Watanzania waliokwama India kwa sababu ya Corona kurejeshwa nchini hivi karibuni

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,480
9,241
3322c2029d226975a7fe6ef7b98d24dc


Ubalozi wa Tanzania nchini India umeeleza kuwa unaendelea kuandaa utaratibu wa kuwarejesha nchini Watanzania waliokwama India.

Katika taarifa yake, ubalozi huo umesema kuwa utahusika katika kuomba vibali vya ndege ya Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) kutua katika Jiji la Mumbai tarehe 11 Mei 2020 kwa ajili ya safari ya tarehe 12 Mei 2020 ya Mumbai-Dar es Salaam.

Aidha, ubalozi umebainisha kuwa utahusika katika kuwaombea vibali wale wote watakaokuwa wamelipia tiketi ya ndege hiyo ili waweze kutoka sehemu walipo na kufika Mumbai kwa ajili ya safari hiyo.

Ubalozi umewasisitiza Watanzania waliokuwa wamekwama nchini India baada ya kukamilisha matibabu na wanafunzi waliohitimu masomo yao kuchangamkia fursa hiyo adhimu.
 
Ila watu walioko huko wanalalamika sana kwamba nauli ni kubwa kupita kiasi, nauli ni US dollar 850 inakaribia Tsh 2 million kuja tu
 
Ubalozi wa Tanzania nchini India umeeleza kuwa unaendelea kuandaa utaratibu wa kuwarejesha nchini Watanzania waliokwama India.
This is why I always thank Allah who gave us such a strong president in our country, the government is really listening to it's people. Good!

Welcome back guys. Being out of your country was definately difficult. Poleni sana wajomba.
 
Aisee mie sirudi kwa hali jinsi ilivyo sasa hivi china ni safa zaidi kuishi hasa kwa kuepuka corona kuliko nchi nyingi
 
Dunia itamuelewa tu Rais Magufuli.
 

Attachments

  • IMG_20200510_181931.jpg
    IMG_20200510_181931.jpg
    163.4 KB · Views: 1
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom