Watanzania wamjia juu Mkenya, aomba radhi.

Ashura9

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
740
485
Watanzania wamjia juu Mkenya, aomba radhi.

Watanzania wamemjia juu Mkenya Rosemary Odinga ambaye pia ni mtoto wa mwanasiasa mkubwa wa nchini kenya Raila Odinga, ambaye ametoa taarifa za bonde la Olduvai Gorge kuwepo nchini Kenya, na kumtaka kuomba msamaha na kusahihisha kauli yake.

stdejilovulyfwrm.jpg

Wakiendesha kampeni hiyo kwenye mitandao ya kijamii kwa kutoa maoni kwenye picha yake, kumeibua hisia kubwa baina ya jamii ya Wakenya na Watanzania, huku Watanzania wakidai Wakenya wanawachokoza.

onesmo_killenga: Na hili tutalifanya fundisho kwenu omba msamaha mapema @rosemaryodinga la sivyo tutachukua hatua kama wananchi wa nchi yetu na hamta amini tutasusia bidhaa zenu zilizopo nchini ili tuendelee kuheshimiana hubacaren: Rosemaryodinga you still remain silent? ignoring this or what??? umewakosea watanzania wote na you should apologize publicly or you will just tarnish your image.

esteriche: Dd kasema oldvai ipo kenya xa ona watanzania wanavyomfrahisha ...atafrahiii kwa kweli hizo comments watanzania katika ubora wao na masters za kutetea vya kwao yani hapa nacheka na comment tu.

call_me_kimodo: Mama hivi unajua wa tz wewe, haya matusi tutayoanza kukuporomoshea utaomba poa, omba radhi mwenyewe mwizi wa rasilimali zetu.

Baada ya mkiki huo wa kwenye mitandao kutoka kwa watanzania, wakenya hawajakaa kimya na kuamua kujibu mapigo.

kimathijr: Mnajua nyie wabongo huwa mnabonga sana.. hata kichwa zenu tunajua zimejaa maji. sijapata ona majitu majina in the continent kama nyinyi mazee.... ur such as disgrace to our east community. smh.

Baada ya malumbano hayo Rosemary aliamua kujirudi na kuomba radhi., huku akisema hakuwa nania mbaya kusema kuwa Olduvai Gorge ipo Kenya, kwani Afrika mashariki ni moja.

Nini mtazamo wako kwa radhi hiyo aliyoomba?

600950162eL_0.jpg


Chanzo EATV
 
Aende mbele zaidi akakanushie pale pale alipolizungumzia hili na pia awaeleze waziwazi kwamba hata Mlima Kilimanjaro hauko kwao ni mali ya Watz, sema tu yenyewe Matz yamelala usingizi kama yamerogwa vile.
 
Back
Top Bottom