Watanzania Wameanza kumuelewa Dr Slaa na Siasa za Kukurupuka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania Wameanza kumuelewa Dr Slaa na Siasa za Kukurupuka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mlengo wa Kati, Apr 21, 2011.

 1. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Dr Wilbrod Slaa(Phd) amekuwa mwana siasa maarufu hapa nchini hasa kwa namna yake ya kuibua mambo mbalimbali mchanganyiko mengine yakiwa na ukweli na mengine ya kiwa hayana ukweli!

  Suala la kutaja watuhumiwa wa ufisadi ni moja ya mambo aliyofanikiwa kwani hadi sasa hakuna hata miongoni mwa aliowataja hawaja enda kumshitaki mahakamani au wao kukanusha! Mengine ni pamoja na suala la Kontena la karatasi za kupigia kura alilosema limetokea Afica ya kusini hadi leo hakuna ukweli wa jambo hilo!

  Lakini pia amekua kua akitoa matamko yenye muda ambayo pindi muda unapo pita kuna kua hakuna hatua zozote zilizo chukuliwa! Mfano: Alimpa siku 9 Kikwete maisha ya watanzania yawe mazuri,Alitoa siku 21 serikali ihakikishe uchaguzi wa Meya unafanyika!

  Juzi amempa Kikwete siku 90 awe amesha wafukuza Mafisadi ndani ya CCM! Dr Slaa lazima awe makini na ahadi za namna hii kwani zinatoa picha yake halisi ya kukurupuka katika siasa na inampunguzia heshima kwa Jamii. Ni bora awe anatoa siku hizo na utekelezaji Uonekane!
   
 2. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hivi kumbe Slaa ndie amempa Kikwete siku 90 za kufukuza mafisadi? Mmh hili lisredi hili nalo jamani

  Mkuu hata kama ni msongo wa upweke unaweza tu kuvuta mto na usingizi ukaupata bila tatizo lolote kesho ukaamka fresh kabisa kuanza majukumu yako

  Uwe na usiku mwema na pole kwa upweke chijana
   
 3. p

  politiki JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  mheshimiwa labda kiswahili kinakupiga chenga hio ulizozitaja hapo siyo ahadi bali ni madai au wazungu wanaita demands za kuonyesha
  mtazamo wa chama dhidi maamuzi mengi ambayo hawakubaliani nayo kimsingi. cha msingi ni kushinda kwa nguvu ya hoja kitu ambacho chadema inaonekana kushinda ktk hilo kwa maana umma mzima huko nyuma yao na M-kiti wako anaonekana kuicheza ngoma hiyo kila kukicha.
   
 4. Chamoto

  Chamoto JF-Expert Member

  #4
  Apr 21, 2011
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 2,057
  Likes Received: 1,091
  Trophy Points: 280
  Huyu Dr. Slaa ni lazima atakuwa anawasumbua sana nyiyi kwenye vichwa vyenu. Yeye siyo kiongozi wa serikali lakini mnamwandama kweli. Yaani katika viongozi woote wa upinzani ni yeye tu mnaye mfuatafuata. Hii inaashiria kunakitu anawakuna sana nyinyi SISI 'EM, lazima atakuwa amewabana vilivyo, ndiyo maana hamuishi kumtajataja.
   
 5. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #5
  Apr 21, 2011
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Mbona contents za post yako zinakinzana na heading ya posts?Hivi aliyekupa jukumu la kuwasemea Watanzania ni nani hasa?Hivi mnalipwa kiasi gani hasa cha kuwafanya muweke kambi hapa mkiwa na ajenda muflisi ya kum-discredit Dkt Slaa?Na kwanini hamjaribu kufanya tathmini ya strategy yenu if it would ever work?

  Nadhani unasahau kuwa jitihada unazofanya zimeshajaribiwa huko nyuma na hazikuzaa matunda.Kama muungano wa Habari Corporation,Uhuru Publication,Tanzania Standard Newspapers (Habari Leo na Daily News) na TBC umeshindwa kumtenganisha Dkt Slaa na Watanzania anaowatetea utaweza wewe unknown entity?Usiwafanye Watanzania wapumbavu wa kutofahamu mwanasiasa gani yupo kwa maslahi yao na nani yupo kwa ajili ya tumbo lake,nyumba ndogo yake na ufisadi mwingine.

  Tatizo mlilonalo ni poor organisation.Huyo anaywafadhili kuandika upuuzi wenu hana akili ya japo kutengeneza mkakati madhubuti unaoweza angalau kuchota akili za mbumbumbu wachache.Kibaya zaidi,hamtaki kabisa kuelewa kuwa tatizo sio Dkt Slaa au kauli zake bali hao wanaompa ammunition.Unadhani kama CCM isingekuwa bahari ya madudu,ufisadi,etc then Dkt Slaa angepata wapi anayoongea?Au unadhani laiti hali za Watanzania walalahoi zingekuwa zinaboreka,wangejitokeza kwa wingi kwenye mikutano na maandamano ya Chadema (ambayo contrary na ile ya CCM hakuna takrima za usafiri,flana au vijisenti)?

  Nikusaidie kidogo ndugu yangu (yes bado ni ndugu japo mwenzetu umefunga ndoa ya mkeka na mafisadi) unaonaje ukitumia muda huo unaopoteza bure kumchafua Dkt Slaa kufanya jambo la msingi ktk maisha yako,which could as well be of benefit to your family and friends?Kwanini hutaki kujifunza kwa the likes of Tido Mhando,waliokuwa used and abused baada ya muda wa umuhimu wao ku-expire?Unaweza kuonekana muhimu kwa mafisadi at this moment lakini utatoswa as soon as umuhimu huo utapomalizika.Just like condom inavyokuwa muhimu kabla na during tendo la ndoa lakini baadaye kugeuka uchafu wa kutupwa haraka mara baada ya tendo,ndivyo hatma yako itakavyokuwa.
   
 6. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #6
  Apr 21, 2011
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Mbona contents za post yako zinakinzana na heading ya posts?Hivi aliyekupa jukumu la kuwasemea Watanzania ni nani hasa?Hivi mnalipwa kiasi gani hasa cha kuwafanya muweke kambi hapa mkiwa na ajenda muflisi ya kum-discredit Dkt Slaa?Na kwanini hamjaribu kufanya tathmini ya strategy yenu if it would ever work?

  Nadhani unasahau kuwa jitihada unazofanya zimeshajaribiwa huko nyuma na hazikuzaa matunda.Kama muungano wa Habari Corporation,Uhuru Publication,Tanzania Standard Newspapers (Habari Leo na Daily News) na TBC umeshindwa kumtenganisha Dkt Slaa na Watanzania anaowatetea utaweza wewe unknown entity?Usiwafanye Watanzania wapumbavu wa kutofahamu mwanasiasa gani yupo kwa maslahi yao na nani yupo kwa ajili ya tumbo lake,nyumba ndogo yake na ufisadi mwingine.

  Tatizo mlilonalo ni poor organisation.Huyo anaywafadhili kuandika upuuzi wenu hana akili ya japo kutengeneza mkakati madhubuti unaoweza angalau kuchota akili za mbumbumbu wachache.Kibaya zaidi,hamtaki kabisa kuelewa kuwa tatizo sio Dkt Slaa au kauli zake bali hao wanaompa ammunition.Unadhani kama CCM isingekuwa bahari ya madudu,ufisadi,etc then Dkt Slaa angepata wapi anayoongea?Au unadhani laiti hali za Watanzania walalahoi zingekuwa zinaboreka,wangejitokeza kwa wingi kwenye mikutano na maandamano ya Chadema (ambayo contrary na ile ya CCM hakuna takrima za usafiri,flana au vijisenti)?

  Nikusaidie kidogo ndugu yangu (yes bado ni ndugu japo mwenzetu umefunga ndoa ya mkeka na mafisadi) unaonaje ukitumia muda huo unaopoteza bure kumchafua Dkt Slaa kufanya jambo la msingi ktk maisha yako,which could as well be of benefit to your family and friends?Kwanini hutaki kujifunza kwa the likes of Tido Mhando,waliokuwa used and abused baada ya muda wa umuhimu wao ku-expire?Unaweza kuonekana muhimu kwa mafisadi at this moment lakini utatoswa as soon as umuhimu huo utapomalizika.Just like condom inavyokuwa muhimu kabla na during tendo la ndoa lakini baadaye kugeuka uchafu wa kutupwa haraka mara baada ya tendo,ndivyo hatma yako itakavyokuwa.
   
 7. D

  Dr Willibrod Slaa Verified User

  #7
  Apr 21, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 675
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  Mlengo wa Kati,

  Sina hakika na unachokiita ukurupukaji:

  i) Swala la Kontaina la karatasi za uchaguzi ni vema ulifanyie uchunguzi kabla ya kusema nimekurupuka. Nilitoa Namba ya Gari na Namba ya Container iliyoleta Karatasi toka Afrika Kusini hadi Tunduma upande wa Zambia. Ikafaulishwa kwenye Lori la azam kwa upande wa TZ. Taarifa ilitoka kwa maofisa wa Serikali, na kuthibitisha ukweli wa Taarifa hizo japo mimi sikuwa nimewataja mara moja asubuhi ile waliitwa Dar, na hatimaye kuhamishwa kituo cha kazi kwa taarifa niliyonayo. Kiravu na RPC Advocate Nyombi wakaishia kusema Dr Slaa ni mwongo badala ya kufanya uchunguzi huru. Polisi walihusika na tuhuma hizo, immigration na TRA wote walihusika kwanini wao waioshie kutukana badala ya ucunguzi huru?

  Pili Bungeni Waziri Mara alitangaza kuwa Serikali imenunua, machine na kuwa tayari ziliingia nchini, iweje ghafla serikali hiyo hiyo kupitria Tume kuwa sasa Karatasi zimechapishwa na Kampuni ya Kalamazoo, UIingereza, nani alishirikishwa na ziko wapi machine zilizoingizwa kwa kazi hizo. Tatu, ,ikononi mwetu (Chadema tuna karatasi za uchaguzi ambazo hazina maandishi kabisa maerlfu kwa maelfu kutoka vituo vya kupigia kura. Tumeuliza je ni Kampuni ya Kalamazoo ilituuzia Karatasi hizo hafifu(Kalamazoo ni Kampuni inayojulikana duniani kwa security printing) au kumetokea nini. Kama walituuzia Karatadsi hafifu ni kwanini hawakushitakiwa? Dr Slaa nimepigia kelele hayo wenye madsikio wamesikia na kuelewa na ndio msingi moja wa kura kuchakachuliwa. Nani kakurupuka Dr. Slaa au anayesema Dr Slaa Kakurupuka bila yeye kufanya utafiti au labda karukia tu hoja bila kujua msingi.

  2) Hoja ya siku 9 kwa Kikwete kupunguza bei ya sukari. Ni mtanzania gani hajui kuwa kutokana na shinikizo hilo Kikwete katekeleza agizo la kushasha bei ya Sukari kutoka alichoita mwenyewe 2,200 hadi 1,700 na baada ya siku 3 kuishusha chini zaidi kuwa 1,500(japo Kikwete bila kupanga kashusha kwa kuagiza wauzaji wadogio kushusha beio zao kwa mlaji bila kujua kwanini imepanda,mwuzaji huyo naye alinunua kwa kiasi gani, nasa ni katika hatua gani inapanda(kukurupuka huko ndiko kunafanya agizo hilo lisitekelezeke) Lakini kwa maana ya agizo la Chadema Kikwete amelitekeleza ndani ya siku 9. Mtanzania gani hajui katika ziara zake kwenye wizara aliagiza bei ya Mafuta ya kupikia, sembe, maharage zishushwe? Kama agizo la Chadema limetekelezwa ila kwa kiwango gani na namna gani ni swala lingine. Ndiyo maana tumeendelea kumwita msanii, tumeendelea kumtaka kupunguza makali ya maisha kwa wananchi.

  3) Kuhusu siku 21 za Umeya Arusha, kwanza ndugu yangu naona hata facts hujui. Agizo hilo ni la Kamati Kuu ya Chadema. Dr Slaa alikuwa tu mdomo wa kulifikisha kwa Watanzania kupitia Press Conference lakini siyo Dr Slaa alikurupuka tu. Naomba niweke hiyo record sawa. Kuhusu utekelezaji, Kamati Kuu popote haikutamka kuwa siku ya 22 tutafanya....Naomba soma vizuri na uelewe kabla ya "kukurupuka kuhukumu". Hata hivyo nataka niwahakikishie kuna mengi yamekuwa yaiendelea kutoka wakati huo ninaombanndugu yangu uvute subiri, mambo makubwa na magumu hayaendi kwa ushabiki.

  Nadhani nimesaidia Jamvi kwa kutoa taarifa sahihi.
   
 8. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #8
  Apr 21, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,274
  Likes Received: 19,420
  Trophy Points: 280
  big up dokta kwa kutoa ufafanuzi unaeleweka, nadani huyu jamaa ashafungika mdomo, labda aje na point za jazba ila hana hoja nyingine hapa
   
 9. j

  junior2008 JF-Expert Member

  #9
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 528
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lazima tuwe serious hivi unaposema Dr Slaa anakurupuka, utasemaje kuhusu akina Nape Nnauye na secretariet yake ya CCM wanaopita mikoani kuzungumzia mambo ambayo hayakujadiliwa na CC wala NEC ???????????
   
 10. chuki

  chuki JF-Expert Member

  #10
  Apr 21, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,691
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Dr Slaa ni kweli unakurupuka.wewe hukuzungumzia bei ya sukari maisha siyo sukari tt
  tu.unajiliwaza bure hakim unachofanikiwa, ukumbuke uongo ni mfupi na hauchelewi kubainika. Juzi juzi ukiwa Maswa ulitangaza kifo cha mkuu wa mkoa wa Shinyanga ulitafit na ni kweli amekufa Kama siyo kukurupuka ni nini? Mbona hadith Leo hujaomba radhi? Unweza kuwadanya watu wachache kwa muda tu, lakini huwezi kuwadanganya watu wore wakati wote. ACHA kUKURUPUKA !
   
 11. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #11
  Apr 21, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,682
  Likes Received: 637
  Trophy Points: 280
  2) Hoja ya siku 9 kwa Kikwete kupunguza bei ya sukari. Ni mtanzania gani hajui kuwa kutokana na shinikizo hilo Kikwete katekeleza agizo la kushasha bei ya Sukari kutoka alichoita mwenyewe 2,200 hadi 1,700 na baada ya siku 3 kuishusha chini zaidi kuwa 1,500(japo Kikwete bila kupanga kashusha kwa kuagiza wauzaji wadogio kushusha beio zao kwa mlaji bila kujua kwanini imepanda,mwuzaji huyo naye alinunua kwa kiasi gani, nasa ni katika hatua gani inapanda(kukurupuka huko ndiko kunafanya agizo hilo lisitekelezeke) Lakini kwa maana ya agizo la Chadema Kikwete amelitekeleza ndani ya siku 9. Mtanzania gani hajui katika ziara zake kwenye wizara aliagiza bei ya Mafuta ya kupikia, sembe,maharage zishushwe? Kama agizo la Chadema limetekelezwa ila kwa kiwango gani na namna gani ni swala lingine. Ndiyo maana tumeendelea kumwita msanii, tumeendelea kumtaka kupunguza makali ya maisha kwa wananchi.

  With all due respect Dr,bei ya sukari duniani ilikuwa ikiongezeka kwa kasi tangu mwezi wa nane 2010,kutokana na mambo mbali mbali kama vile natural disasters zilizoikumba BRAZIL,kupanda kwa bei ya mafuta(leading to ethanol as a cheaper alternative)n.k.
  Kwa mwezi march na April bei ya sukari imeshuka kwa takriban 329 points(almost 10% if yuo know what that means).Najua uli demand JK apunguze bei,ila ukiangalia kwa undani bei ya sukari kupungua is just a reflection of the world sugar index.
  You are a politician,a great politician,so I expect you to politicize this trend and coincidentially it worked because you are rumbling with a government that is weak ind misinformed.
  Thanks but no thanks,your demands didn't really affect the decline!

  World food prices fall for first time in eight months
  (AFP) – Apr 7, 2011
  ROME - World food prices fell for the first time in eight months in March after record highs largely due to oil prices, though the situation remains volatile, the UN's food agency said on Thursday.
  The Food and Agriculture Organisation's Food Price Index dropped to an average 230 points in March, down 2.9 percent from its peak in February, but still 37 percent above March 2010, the Rome-based agency said.
  "The decrease in the overall index this month brings some welcome respite," said David Hallam, director of the FAO's trade and market division.
  "But it would be premature to conclude that this is a reversal of the upward trend," he added.
  The FAO index, which monitors average monthly prices for key staples, showed international prices for oils, sugar and cereals in particular had dropped.
  Rice prices also fell, largely as a result of abundant supply in exporting countries and sluggish import demand. By contrast, dairy and meat prices rose.
  "The biggest story is the oil sector, that's the driver behind the decline in prices," said Abdolreza Abbassian, FAO economist and grains analyst.
  "The drop was driven by sell-offs in the market, but didn't last," he said.
  "We saw a decline only in the first two weeks of March. In the second half of the month prices rebounded. Most of the price increase is not captured in this index but is likely to be reflected in the next one," he said.
  March was also extremely volatile for grains, largely due to growing economic uncertainties and the turmoil in North Africa and parts of the Near East as well as the Japanese earthquake and tsunami, the FAO said.
  "We need to see the information on new plantings over the next few weeks to get an idea of future production levels," Hallam said.
  "But low stock levels, the implications for oil prices of events in the Middle East and North Africa and... Japan all make for continuing uncertainty and price volatility over the coming months," he said.
  The oil and fats price index fell 19 points in March, breaking nine months of consecutive increases, while the sugar price index averaged 372 points -- down as much as 10 percent from the highs of January and February.
  The dairy price index averaged 234 points, up 1.9 percent from the previous month and 37 percent above its level in March 2010, while the meat price index changed little from its February levels at an average of 169 points.
  "As we have said before, this crisis will be volatile. The prices are still at very high levels. It all depends on the 2011 harvest. The market is not going to ignore uncertainty for at least the next six months," Abbassian said.
  World food prices hit record highs at the beginning of the year and the agency had warned in March that oil price spikes could push them even higher as increasing violence in Libya sent jitters through commodity markets.
  "With many poor communities already feeling the effects of higher food prices and grain stocks in the main food exporting countries at dangerously low levels, sighs of relief in response to today?s announcement by the FAO would be premature," Oxfam's policy advisor Luca Chinotti said in a statement.
  "Food remains far too expensive for many poor people," he said.
  Copyright © 2011 AFP. All rights reserved.
   
 12. Elungata

  Elungata JF-Expert Member

  #12
  Apr 21, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 28,022
  Likes Received: 8,504
  Trophy Points: 280
  slah mbona namsoma tu humu ndani.haonekani kwenye tv au imekuaje?
   
 13. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #13
  Apr 21, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,682
  Likes Received: 637
  Trophy Points: 280
  With all due respect Dr.....bei ya sukari haikupungua kutokana na shinkizo lako,imepungua kutokana na kupungua kwa bei ya sukari katika soko la dunia,that's according to FAO.
   
 14. I

  IRAQW MINING Member

  #14
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 18, 2011
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dr yupo vzr achen mzaha na dr.
   
 15. regam

  regam JF-Expert Member

  #15
  Apr 21, 2011
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 268
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Naungana na mchangiaji mmoja kuwa laiti kama ccm wangetekeleza ilani yao cdm wasingekuwa na cha kuongea. Tukijaribu kufuatilia mambo yanayotokea kwa sasa ndani ya ccm, ni ukweli usiopingika kwamba ccm wanajaribu kutekeleza yale baadhi yetu tunayodhani cdm wamekurupuka. Ni ukweli usiopingika kwamba kama cdm wasingeongoza haya mapambano, kusingekuwa na kujivua magamba.
   
 16. D

  Dr Willibrod Slaa Verified User

  #16
  Apr 21, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 675
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  Sailor1
  Kama ungelikuwa makini ungelisoma kwanza post yangu kuhusu "kutaja kifo cha Dokta Ballele" na kisha ndiyo uzungumze. Kwa kuwa hujasoma au kwa kuwa unakataa makusudi sina sababu ya kujibizana. Haya kama Dr Slaa na Chadema hatujazungumzia Sukari, siku 9 unazozungumzia zilikuwa za nini. Mbona mtoto wa miaka miwili atakushangaa kwa hoja zako. Sitapoteza muda kujibizana nawe kwa sababu haina tija na kuna ajenda muhimu zaidi na muda ni fedha. Nitaendelea kuwaelimisha wana/JF wenye nia ya kweli kutaka kujua ukweli   
 17. n

  niweze JF-Expert Member

  #17
  Apr 21, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Unapewa inform kama raia na kazi ni yangu na ya kwako kuchukua hatua. Kwa mawazo yako, unataka Dr Slaa awaweke ndani na chombo cya JK sio? Unachotakiwa ni ku-pressure your government to investigate na kama hakuna ukweli mbona hawaendi mahakamani kufungua kesi za kutaka Dr Slaa afikishwe mahakamani? Hizi ni docs Dr Slaa na Chadema na wananchi wanazo, kwa faida ya watanzania wananchi wanafanya kazi kubwa kupata hizi docs. Mafisadi wanaogopa kwenda kumshitaki Dr Slaa kwasababu watachunguzwa na kukutwa ni ukweli. Msaidie Rostam afungue kesi basi ili tuone kama yeye sio fisadi. Kuwa mzalendo na pigania nchi yako achene kutumia kama watumwa.
   
 18. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #18
  Apr 21, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,340
  Trophy Points: 280
  Kobello, You're absolutely out of touch. Unajitahidi sana kutumia data za duniani ku justify hata yale usio na uhakika.
  Waziri mkuu wa Tanzania, Mh Mizengo Kayanza peter Pinda (MB) alikutana na wafanyabiashara wa sukari. Katika mambo aliyoyagundua ilikuwa ni uhujumu wa kuficha sukari ili kuleta upungufu na bei kupanda. Haya si maneneo yangu ni ya Waziri mkuu.
  Akaendelea, hakukuwa na sababu ya kupanda bei ya sukari kwani nyingi ipo maghalani. Ni baada ya tamko hilo sukari ikashuka bei. Hii ilifuatia maandamano ya Chadema kanda ya ziwa na shinikizo kutoka kwa wananchi. Baada ya taarifa ya waziri mkuu sukari ikateremka bei kuonyesha kuwa hakuna mahusiano kati ya data zako za FAO, kupanda bei za mafuta au ethanol.

  Pili, kwa viwanda tulivyonavyo na matumizi yetu ya bidhaa kama sukari ni kidogo kuweza kutetereka kwa siku chache kunapotokea matatizo ya uzalishaji duniani. Kwa nchi zenye matumizi makubwa hili linaweza onekana siku chache sana.

  Tatu kupanda kwa bei za mafuta inaweza kuwa sababu, lakini kwa serikali makini ipo njia ya kupunguza makali kwa walaji(consumers) kwa kutumia upandaji wa bei. Kwa mfano lita ya mafuta inachajiwa kwa % ya VAT, kuongezeka kwa bei ya mafuta hakusimamishi %, kwa hiyo ilikuwepo loophole ya kupunguza kodi kwa bidhaa muhimu kama sukari bila kuathiri mapato ya taifa.
  Hii imefanyika marekani ulipo, Uingereza na Canada wakati bei ya mafuta ilipofikia kiwango cha juu, waliondoa kodi za usafirishaji wa bidhaa hasa vyakula ili kutoa unafuu na bila kuathiri makadirio ya mapato.

  Kama unaufahamu zaidi ya waziri mkuu, basi weka jamvini, lakini takwimu za FAO haziwi supported na Rais au Waziri mkuu wa nchi yako.
   
 19. Salanga

  Salanga JF-Expert Member

  #19
  Apr 21, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 375
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mara zote kila jambolina watu wanaopinga aidha kwa kujua au bila kujua

  Dk Slaa hakurupi bali wanaoshindwa kumwelewa ndio wakurupukaji,,,wengine hawana aibu kutetea mambo yanayowakandamiza watz.
   
 20. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #20
  Apr 21, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Napata shida kuchangia hapa kwa sababu 1 tu! Mwandishi mwenyewe kakurupuka kusema Dr slaa anakurupuka! Sababu alizozitaja zilishajadiliwa humu na ufafanuzi ulitolewa. Labda hakusoma au ni mgeni humu mi sijui. Ninapenda kuwakumbusha tu wana jf wenzangu kuwa tupo na mamluki ambao kwa sasa wameongezeka sana hasa baada ya kauli ya Msekwa kupambana nasi. Unaweza kuwatambua kwa thread na comments zao. Ni za kipuuzi, hazina utafiti na hata ukijaribu kuwaelewesha ni wabishi tena bila kutumia hoja! Na mwandishi ni m1 wao. Tuendelee tu kuwavumilia maana kwenye msafara wa mamba, kenge nao huwamo. Nimalizie kwa kumshukurt Dr. W. Slaa kwa kuwa karibu na sisi na kutufafanulia na kujibu maswali na hoja mbalimbali tena kwa haraka. Asante sana.
   
Loading...