Watanzania wameanza kuamka - Risasi zapigwa, wanachi waimba "tunataka tunataka"! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania wameanza kuamka - Risasi zapigwa, wanachi waimba "tunataka tunataka"!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mzee Mwanakijiji, Jul 22, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jul 22, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #2
  Jul 22, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu umechanganyikiwa au mbona unaita watanzania wote hao si asilimia chache tu
   
 3. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  I will differ with you Mzee MKJJ kwa hilo.
  Tatizo si kuamka bali elimu finyu ya matumizi ya barabara kwa pande zote , Serikali na wananchi.
  Pita pale Kunduchi na utakuta shoulder zote aidha magari yamepark au wananchi wanauza machungwa au zinakaangwa chips.
  Kwa hiyo mtembea kwa miguu anashindana na gari kutumia barabara, at his/her own risk
  Mabega ya barabara ni kwa matumis=zi ya watembea kwa miguu au emergency na si vinginevyo-enforcement ya hili halifanyiki!

  Suluhisho SI KUWEKA MATUTA. Kwa akili nyepesi basi pasingekuwepo haja ya kujenga barabara pale kama matumizi yake ni kwa waenda kwa miguu tu.
  Udhaifu huu mkubwa unaoneka sehemu nyingi nchini huku watu wakidhani pale baranbarani ni sitting room-elimu inahitajika hapo.Gari hata likienda kwa 5km/hr bado ltakukanyaga na kufa.
  Ni hapa nchini tu ambapo elimu ya matumizi ya barabara ni finyu sana.
  Naomba kuwasilisha
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Jul 22, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  sasa hao ni wachina?
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Jul 22, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  LG.. unachosema ni kweli.. lakini for now tatizo ni kuwa watu saba wameshakufa hapo, na wananchi wanasema wamechoka.. jukumu la kuwaelewesha nini kifanyike ni la serikali. Kwenye majanga na dhulma elimu peke yake haitoshi.
   
 6. Tindikali

  Tindikali JF-Expert Member

  #6
  Jul 22, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 770
  Likes Received: 555
  Trophy Points: 180
  Kwa kiasi kwamba matuta sio suluhisho nakubaliana nawe kabisa, yenyewe si salama. Tuta lilitaka kunidondosha njia panda mikoani kwa sababu mengi hayana tahadhari, unashtukia vuuuup, hilo hapo, ukilazimisha breki noma, ukilivaa na moto noma. Nakubali pia, mwendo mdogo unaweza kuua.

  Ambacho tunatofautiana ni kwamba nadhani mchangiaji wa kwanza yuko sahihi, wananchi wameanza kuamka kudai wanavyovitaka. Hata kama kuna kingine bora zaidi. Wacha wadai, serikali itatia akili.
   
 7. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #7
  Jul 22, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Mkuu, pamoja na kuwalaumu watembea kwa miguu kwamba hawajui matumizi ya barabara, mi naona tatizo KUBWA pia liko kwa madereva kwa magari. Madereva wetu wengi hawamjali kabisa mtembea kwa miguu awe amekosea alama za barabara au hata anapokuwa sahihi. Wenye magari wanajiona sana kwamba wao ni wao tu wakiwa kwenye magari yao. Hata mahali palipo na alama za punda milia barabarani ambapo ni sehemu maalum ya mtembea kwa miguu kupita /ku -cross tena si kwa kukumbia bali kwa kutembea, utakuta wenye magari hawasimami sehemu hizo wanakwenda tu tena kwa kasi. Ukiona dereva anasimama kuwapisha watembea kwa miguu wapite ujue trafiki yuko hapo karibu vinginevo jamaa yuko km 60 au 80 kwa saa. Je, kwa mwendo huo dereva ataacha kukanyaga watu?

  Unyama wa madereva wa mtindo huu wapo tanzania tu. Hukuti ushenzi wa aina ile katika nchi zilizoendelea. Waendesha magari wanaheshimu sana mtembea kwa miguu tena sana tuuuu! Hata kama mtembea kwa miguu amekosea sheria, yaani anakatisha barabara bila kuruhusiwa dereva lazima atasimama tu mtu apite zake. Fanya hayo hapa tanzania kama hujaenda kuzikwa leo. Wenzetu nchi zilizoendelea wanafuata sheria/alama za barabarani kwa kiwangi cha juu. Na hii inaepusha sana ajali licha ya kwamba wana magari mengi kama mchanga wa pwani. Mi naamini madereva wakibadilika, wakawa waungwana wataokoa sana maisha ya watu: hata pale watembea kwa miguu wanapojisahau. Kusema barabara imejengwa kwa ajili ya magari kwa hiyo mtembea kwa miguu na maisha yake si kitu ni kukosa utu kabisa. Maisha ni maisha hayarudi yakishapotea. Tusicheze nayo, wala hakuna mwenye maisha bora / ya maana zaidi kuliko ya mwingine.
   
 8. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #8
  Jul 22, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Ni mchezo mbaya sana polisi hawa wanaufanya. Yaani wanatishia kina mama na watoto kwa risasi za moto hewani. Ule wakati wa kuwatisha wananchi kuogopa polisi umeisha, huu ni wakati wa kuwafanya wananchi wawapende polisi. Polisi anatakiwa awe rafiki wa raia, hapo ilitakiwa kutumika busara tu ila kwa kuwa jeshi letu halina utaalamu wa kujua kuwa wanachofanya ni provocation kwa ku-pull trigger basi wajiandae kuwalaza watu harakati za kampeni zikianza.

  Wanatakiwa kujifunza kuwa katika advanced technology ya security and angry mob management, huwezi kuzuia vurugu kwa kuanzisha vurugu. Kupiga risasi hewani ni dalili mbaya sana hasa pale watu wanaofanyiwa hivyo wengi wao ni wanawake na watoto wasiokuwa na silaha. Wanamtisha nani?, au ndiyo kuendeleza ile dhana potofu ya kidikteta kuwa FFU = Fanya Fujo Uone?.

  Hii kitu inankumbusha mauaji ya mwembechai 1998, kwa wale tuliobahatika kuona habari iliyorushwa na ITV mara moja tu kabla hawajakatazwa kurudi kuirusha watakumbuka polisi walikuwa wakipiga risasi kama hivi, watu hawakimbii na kuanza kuokota mawe hapo ndipo sauti ya afande ilipoanza kusema ripige, jamaa anafyatua mtu anaanguka, anasema tena piga jamaa anafyatua mtu mwingine anaanguka, mpaka jamaa alipoambiwa piga akawa anasita na kutetemeka baada ya kuona walioanguka hawainuki. na baadae ITV wakatuonesha jamaa mmoja aliyeanguka huku kashika jiwe polepole mkono unaachia jiwe huku vidole vikitetemeka akikata roho na mwsho kutulia. Sasa wasitukumbushe image zile za uchungu na kuonesha kutokomaa kwa polisi katika kushughulikia matatizo ya raia wasio na silaha.
   
 9. dengeru

  dengeru Member

  #9
  Jul 22, 2010
  Joined: Oct 1, 2009
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  na mimi nasema watanzania wameanza kuamka,zamani ukiona risasi za moto zinapigwa ungetegemea watanzania wakimbie mbio vibaya sana laikini sana wanasimama na kuendelea kuimba''tunataka tunataka'' tunakoelekea nafikiri kuzuri'' begining is always tough
   
 10. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #10
  Jul 22, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Nafikiri ujumbe mkubwa uliopo hapa si kwa wananchi kutaka matuta, hiyo unaweza kuiona kwa mtazamo wa wananchi hawa ambao wengi wanafikiria kuwa njia pekee ni kuwafanya madereva waendeshe kwa mwendo wa kuwa na tahadhari. Tatizo kubwa hapa ni wananchi kukosa ulinzi wa serikali yao linapokuja suala la Public safety. Tanzania tunaona usalama wa raia ni kutoingiliwa na majambazi au kuonewa lakini hatuna utamaduni wa tahadhari. tahadhari inaweza kuletwa na mambo mengi ambayo yote ni wajibu wa serikali ambayo ipo kwa ajili ya watu wake. Kwa mfano

  1. Kuhakikisha kuwa sheria zote za kuwalinda raia zinafuatwa, hii ikiwa ni pamoja na kuwa alama za barabarani, kuadhibu wenye kuzivunja adhabu kali sana ikiwa ni pamoja na kufutiwa leseni na kifungo plus fine

  2. Kuzihudumia barabara zetu, yaani kila siku halamashauri ya eneo husika inakuwa na team ya kukagua wapi pamekuwa vipi na nini kifanyike kabla haijawa too late. Sisi bongo barabara ikiisha jengwa inabaki kuwa mwana mkiwa, hakuna ukarabati wala ufuatiliaji mpaka hapo itakapopitishwa bajeti ingine ya kuijenga upya.

  3. Utoaji wa leseni za udereva, hili ni suala ambalo ni tatizo kubwa sana bongo. unakuta makonda wanajifunza kupaki na kugeuza kituoni ikifika usiku wanakabidhiwa magari wanazunguusha, wanakusanya pesa na kumpatia traffic police na kupewa leseni kama wananawa vile

  Sasa mambo kama haya huwezi kuyaleta kwa kutishia wananchi kwa risasi za hewani, bali ni kutekeleza wajibu wa serikali na kama ingekuwa ni nchi zilizo na demokrasia ya kweli ya uchaguzi yaani wananchi hawakupigii kura kama hutawalinda basi tungeshuhudia leo hii wananchi hawa wasingepewa majibu ya risasi za hewani bali angalau wangeahidiwa pipi tu kuwa serikali itajenga hayo matuta na baada ya siku mbili unaleta vibrator na lory moja la Asphalt concrete au hata zege la simenti kama asphalt huna bajeti na vibao vya kuonesha mbele kuna matuta shughuli inaishia hapo wakati mnasubiri uchaguzi uishe mtekeleze sera zenu za kimagirini.
   
 11. N

  Nick Member

  #11
  Jul 23, 2010
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 55
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Kweli Bongo kuna shida. Tatizo huwa linaongezewa tatizo bila kutatua tatizo. Ni kweli usalama wa raia ni muhimu na usafiri ni muhimu vile vile. Swala la kulaumu madreva angali waendaeo kwa miguu hawajali magari si haki. Ndio kuua sio haki na kudhara magari sio haki vile vile. Naona kutatua tatizo hapo ni, mipaka ya barabara izingatiwe na kuheshimiwa. Watu wasiingilie kwa kujenga, kufanyia biashara au shughuli nyingine mbali na usafirishaji.
  Aliyesema nchi zilizoendelea huheshimu waendao kwa miguu hata kama wamekosea si kweli. Tazama nchi nyingi hakuna matuta. Ni hapa bongo tuu. Endapo utaingia highway kwa kukosea hapo ndipo mwisho wako na kusababisha wingi wa ajali ambazo hazikutarajiwa.
  Tafadhali tuheshiane na kutii wajibu wetu.
  Mungu ibariki Tanzania
   
 12. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #12
  Jul 23, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Bongo yapo matuta kutulazimisha madereva kusimama au kupunguza kasi kwa nguvu tadhani hatuna akili na utashi. Ni ukweli usiopingika Ulaya kwa mfano madreva wangekuwa kama sisi huku sijui kungekuwa na ajali ngapi: kwanza kuna magari mengi kama utitiri, pili msongamano wa watu ni mkubwa sana. Lakini kuna usalama mkubwa kuliko hapa kwetu, japo sisi magari yetu huwezi kuyalinganisha kwa wingi na yale ya London, au Paris, au Berlin. Lakini ajali kila kukicha. Aibu yetu. Mpaka tuwekewe matuta????
   
 13. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #13
  Jul 23, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,473
  Likes Received: 5,852
  Trophy Points: 280
  Hivi wakigonwa watu wawili au watatu pale Luthuli Road yatawekwa matuta pi?
   
 14. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #14
  Jul 23, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  WKUU,
  Mimi bado narudi katika ELIMU ya matumizi sahihi ya barabara,
  Nalipongeza gazeti la NIPASHE toleo la leo 23/07/2010 kwa tahriri yake ya kuelezea tatizo linaloikabili jamii juu ya matumizi bora ya barabara zetu.
  Usipoitumia barabara vizuri ni kichocheo cha KIFO na ulemavu wa maisha.
  Nanukuu NIPAHE(leo 23/07/2010
  "KWA UPANDE MWINGINE WANANCHI(JAMII) IMEBWETEKA SANA, WATU HAWAJALI JUU YA MATUMIZI BORANA SAHIHI YA BARABARA;SHERIA ZINATIZAMA ZAIDI MADEREVA WAWAJIBIKE HATA PALE UZEMBE WA WAZI UNAPOKUWA NI WATUMIAJI WENGINE WA BARABARA.
  KUTOKUWEPO KWA UTARATIBU WA KUWAWAJIBISHA WANANCHI, KUMEKUWA NI KICHOCHEO CHA BAADHIYAO KUPUUZA KANUNU NA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI......."

  Ndugu zangu kama nilivyosema hapo awali, watu wanauza machungwa, nguo, kwenye kingo za barabara ,wengine wamegeuza kuwa maegesho ya malori au magari.
  Hivyo hakuna mahali pa emergency itokeapo hitilafu ya gari au chombo cha moto.
  Sasa hivi wengi hili tunaliona kama ni jambo la kawaida, polisi au mgambo wakiwakamata watu hao ,tunasikia kila aina ya utetezi.
  Sasa ajali zimeanza kuua watu kwa sababu wanshindania kutembea kati kati ya barabara kwa kukosa sehemu ya kupita ukingoni.
  Hii inatokea hapa Tanzania tu(na pengine nchi nyingine za dunia ta 3)
  Serikali iwe na ukali wa kusimamia matumizi sahihi ya barabara na wananchi inabidi waendelee kuelimishwa juu ya hilo.
   
 15. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #15
  Jul 23, 2010
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kaka Mwanakijiji huu ni uamsho chanya na kamwe hatupaswi kuushabikia. Hapa sio kuwa watanzania wanatambua haki yao bali ni dalili za utamaduni wa kutoheshimu sheria na dola ambao ni hatari kwa jamii yoyote ile. Hizi ni dalili mbaya kwa upande wa watawaliwa na watawala kwa pamoja na hauna faida kwa yeyote yule.

  omarilyas
   
 16. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #16
  Jul 23, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
  Ebo! Sasa viongozi wa serikali wanapofikiri walichaguliwa ili wavae suti na kusafiri huku wakisahau wananchi waliowapa madaraka unafikiria ni nini matokeo yake? Mwanakijiji ashabikie au asishabikie hataweza kubadilisha hali halisi! Ni juu ya hao viongozi kuzuia hii hali kwa kutimiza wajibu wake. Na kama wewe ni mwandishi wa habari inabidi ubadilike... uache kuhongwa fedha ili upindishe ukweli kwa manufaa ya hao wasanii wanaofikiria urais ni kusafiri na ku-enjoy!!!
   
 17. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #17
  Jul 23, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
  Haya yoooooooote uliyoeleza yanatokea kwa sababu watawala wako likizo! Ni matokeo ya serikali kulala muda mrefu! Watawala wanafikiri uongozi ni kula maisha
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  Jul 23, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  guess what.. a day after the confrontation:

  [​IMG] THEIR voices have been heard! Labourers cut a portion of Kunduchi Beach Road in Dar es Salaam to put up a hump on Thursday morning following Wednesday's accident involving a mini bus which killed one pupil of Mtakuja Primary School and injured a schoolmate. The pupils complained bitterly. (Photo by Robert Okanda)
   
 19. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #19
  Jul 23, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,415
  Trophy Points: 280
  Wow! Just wow! I am super impressed, by the people, of course.
   
 20. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #20
  Jul 23, 2010
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  ukienda kariakoo watu wanauza vitu pembeni ya barabara lakini watu hawagongwi na magari, sababu ni kuwa kariakoo magari ni mengi sana na huwezi kukimbiza na ukigonga mtu unaweza na wewe mwenyewe kupoteza maisha na hii imeingia akili mwa madereva.
  pale kunduchi hamna magari mengi na unaweza ukakimbiza gari sana tu

  mimi binafsi siku moja nilikuwa nawahi mjini barabara ya africana(old bagamoyo chini) nikafika kwenye tuta nikasima nikaruhusu watoto wavuke nyuma yangu kulikuwa kuna magari matatu gari la nne lika tu overtake kidogo liue wale watoto, wale watoto walikwepa lile gari kama mpira wa rede. baada ya hapo nikaanza kufukuzana na yule jamaa mpaka kwenye junction ya tank bovu akasimama kulikuwa na polisi pale nikamwambia huyu jamaa ni reckless driver na alichofanya, yule polisi aliniona mimi mwendawazimu na niache kuingilia kazi yao
   
Loading...