Watanzania Wameanza kumuelewa Dr Slaa na Siasa za Kukurupuka

Ama kweli kama Dr. Slaa anakurupuka ndio maana akapata kura zaidi ya milioni 2 hata mimi naomba karama ya kukurupuka. Kama Slaa alitoa list of shame kwa kukurupuka ndion maana CCM wamejuvua gamba nami eeh mola nijalie kukurupuka. Ndio kama Slaa amemshussha JK toka asilimia zaidi ya 80% hadi 60% niombe nini kama sio kukurupuka?

acha ukichaa,kwani slaa alikuwa mgombea pekee katika uchaguzi ule? bogus kabisa wewe
 
Unajua kama mtu uko unapigana nae ngumi kisha ukamdunda vya ukweli, akiona watu atakuwa anajisemesha jamani nishikeni nisije kumuumiza, nishikeni nishikeni nishikeni, kumbe hakuna kitu na ataishia kusema ngoja siku nikikushika utanikoma, kwahiyo ndio maana Slaa amebaki anatapatapa huku na kule. yaani katika vyama vitaisha vibaya ni cdm. unazungumzia siku 21 alizotoa Arusha wachague meya upya? mwambieni atoe siku zingine wawe wamesha tengua bajeti iliyopitishwa na madiwani na meya anayetambulika.
 
Wakati mwingine najiuliza, hivi tusingekuwa na wanasiasa wa kaliba ya Dr. Slaa, mambo yangekuwaje? Ni bora kuwa na madokta 'waropokaji' kama Slaa au watu wapole kama R.A? Kuna watu wasingetamani kabisa Dr. Slaa awepo. Wanataka pasiwe na 'waropokaji' ili watafune nchi hii kwa amani na utulivu kabisa. Yaani kama hata visingekuwepo vyama vya siasa, mambo yao yangenyooka kweli! Poleni sana!
 
Kuna watu huwa wanaongea tu ili nao waonekane wamesema kitu, wapo na wapo humu JF na ni haki yao kuonge
a, lakini mwenye akili atachuja na kuamua, miongoni mwa hao ni wewe! uliyeanzisha mada hii.

Napenda kukupongeza Dr Slaa kwa mara nyingine tena kwa kujitokeza na kujaribu kuwaelimisha waJF juu ya mambo mbalimbali, na pia kujibu vioja vinavyokulenga moja kwa moja kutoka kwa vibaraka wa mafisadi ambao wanatamani usiwepo mtu kama wewe TZ, naomba usife moyo na uendelee kuwapa bakora mpaka washike adabu, haya wanayoongea ndiyo matokeo ya juhudi zako za bila kuchoka, sasa wanaweweseka, wanawasiwasi na hawalali, na bado tusubiri waanze kusemana wao kwa wao na kupigana vikumbo wao kwa wao, maana wameshakubali kwamba miongoni mwao wapo mafisadi nyangumi na papa na wamepeana muda wa kujiondoa magamba kwa hiari, sasa tukae tusubiri hizo siku ziishe ndio tutajua nani ni nani katika nchi hii.

Hawa watu wanaoandika mambo ya namna hii ni miongoni mwa mafisadi na wanafaidika na pesa za kuiba serikalini, ufisadi upo kila kona ya nchi na hawa ni miongoni mwao, wao wanapenda maisha yaendelee kuwa hivi hivi ili waendelee kuibia serikali na kufaidi katika maisha yao.

Yanayotokea sasa katika nchi hii wote tunayashihudia na hawakupenda ila ni kwa mashambulizi ya majemedari hodari wa Chadema wakiongozwa na Dr Slaa ndio wamelazimika kufanya hayo, lakini pia tunasema hatudanganyiki na hatutarudi nyuma CCM inatakiwa kupumzishwa ikae pembeni kama vyama vingine vya Kenya, Zambia na kwingineko.

Dr Slaa Hakurupuki na angekuwa nakurupuka mpaka sasa angekuwa pabaya sana, maana masikio na macho yote yapo kwake, na pia wamemtafuta sana hawampati hata kwa skendo za kusingizia, na bado tunategemea kusikia mengi sana ya kujaribu kumchafua lakini hatachafuka kamwe, naomba ni wakumbushe kwamba " UKIINULIWA NA MUNGU JUU HUTAKAA USHUKE CHINI, UKIINULIWA NA WANADAMU UTASHUKA CHINI, Dr W. Slaa ameinuliwa na Mungu Kuja kuwaelimisha na kuwafumbua watanganyika walio wengi na sasa mafisadi na jamii yao haitaki maana watanganyika walio wengi wakishaelimishwa wakaelimika ndio mwisho wa Ufisadi katika nchi.
 
Dr Wilbrod Slaa(Phd) amekuwa mwana siasa maarufu hapa nchini hasa kwa namna yake ya kuibua mambo mbalimbali mchanganyiko mengine yakiwa na ukweli na mengine ya kiwa hayana ukweli!

Suala la kutaja watuhumiwa wa ufisadi ni moja ya mambo aliyofanikiwa kwani hadi sasa hakuna hata miongoni mwa aliowataja hawaja enda kumshitaki mahakamani au wao kukanusha! Mengine ni pamoja na suala la Kontena la karatasi za kupigia kura alilosema limetokea Afica ya kusini hadi leo hakuna ukweli wa jambo hilo!

Lakini pia amekua kua akitoa matamko yenye muda ambayo pindi muda unapo pita kuna kua hakuna hatua zozote zilizo chukuliwa! Mfano: Alimpa siku 9 Kikwete maisha ya watanzania yawe mazuri,Alitoa siku 21 serikali ihakikishe uchaguzi wa Meya unafanyika!

Juzi amempa Kikwete siku 90 awe amesha wafukuza Mafisadi ndani ya CCM! Dr Slaa lazima awe makini na ahadi za namna hii kwani zinatoa picha yake halisi ya kukurupuka katika siasa na inampunguzia heshima kwa Jamii. Ni bora awe anatoa siku hizo na utekelezaji Uonekane!

Sisi wana CHADEMA tumekwisha kukuelewa vyema wewe huna lolote. Nashangaa unashabikia nini wakati CCM ni kweli ni wezi!!!

Unabisha nini wakati Ridhwani Kikwete wakati anamaliza shule alikuwa hana kitu....leo anamiliki TZS karibu 7.8 Billion, je bado unatetea chama cha majambazi??? Mshenzi wewe!!
 
Watu wanatakiwa wajue kitu kimoja. Wakati wa mapambano kama haya ya kisiasa lazima kuwe na mbinu mbali mbali za kumkabili adui. Sio lazima, absolutely, sio lazima kila kombora wanalorusha limpige adui moja kwa moja. Chamsingi linaelekezwa upande anakodhaniwa adui yupo na bila shaka adui atatishika hata kuweza kujichanganya hivo kuweza kumkabili vizuri. Kwa manthiki hiyo basi, kisiasa, sio lazima kila kombora la cdm au slaa liwe la ukweli asilimia mia bali chamsingi lielekee na kuendana na hali hali halisi ya mambo yalivyo. CCM wao wanapaniki wnahangahika huku na huko kutafuta majibu in the process mengine ya msingi zaidi yanaibuka! Hebu angalia sasa hivi wameanza kuchukulia serious mambo yalyopigiwa kelele siku nyingi ya ufisadi wa rostam, amayo yalikuwa yanaonekna ni kukurupuka. Kwenye siasa hakuna kukurupuka ndugu yangu. Lazima uwe na mbinu za kumvuruga mwenzako, na Slaa amefanikiwa sana kwa hili na CCM sasa inamwogopa kama ukoma!!. 0714061253
 
DR, Slaa...acha hao watumwa wa fikra na tumbo wakuvalishe taji ya miiba.....iko siku..si mbali...watanzania wenye fikra huru, tutakuvalisha taji ya utukufu....!
 
Mlengo wa Kati,

Sina hakika na unachokiita ukurupukaji:

i) Swala la Kontaina la karatasi za uchaguzi ni vema ulifanyie uchunguzi kabla ya kusema nimekurupuka. Nilitoa Namba ya Gari na Namba ya Container iliyoleta Karatasi toka Afrika Kusini hadi Tunduma upande wa Zambia. Ikafaulishwa kwenye Lori la azam kwa upande wa TZ. Taarifa ilitoka kwa maofisa wa Serikali, na kuthibitisha ukweli wa Taarifa hizo japo mimi sikuwa nimewataja mara moja asubuhi ile waliitwa Dar, na hatimaye kuhamishwa kituo cha kazi kwa taarifa niliyonayo. Kiravu na RPC Advocate Nyombi wakaishia kusema Dr Slaa ni mwongo badala ya kufanya uchunguzi huru. Polisi walihusika na tuhuma hizo, immigration na TRA wote walihusika kwanini wao waioshie kutukana badala ya ucunguzi huru?

Pili Bungeni Waziri Mara alitangaza kuwa Serikali imenunua, machine na kuwa tayari ziliingia nchini, iweje ghafla serikali hiyo hiyo kupitria Tume kuwa sasa Karatasi zimechapishwa na Kampuni ya Kalamazoo, UIingereza, nani alishirikishwa na ziko wapi machine zilizoingizwa kwa kazi hizo. Tatu, ,ikononi mwetu (Chadema tuna karatasi za uchaguzi ambazo hazina maandishi kabisa maerlfu kwa maelfu kutoka vituo vya kupigia kura. Tumeuliza je ni Kampuni ya Kalamazoo ilituuzia Karatasi hizo hafifu(Kalamazoo ni Kampuni inayojulikana duniani kwa security printing) au kumetokea nini. Kama walituuzia Karatadsi hafifu ni kwanini hawakushitakiwa? Dr Slaa nimepigia kelele hayo wenye madsikio wamesikia na kuelewa na ndio msingi moja wa kura kuchakachuliwa. Nani kakurupuka Dr. Slaa au anayesema Dr Slaa Kakurupuka bila yeye kufanya utafiti au labda karukia tu hoja bila kujua msingi.

2) Hoja ya siku 9 kwa Kikwete kupunguza bei ya sukari. Ni mtanzania gani hajui kuwa kutokana na shinikizo hilo Kikwete katekeleza agizo la kushasha bei ya Sukari kutoka alichoita mwenyewe 2,200 hadi 1,700 na baada ya siku 3 kuishusha chini zaidi kuwa 1,500(japo Kikwete bila kupanga kashusha kwa kuagiza wauzaji wadogio kushusha beio zao kwa mlaji bila kujua kwanini imepanda,mwuzaji huyo naye alinunua kwa kiasi gani, nasa ni katika hatua gani inapanda(kukurupuka huko ndiko kunafanya agizo hilo lisitekelezeke) Lakini kwa maana ya agizo la Chadema Kikwete amelitekeleza ndani ya siku 9. Mtanzania gani hajui katika ziara zake kwenye wizara aliagiza bei ya Mafuta ya kupikia, sembe, maharage zishushwe? Kama agizo la Chadema limetekelezwa ila kwa kiwango gani na namna gani ni swala lingine. Ndiyo maana tumeendelea kumwita msanii, tumeendelea kumtaka kupunguza makali ya maisha kwa wananchi.

3) Kuhusu siku 21 za Umeya Arusha, kwanza ndugu yangu naona hata facts hujui. Agizo hilo ni la Kamati Kuu ya Chadema. Dr Slaa alikuwa tu mdomo wa kulifikisha kwa Watanzania kupitia Press Conference lakini siyo Dr Slaa alikurupuka tu. Naomba niweke hiyo record sawa. Kuhusu utekelezaji, Kamati Kuu popote haikutamka kuwa siku ya 22 tutafanya....Naomba soma vizuri na uelewe kabla ya "kukurupuka kuhukumu". Hata hivyo nataka niwahakikishie kuna mengi yamekuwa yaiendelea kutoka wakati huo ninaombanndugu yangu uvute subiri, mambo makubwa na magumu hayaendi kwa ushabiki.

Nadhani nimesaidia Jamvi kwa kutoa taarifa sahihi.

thanks for making it clear to them!
 
Napata shida kuchangia hapa kwa sababu 1 tu! Mwandishi mwenyewe kakurupuka kusema Dr slaa anakurupuka! Sababu alizozitaja zilishajadiliwa humu na ufafanuzi ulitolewa. Labda hakusoma au ni mgeni humu mi sijui. Ninapenda kuwakumbusha tu wana jf wenzangu kuwa tupo na mamluki ambao kwa sasa wameongezeka sana hasa baada ya kauli ya Msekwa kupambana nasi. Unaweza kuwatambua kwa thread na comments zao. Ni za kipuuzi, hazina utafiti na hata ukijaribu kuwaelewesha ni wabishi tena bila kutumia hoja! Na mwandishi ni m1 wao. Tuendelee tu kuwavumilia maana kwenye msafara wa mamba, kenge nao huwamo. Nimalizie kwa kumshukurt Dr. W. Slaa kwa kuwa karibu na sisi na kutufafanulia na kujibu maswali na hoja mbalimbali tena kwa haraka. Asante sana.
Nakubaliana na wewe muheshimiwa; watu wanaomuongelea Dr wa ukweli wanashindwa kutambua kuwa wanafanya dhambi kubwa sana na malipo yao yanakaribia kwani chama wanachokipigania kinaelekea kufa kisiasa. poleni sana wanasisiemu.
 
Ukitaka kujua mziki wa Dr Slaa kamuulize baba Ridhi moko ndio atakueleza kama ana kurupuka au la?Usije ukawa wewe ndio umekurupuka kuanndika hii thread hapa........Dr phd ya ukweli ndio raisi wa wananchi wa Tanzania hilo halina ubishi.....:spy::spy:
 
Ni kweli kuwa kuna kipindi anakurupuka na kusema mambo yasiyo na ukweli wowote. Hii siwezi kushangaa kwa sababu ndio tabia ya wanasiasa wetu. Hata wanaposhindwa kwenye uchaguzi hubisha. Mara nyingi wanazua mambo ya uongo ili kuvuta hisia za wananchi ambao mara nyingi huvutiwa na migogoro.
 
Dr Slaa ni kweli unakurupuka.wewe hukuzungumzia bei ya sukari maisha siyo sukari tt
tu.unajiliwaza bure hakim unachofanikiwa, ukumbuke uongo ni mfupi na hauchelewi kubainika. Juzi juzi ukiwa Maswa ulitangaza kifo cha mkuu wa mkoa wa Shinyanga ulitafit na ni kweli amekufa Kama siyo kukurupuka ni nini? Mbona hadith Leo hujaomba radhi? Unweza kuwadanya watu wachache kwa muda tu, lakini huwezi kuwadanganya watu wore wakati wote. ACHA kUKURUPUKA !

Mbona unaacha mambo ya msingi nakukimbilia mambo yasiyo na masilahi kwa taifa hili? Kifo au uhai wa mkuu wa mkoa vinamuathili vipi mtanzania?Rudi kwenye hoja aliyoiweka mchovu mwenzako huko mwanzo. Lakini sishangai hiyo ndio hulka ya watu mnaotumwa kazi za ovyo na makuwadi wenu.
 
Hapana bro,mwanasheria mkuu wa serikali inabidi akusanye ushahidi na kufungua mashtaka.Huu ni mhimili ambao kwa nchi nyingi za kidemokrasia ni muhimu sana,ila hapa kwetu,rais ndio tunaona kama anatakiwa afanye kila kitu.
Kuhusu chama kuwawajibisha,hiyo poa tu! kwani wewe inakuudhi nini?Ni gharama ndogo,haraka na haiitaji utaalamu mwingi wa kukusanya ushahidi.

Am afraid all evidence will implicate the president himself. Thats where the catch is......
 
Dr Slaa ni kweli unakurupuka.wewe hukuzungumzia bei ya sukari maisha siyo sukari tt
tu.unajiliwaza bure hakim unachofanikiwa, ukumbuke uongo ni mfupi na hauchelewi kubainika. Juzi juzi ukiwa Maswa ulitangaza kifo cha mkuu wa mkoa wa Shinyanga ulitafit na ni kweli amekufa Kama siyo kukurupuka ni nini? Mbona hadith Leo hujaomba radhi? Unweza kuwadanya watu wachache kwa muda tu, lakini huwezi kuwadanganya watu wore wakati wote. ACHA kUKURUPUKA !
Wewe ni sawa na mnyama asiye na utimamu wa akili za kibinadamu
 
Dr Wilbrod Slaa(Phd) amekuwa mwana siasa maarufu hapa nchini hasa kwa namna yake ya kuibua mambo mbalimbali mchanganyiko mengine yakiwa na ukweli na mengine ya kiwa hayana ukweli!

Suala la kutaja watuhumiwa wa ufisadi ni moja ya mambo aliyofanikiwa kwani hadi sasa hakuna hata miongoni mwa aliowataja hawaja enda kumshitaki mahakamani au wao kukanusha! Mengine ni pamoja na suala la Kontena la karatasi za kupigia kura alilosema limetokea Afica ya kusini hadi leo hakuna ukweli wa jambo hilo!

Lakini pia amekua kua akitoa matamko yenye muda ambayo pindi muda unapo pita kuna kua hakuna hatua zozote zilizo chukuliwa! Mfano: Alimpa siku 9 Kikwete maisha ya watanzania yawe mazuri,Alitoa siku 21 serikali ihakikishe uchaguzi wa Meya unafanyika!

Juzi amempa Kikwete siku 90 awe amesha wafukuza Mafisadi ndani ya CCM! Dr Slaa lazima awe makini na ahadi za namna hii kwani zinatoa picha yake halisi ya kukurupuka katika siasa na inampunguzia heshima kwa Jamii. Ni bora awe anatoa siku hizo na utekelezaji Uonekane!

Je yaweza kuwa kwamba kati ya mambo ambayo uliwahi kufanya, uliwahi kujihusisha na ukabaji?
 
Ni kweli kuwa kuna kipindi anakurupuka na kusema mambo yasiyo na ukweli wowote. Hii siwezi kushangaa kwa sababu ndio tabia ya wanasiasa wetu. Hata wanaposhindwa kwenye uchaguzi hubisha. Mara nyingi wanazua mambo ya uongo ili kuvuta hisia za wananchi ambao mara nyingi huvutiwa na migogoro.
Toa hoja zenye ushahidi kama unao wa yale aliyokurupuka na udhihirishe hilo kwa hatua zilizochukulia dhidi yake tokana na jambo alilolikurupukia. Vinginevyo, unacho sema hakina ukweli. Dr asingekubali kushindwa hata wewe sasa ungekuwa na akili timamu, ila sasa akili yako imefisidiwa na mfumo wa mambo wa sasa, Pole.
 
mnaweza kumlaumu bure huyu jamaa ila huyu c mzima kabisa laana ya kuiba mke wa mtu c mchezo nyie subirini tu iko siku nchi hii tutaongozwa na matahira.......
 
Nilishasema wageni humu watakuwa ni wengi
ma wengi wao watakuwa wametumwa sasa sijui kwa manufaa ya nani maana Kama ni hali ngumu inatukuta wote haijalishi unatetea chama cha magamba au vingine.Asante Dkt kwa kutusaidia kuwaelimisha hawa walotumwa.
 
Back
Top Bottom