Watanzania wako vizuri ukiangalia shule za kulipia zilivyo nyingi mtaani

Huu ni kuonesha shule za sirikali ni majanga na hamna kitu ni dhaifu hata kama hawataki kuambiwa serikali ni dhaifu ndo tunasema sasa mpaka wabadilike
Ndio maana nikasema serikali imeshindwa kusimamia swalal la elimu. Mbona miaka ya 90 kurudi nyuma shule za serikali zilifanya vizuri sana, hakukuwa na hizi shule za kila mtaa? Kuna mahali hapako sawa.
 
Unaandika nyuma ya keyboard ikiwa leo kuna watu hawana hata chakula
Huu utitiri wa ST .. kwa nursery, primary & secondary ni janga la Kitaifa. Kama serikali inashindwa kusimamia vizuri shule zake. Je, hizi STs zinawezaje/ Au wakaguzi wa Elimu wakifika katika shule hizo wanapewa kitu kidogo? Sidhani kama kuna walimu wazuri sana kule ! Pia michango nayo ni mingi kuanzia usafiri wa gari la shule, kama mtoto yuko std 4, form 2 and 4 wanaongeza gharama eti ya tuition wakati mzazi analipa kwa kujibu wa utaratibu uliwekwa wakati anamuandikisha mtoto shule! Kwa hiyo, nakubaliana na wewe kuwa wengine tutajikuta uko katika umaskini pamoja na watoto kwa vile kila senti unayopata inalipa ada za shule. Na hali hii inasababisha wazazi asiwe waaminifu katika kazi zao hasa watumishi wa umma ili wapate pesa kwa njia zisizo halali
 
Back
Top Bottom