BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,831
- 287,782
Watanzania wamepoteza kabisa imani na serikali iliyo madarakani kufuatia kashfa nyingi zinazowakabili watendaji wakuu wa awamu ya tatu na ya nne. Kashfa hizi zinahusiana na kusaini mikataba feki ya uchimbaji wa madini isiyo na maslahi kwa Tanzania, ufisadi wa mabilioni ya shilingi uliofanywa na viongozi mbali mbali, kujipatia kampuni na migodi ya madini yaliyo chini ya serikali (KCM) kwa njia za haramu, kuzembea na hatimaye kutoroka kwa mhusika mkuu wa kashfa ya Rada.
Kinachotushangaza Watanzania pamoja na kashfa zote hizi hakuna aliyepoteza ajira yake(Ballali alijiuzulu kabla ya kutenguliwa kwa uteuzi wake) hakuna aliyetiwa ndani ili kuvisaidia vyombo vya dola katika uchunguzi, hakuna ambaye mali zake zimeshikiliwa na serikali ili kujua kama zimepatikana kihalali.
Kwa mantiki hiyo basi tuna wasi wasi mkubwa kwamba serikali iliyo madarakani haina uwezo wa kupambana na kashfa nzito zilizowashtua Watanzania labda kwa kuwaogopa wahusika au kwa watendaji waliomo serikalini kuhusika kwa namna moja au nyingine na kashfa hizo.
Hivyo tunaomba serikali ijiuzulu ili kutoa nafasi ya uchaguzi mpya utakaoinusuru nchi yetu kwa janga kubwa linaloinyemelea Tanzania.