwa ya tatu kikipata 8.3%.

  Kama kuna chama kitaweza kutambua matatizo ya asilimia 54% ya watanzania ambao hawakupiga kura basi chama hicho kitaweza kuwaangusha CCM, Chadema, na CUF. Kwasababu hawa 54% wangelikuwa chama cha siasa basi sasa hivi tungelikuwa na serikali mbadala ya CCM.

  Tafakari!!!
   
 3. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #3
  Nov 23, 2011
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Nasikitika kusema kuwa mpaka leo hakuna CHAMA pinzani ambacho kipo tayari kuelewa matakwa ya hao watanzania wapiga kura. Na kibaya zaidi vyama hivi havikubali ukweli huo na ndio maana havitasonga mbele.

  Hili ni tatizo kubwa sana kwa vyama vya upinzani Tanzania.
   
 4. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #4
  Nov 23, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mnaandika vinyesi na kujijibu wenyewe!!
  Akili cha chiriku hizi.
   
 5. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #5
  Nov 23, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Ndio ukweli huo ndugu wewe beza lakini siku ukija kuzinduka utafahamu nini tunaongea. Kura za marohani za pemba ndizo ziliwaamsha CCM kuwa change is coming in Zanzibar. Tanzania Bara watanzania wengi hawapigi kura na wala kujisumbua kupiga kura kwani wanaona hakuna lamaana chama chochote kitawaletea katika maisha yao. Hivyo ikija kutokea chama kinawagusa tutayaona mabadiliko.
   
 6. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #6
  Nov 23, 2011
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Ingelikuwa mbio za hiyo AVATAR yako ni sawa na mbio za chama chako kuwaelewa watanzania katika jitihada za kuelekea IKULU, ninimani mwaka 2015 mngetua huko. Haa haaaaa haaaaaaa!
   
 7. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #7
  Nov 23, 2011
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Tatizo la vyama vya upinzani ni kutokubali ukweli. Laiti wangejifunza hili wangekuwa mbali. Majibu ya wanachama wa vyama pinzani utayoyaona hapa ni uhakikisho wa maelezo hayo. Ajenda kubwa iliyobakia hivi sasa kwa baadhi ya upinzani ni fujo. Kweli tutafika kwa hili?
   
 8. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #8
  Nov 23, 2011
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mimi nakuomba wewe uliyeweka hii post kwa vile umeliona hilo nenda kwa tendwa ukasajili hicho chama chako cha upinzani unachoona kitawagusa watz.NALOG OFF niko bize na kuelimisha watz juu ya ubovu wa mswaada wa marekebisho ya katiba uliopitishwa sio na bunge ,bali wabunge wa magamba na madem zao cuf
   
 9. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #9
  Nov 23, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  tayari watanzania walishachagua kukitoa ccm ikulu ktk uchaguzi uliopita...kama si kwa kuchakachuliwa kwa kura zao
   
 10. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #10
  Nov 23, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Tatizo si wananchi, tatizo ni mfumo wa uchaguzi hautoi mwanya kwa wananchi kufanya maamuzi. Hii ni hatari sana kama wananchi wanakosa imani na system nzima ya uchaguzi. Tungekuwa na chaguzi huru na haki watu wengi wangeshiriki. Lakini tatizo lingine linalofanywa na Tume ya uchaguzi ya CCM ni voters supression. Ku-scramble majina ya wale wanaoonekana kutowaunga mkono ni moja ya njia pekee iliyobaki ya kupunguza hamasa ya wapiga kura. Mtu hawezi kuwa anahamishwa vituo uchaguzi baada ya uchaguzi bila ridhaa yake. Tume inabandika majina siku moja kabla mtu anatoka kwake na kufika kituoa alichopigia kura uchaguzi uliopita bila mafanikio. Hii ni demotivation factor kubwa sana ya ushiriki wake uchaguzi ujao.

  2015 inaweza kuwa worse zaidi.
   
 11. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #11
  Nov 23, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  You are correct Mkuu, tatizo ni kwamba Watanzania hawajajua umuhimu wa kupiga kura au hawajaona chama makini chenye sela za kuwakomboa!!!!!!!!! Inabidi sasa kuwe na mkakati wa makusudi kuwaelimisha Watanzania wajue kuwa uamuzi wa mustakabali wa maisha yao ni kupiga kura kuchagua chama mkombozi!!!!!!!
   
 12. c

  cheichei2010 JF-Expert Member

  #12
  Nov 23, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hizi research za kitanzania huwezi ni convince nizikubali.
  1:Huwa wasomi wengi mfumo unaowapelekea kuwa wasomi waliishadesa sana.
  2:Questionnaires huwa zinachakachuliwa sana,watanzania hawapendi kufanya kazi ngumu.wanachoongalia ni fedha tu.
  3:Ma prof. wengi wanaajiliwa na serikali, hivyowengi hupenda kujipendekeza kwa serikali ili wapate ulaji na wale wanaokwenda kinyume hupigwa chini.angalia kina Lamwai,Baregu n.k
  4.tuliishaona report za kina Mkandala wanaoheshima na ujinga walioufanya kuelekea uchaguzi mkuu.

  Kwa hiyo naamini mleta hoja hapa,atakuwa sehemu mojawapo ya niliyoyaandika."KATUMWA" na hao wasomi wanaotumiwa kupotosha mambo kwa maslahi yao.
   
 13. ismathew

  ismathew JF-Expert Member

  #13
  Nov 23, 2011
  Joined: May 18, 2011
  Messages: 254
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tumekuelewa kama umeegemea Jembe na Panga, Napita tu.
   
 14. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #14
  Nov 23, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Vijana ahsante kwa utafiti wenu, mwenye macho ahambiwi tazama. Kutokana na hali mbaya ya uchumi hiyo ni changamoto kwa jamaii ya Watanzania. Wazee wa vyama na wana harakati chukua hatua!!!!!!!!!Ukombozi tunao mikononi mwetu ni kujipanga kupiga kura tuondoe serikali dhalimu !!!!!!!!

   
 15. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #15
  Nov 23, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Si ndio maana tunahitaji mabadiliko hata tume ya kusimamia kupiga kura ichaguliwe na wananchi on merits and integrity sio ichaguliwe na Raisi wa nchi, ipitie kwenye vetting ya bunge!!!!!!!!! Katiba mpya baba isiyompa Raisi nafasi ya kuchakachua upo??????????

   
 16. u

  uhurubado JF-Expert Member

  #16
  Nov 23, 2011
  Joined: Mar 25, 2007
  Messages: 396
  Likes Received: 199
  Trophy Points: 60
  Wanafikiri sisiem ndo inaleta njaa kwene mifuko yao, ngoja waitoe na njaa iendelee ndo patakuwa patam!
   
 17. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #17
  Nov 23, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Zawadi Ngoda,
  Nakusikitikia sana na utafiti wako usiokuwa na macho. Taznzania haijawahi kuwa na uchaguzi ulio huru na wa haki kwa sababu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni mteuliwa wa Rais, wasimamizi wa uchaguzi ni Wakurugenzi wa Halmashauri ambao ni wateuliwa wa Rais! Wewe unategemea nini kwenye mazingira haya?
  Hilo la udini na ukabila ni matunda yaliyotokana na mbegu mbaya inayoenezwa na CCM! Hakuna chama chochote cha upinzani kinachopanda mbegu mbaya ya udini na ukabila, ni CCM tu ndio kinara! Wewe kwa akili yako finyu kwa nini hujiulizi Msajili wa Vyama vya Siasa havifuti "vyama vya udini na ukabila" kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, 1992? Ni CCM tu ndio yenye "macho" ya kuona udini na ukabila uliopo kwenye vyama vya upinzani? Hizo propaganda haziendelezi nchi yetu hata hiyo CCM unayoifagilia haitafika mbali kwa mtaji huo!
   
 18. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #18
  Nov 23, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hili nadhani ni ujinga wa Watanzania na sio kukosa chama mbadala...
  Huwezi kuwa na akili timamu kama unadhani kuichagua ccm au kutopiga kura ni sahihi kwa vile hakuna mwingine.
  Ivi kweli Chadema walikuwa hawana policies nzuri na zilizo solid mwaka 2010? Ivi kweli kuibiwa mabilioni ya fedha sio sababu tosha ya kuondoa huyo mwizi?
   
 19. z

  zamlock JF-Expert Member

  #19
  Nov 23, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  :a s 465:
   
 20. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #20
  Nov 23, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mkuu,

  Vyote unavyodai ni sababu tosha kuwaondoa madarakani CCM but tumuweke nani? Hivi mfano unadhani Mbowe anaweza kuwa replacement ya Mizengo Pinda au JK. Mbowe huyu aliye na mgogoro na NSSF hadi leo kuhusu mkopo, aliyewapa tenda ya magari used Chadema. Worse enough na posho anadai bungeni akisema ni haki yake. Unafikiri akipewa funguo za hazina yetu patakuwa salama? Acheni bwana hakuna Chama mbadala hapa tunadanganyana tu? Dawa wacha ufisadi ukue kiwango cha kutisha kuchafuke ndio watu watakuwa na ubinaadamu wa kujua mabaya wanayoyafanya. Vyenginevyo hakuna chama nchini Tanzania kinachoweza kusema kina uadilifu usinidanganye
   
Loading...