Watanzania waishio nje wahimizwa kuwekeza nchini..............

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,468
911,181
Watanzania waishio nje wahimizwa kuwekeza nchini

Wednesday, 08 December 2010 19:28 newsroom




Na Yassin Kayombo
SERIKALI imewashauri Watanzania wanaoishi na kufanyakazi nje ya nchi, kutumia fursa zilizopo za uchumi kuwekeza nchini. Ushauri huo, ulitolewa juzi na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Lazaro Nyalandu, alipozindua ndege za kampuni ya Bold Air inayomilikiwa na mtanzania anayeishi Marekani, John Ndunguru. Kwa mujibu wa Ndunguru kampuni hiyo ina ndege mbili ndogo Cessna 310 na Senetor 1 zenye uwezo wa kubeba abiria sita kila moja na itakuwa inaongeza idadi ya ndege kulingana na mahitaji.

Katika uzinduzi huo uliofanyika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julias Nyerere, Dar es Salaam, Nyalandu alisema kwa kufanya hivyo, Watanzania hao licha ya kusaidia kuinua uchumi wa taifa, wataongeza ajira nchini. Naibu Waziri alisema, serikali inakusudia kufanya marekebisho kwa baadhi ya vipengele vya sheria zilizounda Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), ambazo zinasababisha ukiritimba na usumbufu kwa wawekezaji wa ndani na nje. Alizitaja baadhi ya kasoro zinazokatisha tamaa wawekezaji kuwa ni utitiri wa kodi na leseni, ambapo alisema huu ni wakati mwafaka kwa serikali kuzipitia upya na kuzifuta zile zinazoonekana kuwa kikwazo kwa wawekezaji.
Hata hivyo, alitoa mwito kwa Watanzania kuzisoma sheria za TIC kupitia majarida mbalimbali na kwenye mtandao badala ya kulalalamikia utaratibu unaopaswa kufuatwa na wawekezaji, kwa kuwa baadhi ya vipengele vinatoa nafuu kwa wawekezaji wazalendo.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Ndunguru aliiomba serikali kupunguza ukiritimba kwa wawekezaji wazawa kwa kuwa inawakatisha tamaa katika kuwekeza.
Akitoa mfano, Ndunguru alisema, hakuna sababu kwa mwekezaji Mtanzania kumchukua miezi mitatu kukamilisha taratibu za kupata kibali cha uwekezaji kama ilivyo kwa wawekezaji kutoka nje.
 
Hii ni habari njema, ila hata zikirekebishwa sheria nina wasiwasi na utendaji kwenye idara kuu TIC, BRAC na TRA, huko utitiri, usumbufu na ukiritimba ni mkubwa, huko kwenye hizi idara watendaji hawafuati sheria na vitabu kwa vile rushwa imeshika mizizi.
Kwa kweli serikali ina kazi nzito kuwavutia wawekezaji ukizingatia ushindani toka nchi kama Rwanda ambayo wamejitahidi sana kuweka mazingira bora kwa wawekezaji.
Kidogo kidogo tunaweza kufika.
 
Waziri nadhani hana uelewa sawasawa wa hali ilivyo hapo nchini. Akitaka kusikia madudu baadhi yetu tuliyokwisha fanyiwa ajaribu kutukaribisha wale ambao tumeshafanyiwa unyama katika harakati za kutaka kuwekeza hapo nchini tuje tumweleze mambo mazito. Asizungumzie tu majukwaani atuite ofisini tuje tumwonyeshe jinsi wengine tulivyowahi kuingia hasara hapo nchini. Kuna baadhi yetu tumejenga majengo yako tayari kuanzisha shughuli muhimu kama training centres na Hoteli ya kitalii lakini tumekatishwa tamaa utafikiri sisi ni wageni wa kutoka nchi za mbali tunavamia nchi. Tafadhali kama kuna mwenye uwezo amfikishie ombi langu, akituita tukamwonyeshe pamoja na vithibiti vya kumtosha tuone hatua serikali itachukua. Loh! Mungu ibariki Tanzanania.
 
Back
Top Bottom