Watanzania wamjia juu swahiba wa Kikwete

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,947
4,444
WATANZANIA kadhaa wamejitokeza na kumshutumu rafiki wa karibu wa Rais Jakaya Kikwete, ambaye ni mwekezaji katika sekta ya madini, James Sinclair, kwa kuanika hadharani kwa wawekezaji wenzake, ripoti ya Kamati ya Rais ya Madini ambayo bado ni siri.

Wananchi kadhaa wamekuwa wakipiga simu katika ofisi za gazeti hili na kueleza kushangazwa kwao na hatua ya Bw. Sinclair kuweka hadharani yale yaliyomo katika ripoti hiyo ikiwa ni siku chache tu baada ya Rais Kikwete kukabidhiwa ripoti hiyo.

27.jpg


JAMES Sinclair

Gazeti hili liliripoti katika moja ya safu zake, toleo lililopita, kwamba Bw. Sinclair ameandika waraka na kuuweka katika tovuti ya kampuni yake akiwaeleza wawekezaji wenzake katika sekta ya madini Tanzania kwamba amefanikiwa kuisoma ripoti hiyo ambayo bado ni ya siri, na kwamba ina mambo ambayo ni ya manufaa kwao.

Aidha, kufuatia taarifa iliyomo kwenye safu hiyo ya Raia Mwema ya Lula wa Nzela Mwananzela, mtandao wa JamiiForums.com ambao mwanzoni ulikuwa unajulikana kama Jambo Forums, ulianzisha kampeni kamambe ya kumtaka Bw. Sinclair kuacha kutoa siri za serikali kwa kuweka hadharani mambo ambayo hata Watanzania wenyewe hawajapata nafasi ya kuyajua.

Mpaka sasa haifahamiki ni vipi Bw. Sinclair aliweza kuiona ripoti hiyo ya Kamati ya Rais ya Madini ambayo bado ni siri, na pia kwa nini aliamua kueleza yaliyomo kwenye ripoti hiyo katika ovuti ya kampuni yake wakati akijua kuwa bado ripoti hiyo ni siri.

Kampeni hiyo ya JamiiForums ilianza wiki iliyopita baada ya makala hiyo ya Lula kufunua waraka wa Bw. Sinclair kwa wanahisa wa kampuni yake kuhusu mapendekezo ya Kamati hiyo ya Madini iliyoongozwa na Jaji Bomani.

Katika waraka huo wa Mei 30, wiki moja tu tangu Rais Kikwete kukabidhiwa ripoti hiyo, Bw. Sinclair anadai kwa ujasiri wote kuwa amepata kuyaona mapendekezo ya Kamati hiyo na maoni ya Chemba ya Biashara ya Tanzania na kuona kuwa yatawanufaisha watafutaji wa madini wanaolipwa kwa mrabaha kama yeye.

Katika waraka huo ulioandikwa kwa Kiingereza, Sinclair anasema hivi: “Wapendwa rafiki,…Mwaka jana Rais Kikwete wa Tanzania aliunda Kamati kupitia sheria ya Madini.

Kamati hiyo ambayo ilipewa jina linaloashiria majukumu na mipaka yake, ilijulikana kama “Kamati ya Rais ya Kupitia na Kuishauri Serikali Kuhusu Usimamizi wa Sekta ya Madini”

Nimepata nafasi ya kupitia mapendekezo ya Kamati hiyo – pamoja na maoni ya Baraza la Madini – na sina matatizo makubwa nayo. Hata hivyo, jambo la muhimu kujua ni kuwa uamuzi wa mwisho wa mapendekezo hayo uko kwa rais – na si Kamati.

Rais Kikwete ana ufahamu na uwezo mkubwa na hatafanya jambo lolote ambalo linaweza kuvuruga uwiano wa sera za kusisimua uchumi na matumizi ya Serikali ambazo zimesababisha ukuaji mkubwa wa msingi wa uchumi wa Tanzania, ukuaji ambao kwa kiasi kikubwa umetokana na wawekezaji wa kimataifa.

Kuna pendekezo moja lililotolewa ambalo limenivutia, linasema ‘sera (mpya ya madini) ielekeze kutoa manufaa kwa watafutaji wa madini (kama Sinclair) na si kwa wachimbaji.’

Sina shaka mawazoni mwangu kuwa mapendekezo ya Kamati hiyo yana lengo la kuboresha mazingira na faida kwa makampuni ya utafutaji (kama ya kwake) ambayo kwa ugunduzi wake wanaleta utajiri mpya kwa taifa na wananchi wake.”

Baada ya yaliyomo kwenye barua hiyo kuanikwa na Raia Mwema ndipo wanachama wa JamiiForums, mtandao ambao ni maarufu duniani kwa wazungumzaji wa Kiswahili, walipoandika barua ambayo wamekuwa wakiisambaza kwa vyombo mbalimbali vya habari duniani, wadau wa mambo ya kiuchumi na kwa Sinclair mwenyewe, kumtaka aombe radhi kwa kutoa nje siri za Serikali.

Barua hiyo ya Watanzania hao inaonyesha ni jinsi gani wanajihisi kudharauliwa na kutendwa vibaya na wawekezaji wageni ikizingatiwa kuwa suala la madini ni jambo nyeti nchini.

Aidha Watanzania sehemu mbalimbali nao walijitokeza kueleza hisia zao kuhusu suala hilo. “Inawezekana alichofanya Bw. Sinclair ni kuingilia ununuzi wa hisa kwa kampuni yake kwa kuwapa habari za ndani (inside trading) wawekezaji wake; hasa kwa kuwahakikishia kuwa hakuna mabadiliko makubwa yatakayo vuruga kazi za kampuni yake”, alisema mtaalamu mmoja wa masuala ya fedha anayeishi Dallas, Marekani.

Hakuna taarifa yoyote, ama ya Sinclair mwenyewe au ya Serikali iliyokwisha kutolewa kuhusu hatua hiyo ya mwekezaji huyo. Baadhi ya Watanzania waliochangia wamesema wanatarajia Bunge lifanye kama lilivyofanya wakati wa tukio la sinema ya “Mapanki “ya Hubert Sauper.

“ Natumaini wabunge wenzangu wataonyesha mshikamano na kumkemea Sinclair kwa kitendo chake hicho cha kudhalilisha nchi yetu kama tulivyofanya kwenye suala la mapanki, ” alisema mbunge mmoja aliyekuwa anajiandaa kwenda Dodoma kwenye kikao cha bajeti.

Rais Kikwete na Sinclair ni marafiki wa muda mrefu, yapata takribani miaka 20. Sinclair alikuwa akimiliki kampuni ya madini ya Sutton Resources aliyoiuza baadaye.

Moja ya ripoti zilizopatikana inasema Sutton Resources ilikuwa na kampuni tanzu, Kahama Mining Corporation Ltd., ambayo Agosti 5, 1994 iliingia mkataba na Serikali ulioonyesha wazi kwamba ulikuwa unahusu eneo la Butobela, Wilaya ya Geita, Mwanza.

Agosti mwaka 1996 Kahama Mining Corporation iliingia eneo la Bulyanhulu, Wilaya ya Kahama, Shinyanga na kuwaondosha wachimbaji wadogo wadogo takriban laki nne waliokuwa wakiishi na kuchimba dhahabu katika eneo hilo.

Baadaye, Sutton Resources iliiuza Kahama Mining Corporation na Bulyanhulu kwa Kampuni ya Dhahabu ya Barrick Gold Corporation ya Toronto, Canada kwa dola za Marekani milioni 280. Leo Bulyanhulu ni moja ya migodi tajiri kwa dhahabu katika Bara la Afrika.

Kampuni hiyo ya Barrick Gold ndiyo ambayo ilihusika kwa kuchangia mtaji katika uanzishwaji wa kampuni mpya ya Tanzania Royalties Exploration ambayo inaongozwa na Sinclair na wana makubaliano maalumu ya utendaji wa kazi zao. Na uhusiano huu pia unadaiwa kuonekana kwenye mkutano ulioisha juzi huko Arusha wa Sullivan ambao Mkuu wake Balozi Andrew Young ni mwanabodi katika kampuni hiyo ya Barrick.

Barua hiyo ya Watanzania kuhusu Sinclair inaweza kupatikana kwenye mtandao huo wa JamiiForums.com au kwenye mtandao wa habari wa Klhnews.com ambapo watanzania wameombwa kuichukua na kuituma katika barua pepe kadhaa ili kuonyesha kuchukizwa na kukerwa kwao na kitendo hicho cha Sinclair.


source;http://www.raiamwema.co.tz/08/06/11/3.php
 
Kilio chetu kimesikika wana JF ni kazi sasa ya mungwana kujiosha sasa pindi asomapo.
 
Jf After Being Denounced As Threat To The So Called National Security Are Now Being Declared Heroes Even Though They Are In One Way Or The Other. Thanx Jf
 
A good start, let's not rest on our laurels just yet...safari bado ni ndefu, vita mbele, JF oyeee!!
 
Jk naona karogwa siamini kama ana akili timamu.Bravo JF
 
Walivyoiweka nafarijika sasa jamiiforums itajulikana na kusomwa na wananchi wengi zaidi.
Kutokana na ufwatiliaji nilofanya hivi karibuni nilishangazwa na watu walioko kwenye ofisi muhimu za umma ambao bado usiku wa giza.. wanaisikia tu JF mtaani, na wamezidi kuwa mbali zaidi baada ya jina jipya.
 
kama kawaida ya magazeti ya Tanzania. JF haipewi credit kwenye hili

jamaa ni ma haters ajabu
 
Nami naunga mkono kilio cha wengi inakuwa kama laana kwa wanaojifanya hawasikii....
 
kama kawaida ya magazeti ya Tanzania. JF haipewi credit kwenye hili

jamaa ni ma haters ajabu

Tenda wema wende zako husingoje shukrani. JF ni moto wa kupulizia mbali, tutachangia hoja na kuweka uchafu wa either Serikali, Bunge etc.............. Atakayetoa credit atoe, asiyetoa na anyamaze lakini mwendo mdundo tu na ujumbe utakuwa umefika.
 
Swahiba wa JK ajibu barua nzito aliyotumiwa na wana shupavu wa JF.....Rev Kishoka kapost...bofya maandishi mekundu

https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=14270&page=4
 
kama kawaida ya magazeti ya Tanzania. JF haipewi credit kwenye hili jamaa ni ma haters ajabu

"Sema wewe si Kiazi. Nikisema mimi Muhogo nitaambiwa nina Mzizi."

Huyu Sinclair nimekuona wewe GT, kina Mwkjj na wengine mnamchambua toka August mwaka jana kwenye thread inayoitwa "The Jimes Sinclair Connection," halafu leo media ya Bongo inasema condemnation za JF zilifuatia makala yao ya Jumatatu.

Skandali hii mpya ya Sinclair ya kupenyezewa ripoti iliibuliwa na Lunyungu wiki iliyopita kwenye thread yake "Sinclair huyu hapa tena jamani." Ishu ya petition ilianza katika thread hiyo ya Lunyungu kabla ya Mwnkjj kuipa prominence ilipopata thread yake nyenyewe mwishoni wa wiki iliyopita, kabla ya Rai kuja na stori yao Jumatatu, wakati ishu tayari ilishamfikia Jim Sinclair over the weekend. Media ya Bongo bwana kwa ku hate JF! Anyway, letu moja, na hamna anaetaka kupewa kashata au pointi zozote hapa, ila Rai hawakuwa wakweli!
 
Mwanakijiji,

Asante kwa kazi yako kubwa juu ya hili. Inahitaji uzalendo mkubwa sana kuendelea kupigania maslahi ya nchi yetu. Hapa naona unatusaidia kuwafunga paka kengere.
 
Mwanakijiji,

Asante kwa kazi yako kubwa juu ya hili. Inahitaji uzalendo mkubwa sana kuendelea kupigania maslahi ya nchi yetu. Hapa naona unatusaidia kuwafunga paka kengere.

Ndugu yangu, tunavyofanya hivi kila mmoja kwa namna yake kuna watu wanadhani tunafanya hivyo kwa sababu ya chuki dhidi yao au wivu. Nadhani wangefurahi tusingemnyoshea kidole Sinclair...
 
Back
Top Bottom