Watanzania waliushangaza ulimwengu kwenye korona, wameushangaza tena kwenye Uchaguzi Mkuu

Guys uchaguzi umeisha sasa ni muda wa kuijenga Tanzania.
Upinzani ni kwenye sanduku la kura na kampeni. Sasa ni wamoja na rais ni mmoja. Haya mnayoyaongea hayana maana kwasababu watanzania wako busy na kazi zao.

Leteni fursa watu tuamshe nazo
 
Mbona hamziongelei mbinu zilizo tumika kufikia hayo malengo,mbona taifa liko kimyana huzuni kuu imetamalaki? kwa mtizamo wako unaona watanzania wako sawasawa na furaha tele au? kilichotokea zanzibar kila mtu anakijua, kwa staili hiyo ulitarajia mtu aende kuandamana richa ya kuwa ni haki ya kikatiba, nawashauri enyi mnaotambia watu hebu nyamazeni ongeleeni maendeleo sio tambo za ushindi! huu ushinda umepatikana kwa gharama kubwa,na wenye akili wako kimya.
Tanzania ni taifa ambalo limezidi kuwashangaza wengi ambao hawalijui kwa undani.

Hakuna suala ambalo limeshangaza wengi duniani kama mbinu iliyotumika nchini ili kupambana na janga la korona. Hata wale ambalo mwanzo walikuwa hawakubaliani na mbinu hizo na walipiga kelele imebidi wakubaliane baadaye huku wengine wakiamua kuwa kimya baada ya kile walichokuwa wanakitegemea (maiti kuzagaa barabarani) kutotokea.

Uchaguzi Mkuu pia umeshangaza baadhi ya watu wasioijua vizuri Tanzania baada ya kutotokea kile ambacho walikuwa wanakisubiri kwa hamu baada ya kuaminishwa kuwa kitatokea.

Kabla ya Uchaguzi Mkuu, kuna baadhi ya watu waliamini kutatokea machafuko nchini baada ya Uchaguzi Mkuu lakini fikra zao zimewashangaza wenyewe! Wanaojiita ''wajuzi'' wa masuala ya kisiasa nchini waliandika sana na kutoa utabiri ambao baada ya uchaguzi, utabiri wao umekuwa ni takataka!

Umati uliokuwa unahudhuria mikutano ya Tundu Lissu ulimpumbaza hata yeye akadhani anaweza ''kuliamsha dude'' na likaamka wakati wowote akitaka! Siku ile anahitimisha kampeni zake alikuwa anatoa maneno ya vitisho kwa serikali, CCM na Tume ya Uchaguzi akiamini kuwa umati wa Watanzania utaitikia wito wake!

Siku tatu baada ya Uchaguzi Mkuu, viongozi wakuu wa ACT-Wazalendo na CHADEMA wakajaribu kuitisha maandamano wakitegemea Watanzania wengi watajitokeza. Kauli zao zilikuwa zinaonyesha wanaamini wananchi wataitikia wito huo bila kujua kuwa Watanzania ''hawasomeki'' kirahisi. Hakuna aliyeitikia wito huo!

Tuliambiwa Rais Magufuli atakuwa ni Rais wa kwanza nchini kuwa Rais wa awamu moja na aking'ang'ania Ikulu ''atafurushwa'' kwa nguvu ya umma! Wengine wakaenda mbali zaidi na kudai eti ameishalegea mpaka anapiga magoti kuomba kura! waliotuaminisha haya yote sijui kwa sasa wako wapi!

Wiki mbili zimepita baada ya Uchaguzi Mkuu, ukitembea nchini unaweza kudhani haukufanyika Uchaguzi Mkuu kutokana na watanzania kuendelea na kazi zao kama kawaida. Yaani mitaani watu hawaongelei tena Uchaguzi Mkuu, kwenye mtandao hasa wa Instagram kinachoongelewa kwa sasa ni Diamond Platnumz, wanawe na Zari zebosslady!

Hakuna cha maandamano wala vurugu! Hawa ndio watanzania wanaoishangaza dunia hasa wale wasiowajua vizuri watanzania!

Ama kweli, ''ukiona vinaelea lazima ujue vimeundwa lakini kikubwa zaidi, waundaji bado wapo!

Watanzania mnazidi kuishangaza dunia mpaka!
 
Kinachoshangaza zaidi, chama kwa sasa kinafanya shughuri zake kwa kutegemea wanaharakati.

CHADEMA ilikuwa imeishapita harua ya uanaharakati. Walitakiwa wakiendeshe kama chama kinachosubiri kupewa nchi/dola
Tatizo chadema walizani wanakubalika baada ya kuiteka mitandao ya kijamii. Ila ukweli kuhusu anguko lao ulikuwa wazi Sana. Tatizo hawashauliki wamejawa na kashfa na matusi.
Na lichama lenyewe ndio lishajifia
 
Tanzania tuna mtindo wa kuupuuza mambo,corona afrika haijasumbua watu,acha uongo ,korona afrika nzima imegonga mwamba
 
You nailed it!
Comment yako pia imenifanya nimecheka!
Acha tu, tukianguka kwenye maisha au mashindano kama haya ya uchaguzi huwa kwanza tunaugulia kipigo tukiwa chini, tunanyanyuka, tunajisafisha, tunaanza upya tena kwa plan zilizojengeka, wenzetu wanajisahau mpaka unapokaribia uchaguzi, basi wanaanza purukushani wakiongozwa na watu wasio kwenye ground, wakiwa nje hata kujuwa mbinu hakuna, kung'ang'ania uanaharakati wakisahau hizi ni siasa, hawajakaa sawa wanashangaa wanapata kipigo kikubwa zaidi kuliko cha nyuma..
Hawa wakinzani wetu ndorobo kabisa,,
 
Yule mbelgiji alikuja kufurahisha genge tu! Alijua kabisa hatoshinda! ,eti ooh nitawaingiza wananchi barabarani! Mara sujui hapatakalika ! Haya kikowapi sasa! .Kiufupi jamaa alikua na washabiki kwenye mikutano yake na sio wapiga kura! Watanzania walikua wanamchora tu ,kashapata somo sasa!.Arudi kwa Amsterdam.
Binafs Kampeni zake zilikuwa zikinipa maswali mengi Sana, kila mahali alikoenda, ni lazima aulize! Ruvuma mko tayari???

Unajiuliza, wako tayari katika nini!

Bwege Sana huyo Jamaa, na aende Tu, Hana faida Wala hasara Kwa awaye yote, yupoyupo Tu!!!
 
Kinachoshangaza zaidi, chama kwa sasa kinafanya shughuri zake kwa kutegemea wanaharakati.

CHADEMA ilikuwa imeishapita harua ya uanaharakati. Walitakiwa wakiendeshe kama chama kinachosubiri kupewa nchi/dola
Chadema aliondoka nayo Dr Slaa. Kibaya zaidi wanalaana ya kumtusi na kumkashfu eti sababu alipinga fisadi Lowasa asigombee Urais kupitia ukawa.
 
Mtaani kwetu tulizika mtu na mke kwa interval ya siku mbili...watu maelfu walikufa hata leo tukipimwa takwimu zitatisha
 
Aisee. utafikiri mpira wa simba na yanga, kumbe hizi ni marathon, maandalizi, pumzi, mbinu na spidi ya kipepe wakati wa kumaliza mashindano..
Nakumbuka Membe aliwaambia ushindi sio kuangalia idadi ya watu wanaokuja kwenye mikutano bali ni mbinu inayoanzia chini kwenye nyumba na nyumba!

Mikutano ni tukio la mwisho katika chaguzi!
 
Haitakuja kutokea tena, magu alikimbilia chato karibia miezi 2. Kisa corona.

Afu leo unaleta upupu hapa.
 
Nakumbuka Membe aliwaambia ushindi sio kuangalia idadi ya watu wanaokuja kwenye mikutano bali ni mbinu inayoanzia chini kwenye nyumba na nyumba!

Mikutano ni tukio la mwisho katika chaguzi!
Unafikiri hata walimsikiliza basi, angalia walivyomtupa, jamaa siasa bado kabisa. Wao wanaharakati..
 
Mtaani kwetu tulizika mtu na mke kwa interval ya siku mbili...watu maelfu walikufa hata leo tukipimwa takwimu zitatisha
"Watu maelfu" ---- UONGO WENU GHASHASHI TUSHAWAZOEA SANA TU kiasi ambacho tunaweza kupredikti nini mnachoweza kusema neksti.
 
Upinzani ni fikra zinazokinzana na watawala,wengi wetu humu wala hata sio wanasiasa na hatujawahi kuwa hata wanachama!Hivyo basi kama mlitegemea kwa ushindi huo mnaouita wa kishindo ndio kwamba upinzani umekufa basi mmepotea njia!Tunaendelea na maisha ila mtashangaa tunaendelea kuwapinga na kuwakosoa!
Bado tupo tupo sana😁😁!
Mkuu;
Mawazo kukinzana ni nafsi ya binadamu!

Tuendelee kukinzana kifkra na sio kutukanana na kudhalilishana!
 
Back
Top Bottom