Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,595
- 215,272
Watanzania tuishio nje ya nchi (TANZANIA DIASPORA) tumeanza kuandamana kupinga UCHAFUZI uliofanyika juzi hapo nyumbani Tanzania!
Hawa ni ndugu zetu kutoka Ulaya ya Kaskazini (Sweden 🇸🇪, Norway 🇳🇴 na Denmark 🇩🇰) ambao tayari wameanza maandamano yao nje ya Ubalozi wetu uliopo Stockholm, Sweden.
Watanzania tuishio nchini hapa Ufaransa 🇫🇷 tunaandaa maandamano hayo kesho Jumatatu, November 2, 2020 nje ya Ubalozi wa Tanzania 🇹🇿 nchini Ufaransa 🇫🇷.
Maandamano yataanza saa 2 asubuhi na kumalizika saa 6 mchana!
Baada ya maandamano, WAZANZIBARI tuishio nchini hapa, kwa kuongozwa na Balozi wetu (BABU MZANZIBARI), tutazindua Ubalozi wetu (Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar nchini Ufaransa) Ofisi za Ubalozi wetu zipo mitaa ya TROCADÉRO, karibu sana na mnara wa EIFFEL, jijini hapa PARIS.
Kwa niaba ya Wazanzibari wote waishio nchini hapa Ufaransa, mimi, BABU MZANZIBARI, Balozi wa Zanzibar nchini Ufaransa, natumia fursa hii kuwakaribisha ndugu zetu Watanzania waishio nchini hapa, katika uzinduzi wa Ubalozi wetu!
Usafiri, kula, kunywa ni kwa gharama yangu mwenyewe!
Kwa kauli moja, tumekubaliana kuwa hatuitambui serikali haramu ya John Pombe Joseph Magufuli! Hatuitambui serikali haramu ya Hussein Ali Hassan Mwinyi!
Rais wa Zanzibar tunayemtambua ni Maalim Seif Sharif Hamad aliyechaguliwa na wananchi wa Zanzibar!... Na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunayemtambua ni Tundu Antipas Lissu, aliyechaguliwa na Watanzania!
Mungu ibariki Zanzibar yenye mamlaka kamili, Mungu ibariki Tanzania! 🙏🏾