Watanzania wamegoma kufanywa wajinga na Magufuli!

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,526
30,239
Kama ambavyo yeye mwenyewe Rais Magufuli aliwaambia watanzania katika issue ya Mo kuwa watanzania hawawezi kufanywa wajinga na Jeshi la Polisi

Hivi inawezekanaje kuwa aliyemteka Mo, amrudishe na gari ile ile iliyoyotajwa na Polisi hadi Gymkhana na kumbwaga pale, tena akiwa ameacha na silaha, bila Polisi hao kutwambia ni mtu gani huyo mwenye ujasiri wa kutenda kitendo hiko??

Hivi zile siku 3 alizotuahidi IGP kuwa ataweka hadharani kila kitu kinachohusu utekwaji wa Mo, si zilishapita kitambo??

Vivyo hivyo watanzania wamegoma kufanywa wajinga na Profesa Lipumba, ambaye kila mtanzania anajua namna anavyobebwa na vyombo vya dola, ikiwemo ofisi ya msajili wa vyama.

Kuwa licha ya yeye mwenyewe kuamua kwa hiyari yake kujiuzulu kwa maandishi uenyekiti, lakini mahakama kuu imemtangaza kuwa ndiye Mwenyekiti halali wa CUF!

Lengo la CCM lilikuwa kuua upinzani, hususani chama cha CUF kule Zanzibar

Matokeo yake badala ya kuuua upinzani, ndiyo kwanza amefufua upya nguvu ya upinzani!

Baada ya kuona hivyo Maalim Self ameona enough is enough, ametangaza kukihama chama hicho na kuhamia ACT wazalendo

Sasa walichoshikwa na mshangao wale waliokuwa wakimfadhili huyo Profesa Lipumba na huo "uharamia" aliokuwa akiufanya, ni kuona kishindo cha Maalim Seif ameondoka na kila kitu huko CUF, yakiwemo majengo zilizokuwa ofisi za CUF kwa kupakwa rangi na kuwa ni ofisi za ACT wazalendo alikohamia na kupandisha bendera za chama cha ACT Wazalendo na kuzishusha zile za awali za CUF!

Ndipo sasa huyo Profesa Lipumba analalama kuwa eti wanaofanya hivyo wanafanya kosa la jinai!

Hivi inawezekanaje awaite hivyo wanaofanya hivyo wakati ni wenyewe walijitolea majengo yao bure kwa CUF, kutokana na mapenzi yao kwa Maalim Seif??

Sasa unawezaje kumkataza mwenye Jengo lake alilotoa bure kwa CUF eti asipake rangi za ACT wazalendo na kupandisha bendera za chama hicho??

Imenenwa kuwa huo ndiyo mshahara wa usaliti

Na MWISHO WA UBAYA AIBU!

Awe mpole tu Profesa Lipumba, kwa kuwa kama vyombo vya dola vilivyotaka, Maalim Seif keshawaachia chama chenu, sasa kelele zote hizi ni za nini??
 
Hii movie tulishaiona namna wanavyoiandaa, tokea mwishoni mwa mwaka 2015, pale Profesa Lipumba alipopata mwaliko wa kutembelea Magogoni, na kufanya kikao cha siri na Jiwe

Baada tu ya kikao kile, tukashangaa huyo Profesa Lipumba akibadili gia angani na kudai kuwa amerejea tena kwenye nafasi yake ya uenyekit wa CUF, tena akipata "baraka" zote kutoka kwenye vyombo vya dola!
 
tofautisha mali za cuf,na nyumba za kujitolea
lipumba amezungumzia mali za cuf
 
Hiki kinachofanywa na viongozi na mashabiki wa iliyokuwa CUF ndicho hasa tunachoweza kukiita People's Power
 
Kama ambavyo yeye mwenyewe Rais Magufuli aliwaambia watanzania katika issue ya Mo kuwa watanzania hawawezi kufanywa wajinga na Jeshi la Polisi

Hivi inawezekanaje kuwa aliyemteka Mo, amrudishe na gari ile ile iliyoyotajwa na Polisi hadi Gymkhana na kumbwaga pale, tena akiwa ameacha na silaha, bila Polisi hao kutwambia ni mtu gani huyo mwenye ujasiri wa kutenda kitendo hiko??

Hivi zile siku 3 alizotiahidi IGP kuwa ataweka hadharani kila kitu kinachohusu utekwaji wa Mo, si zikishapita kitambo??

Vivyo hivyo watanzania wamegoma kufanywa wajinga na Profesa Lipumba, ambaye kila mtanzania anajua namna anavyobebwa na vyombo vya dola, ikiwemo ofisi ya msajili wa vyama.

Kuwa licha ya yeye mwenyewe kuamua kwa hiyari yake kujiizulu kwa maandishi uenyekiti, lakini mahakama kuu imemtangaza kuwa ndiye Mwenyekiti halali wa CUF!

Baada ya kuona hivyo Maalim Self ameona enough is enough, ametangaza kukihama chama hicho na kuhamia ACT wazalendo

Sasa walichoshikwa na mshangao wale waliokuwa wakimfadhili huyo Profesa Lipumba na huo "uharamia" aliokuwa akiufanya, ni kuona kishindo cha Maalim Seif ameondoka na kila kitu huko CUF, yakiwemo majengo zilizokuwa ofisi za CUF kwa kupakwa rangi na kuwa ni ofisi za ACT wazalendo alikohamia na kupandisha bendera za chama cha ACT Wazalendo na kuzishusha zile za awali za CUF!

Ndipo sasa huyo Profesa Lipumba analalama kuwa eti wanaofanya hivyo wanafanya kosa la jinai!

Hivi inawezekanaje awaite hivyo wanaofanya hivyo wakati ni wenyewe walijitolea majengo yao bure kwa CUF, kutokana na mapenzi yao kwa Maalim Seif??

Sasa unawezaje kumkataza mwenye Jengo lake alilotoa bure kwa CUF eti asipake rangi za ACT wazalendo na kupandisha bendera za chama hicho??

Imenenwa kuwa huo ndiyo mshahara wa usaliti

Na MWISHO WA UBAYA AIBU!

Awe mpole tu Profesa Lipumba, kwa kuwa kama vyombo vya dola vilivyotaka, Maalim Seif keshawaachia chama chenu, sasa kelele zote hizi ni za nini??
Unachekesha sana title yako na yaliyo ndani ni vitu viwili tofauti. Hivi karibu utapata uchizi kwa chuki zako kwa JPM. Tafuta pesa hayo ya magufuli yatakutoa roho bure
 
Muacheni Lipumba mbona seif keshasema pooh,au ni hasira kwa seif kachungulia kaona ufipa nyote ni makambare!
 
tofautisha mali za cuf,na nyumba za kujitolea
lipumba amezungumzia mali za cuf
Utakuwa unaongelea lile kontena la visu na majambia yalitoka Uarabani yakakamatwa na Mahita mwaka 1995? Ok au unazungumzia misikiti waliokuwa wanafanyia Karate wakati wa Ngunguli?
 
Unachekesha sana title yako na yaliyo ndani ni vitu viwili tofauti. Hivi karibu utapata uchizi kwa chuki zako kwa JPM. Tafuta pesa hayo ya magufuli yatakutoa roho bure
Hiyo title ndiyo imekaa mahali pake......

Hivi hujaona namna Jiwe alivyoshupalia issue ya Mo, hadi akasema watanzania siyo wajinga to that extent??

Hivi kama hilo suala halijawa "master planned" kule Magogoni, iweje IGP atudanganye watanzania kuwa within 3 days mambo yote yatakuwa hadharani??

Hivi inawezekanaje ameshindwa kuweka hadharani issue yote ya Mo within 3 days, halafu Rais asimtumbue??

Hivi katika suala hili la Profesa Lipumba, ni mtanzania gani asiyeelewa kuwa Jiwe ana mkono wake??
 
Hii movie tulishaiona namna wanavyoiandaa, tokea mwishoni mwa mwaka 2015, pale Profesa Lipumba alipopata mwaliko wa kutembelea Magogoni, na kufanya kikao cha siri na Jiwe

Baada tu ya kikao kile, tukashangaa huyo Profesa Lipumba akibadili gia angani na kudai kuwa amerejea tena kwenye nafasi yake ya uenyekit wa CUF, tena akipata "baraka" zote kutoka kwenye vyombo vya dola!
Na kesi yake ikafutwa paaap kama ya mdogo wake rostam siku hizi ukishaingi mule ukitoka kama una kesi ur freeman to go!maendeleo hayna vyama
 
Back
Top Bottom