Watanzania wamelogwa Mungu pekee ndio atakaye wafungua muda ukifika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania wamelogwa Mungu pekee ndio atakaye wafungua muda ukifika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mchaga 25, Nov 21, 2011.

 1. Mchaga 25

  Mchaga 25 JF-Expert Member

  #1
  Nov 21, 2011
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 463
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naandika andiko hili baada ya kukaa kimya kwa muda ni kitafakari muelekeo wa Umaskini huu unaonikabili mimi na ndugu zangu ambao tuko asilimia 80% ya wanachi wote hapa nchini.

  Nimejaribu kuwa na switch side za kiitikadi ili kuanagalia utayari na uzalendo wa haki lakini nachelea kusema safari ya Mapinduzi katika nchi yangu ingeweza kumfanya CHE- aende mbagala au gongo la mboto na kutazama watu wanavyo ishi na kurudi kupanda ndege na kuondoka zake.

  Hakika usaliti umekuwa sehemu ya historia ya afrika nahelea kusema imekuwa kama popular culture ya africa., Namshukuru Mungu kwa uwezo wa kunipa maono mapya ya kuweza kutazama usaliti huu na kuutolea maneno haya katika nyanja zifuatazo:

  SIASA:

  Siasa imekuwa ikutumika kama market strategy ya uuzaji wa nchi yetu, wansiasa ambao wamekua wakiongea mpaka makoo yanawakauka wao ndio wamekua madalali wa nchi yetu na rasilimali zetu. Jamii inashindwa kutofautisha tofauti kati ya ufisadi na wanasiasa wa nchi hili ni la dhati kabisa kwani itakuwa raisi kwa mwananchi kumuita Lowasa, Chenge Fisadi kuliko kumwita Chavda fisadi.
  Siasa imekuwa kama kigezo muhimu cha kutunyima haki wanyonge pale tunaposema pembejeo zinachelewa kufika tunaambiwa tunatumika kisiasa pale tunaposema, power tiller hazina tija tunaambiwa tuna hujuma kilimo kwanza fikra sahihi za mwenyekiti, Pale tunaposema bajaji kama ambulance hazina tija tunaambiwa nyie wapinzani, pale tunaposema shule za kata hazina tija kwa taifa tunambiwa nyie wavivu wa kufikiri, pale tunaposema kituo cha afya kila kijiji ni ubadhirifu wa hela bora tuboreshe vilivyopo tunaambia wanafiki wa kisiasa, safari ya mabadiliko ni ndefu safari ya madiliko yanahitaji utayari, siasa sio kuwa na mtazamo wa rangi, siasa sio udalali, siasa sio unafiki, siasa sio atm, siasa sio bunduki ya kuporea ninawaza tu.

  VYUONI:

  Nasikitika kulisema hili, nasikitika sana, ndugu zangu wana vyuo nyie mmekuwa mnafanya usaliti tena usaliti wa dhambi hata sikumoja hutasikia kuwa manzese watu wanagoma kushinikiza serikali kuwalipa wanafunzi kwa sababu na nyie mmegoma lini machinga wapewe sehemu sahihi za kufanyia biashara?? usaliti usaliti usaliti unaendelea katika nchi yetu, mmewezwa kwa ubinafsi wenu mmeweza kwa unafiki na uchoyo wenu.

  wanafunzi wetu wamekuwa wanapikwa wawe wezi na kwa kuiga mfumo husika, walimu wenu ni ma consultancy wazazi wenu ni makuadi wa soko huria babu zenu ni mafisadi hakika uozo ukishamiri mwisho unakaribia.  ASASI ZISIZO ZA KISERIKALI

  Nyie ni wanafiki na waganga njaa wakubwa tena mnaniuzi sana, kwani hakuna hata mmoja wenu anayeamini anacokisema, tumeyaona mengi kuanzia ya ePA, Dowans na mengineyo mengi tu eti tunaandamana halafu mnaishia kukimbia utayari wenu uwapi unafiki na wizi wa fedha za wafadhili. Leo mnapinga ushoga wakati ASASI ZENU zinaendeshwa na hela za ushoga unafiki unafiki  POLISI

  Mmeoza kwa rushwa, tena rushwa za mauti, haki imekuwa laana kwenu, mnatia huruma sana, mnakatisha tamaa, nachelea kusema la kuvunda halina ubani. Mmekuwa mkitumika kunyima haki za watu, mkitumika kisiasa usaliti usaliti

  Na mengine mengi, MEDIA, CELL NETWORK, TISS, JESH , usaliti mtupu

  Ni rehema za Mungu zitakazo mkomboa mwananchi. Sauti ya watu ni sauti ya Mungu


  Mungu ibariki Tanzania, Mungu sikia sauti za waja wako.
   
 2. BONGE BONGE

  BONGE BONGE JF-Expert Member

  #2
  Nov 22, 2011
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 3,397
  Likes Received: 1,522
  Trophy Points: 280
  .......hatufikirii kabisa, vichwa tunatumia kuvalia kofia (kwa wale wa magamba)
   
 3. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #3
  Nov 22, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Wana Igunga watakuwa wamekusikia
   
 4. Mchaga 25

  Mchaga 25 JF-Expert Member

  #4
  Nov 22, 2011
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 463
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Inauma sana kuona jinsi ndugu zangu wanavyo ishi kwa Matumaini hawajui kesho hawajui mlo wa mchana huu
   
 5. k

  katoto Member

  #5
  Nov 22, 2011
  Joined: Dec 5, 2007
  Messages: 42
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Umesema ukweli kabisa, wanajeshi, madaktari, walimu, manesi, wachungaji, waganga wa jadi, in fact karibu wananchi wote mtanzania wamekuwa wasaliti wa nchi, maadili yanakiukwa kwa asilimia 99, kila mtu anataka ale peke yake.
  Hivi tuna nini?
  Hivi nani atatutoa kwenye wimbi hili na kizazi kijacho kitakuwaje!
   
 6. k

  katoto Member

  #6
  Nov 22, 2011
  Joined: Dec 5, 2007
  Messages: 42
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Hivi hii statistics kuwa 80% ya watz wanategemea kilimo, mbona haibadiliki? Toka nimeanza shule miaka ya late 70s nimesikia ikisemwa?
   
 7. Mchaga 25

  Mchaga 25 JF-Expert Member

  #7
  Nov 22, 2011
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 463
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mkuu ndio uti wa mgongo wa taifa tena kwa kutumia jembe la mkono
   
 8. P

  PAMBANA Member

  #8
  Nov 22, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kiongozi nakubaliana na wewe ulichokisema ni ukweli hasa wanavyuo tumekuwa wabinafsi na kuwasahau wananchi wengine kama ambao wanapata shida kila iitwapo leo mpaka wameshaifanya kuwa sehemu ya maisha yao.Tubadilike jamani na tumwombe maana sisi ndio wa kuijenga Tanzania ya sasa na ya baadae,
   
Loading...