Watanzania waishio nchi za Shirikisho la Urusi kuzindua jumuiya (TANCORU) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania waishio nchi za Shirikisho la Urusi kuzindua jumuiya (TANCORU)

Discussion in 'International Forum' started by Tanzania Russia, Nov 30, 2011.

 1. T

  Tanzania Russia New Member

  #1
  Nov 30, 2011
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Wajumbe wa kamati maalumu ya watanzania waishio Urusi, Jumamosi ya Novemba 26, 2011, walikutana ,ikiwa ni mfululizo wa vikao vya kujadili azma na mchakato wa Uzinduzi rasmi wa Jumuiya ya Watanzania Urusi .The Tanzanian community in Russia(TANCORU).

  Katika kikao hicho kilichofanyika Jijini Moscow,na kuhudhuriwa na wawakilishi toka miji mingine ,ambapo pamoja na mambo mengine , wajumbe walipata nafasi ya kujadili kifungu kwa kifungu Mapendekezo na Muundo wa Uongozi na Rasimu ya Uanzilishi wa Jumuiya ya TANCORU.

  Katika kuweka kumbukumbu sahihi,JUMUIYA YA WATANZANIA URUSI, (TANCORU) ni jumuiya inayowaunganisha Watanzania wote waishio na kufanya kazi katika nchi zote za lililokuwa Shirikisho la Urusi .

  Ni jumuiya ISIYO ya Kisiasa, kidini, Kikabila au Kijinsia ambayo inaheshimu mawazo mbalimbali ya wanajumuiya wake yanayolenga kujenga na kuimarisha umoja wa Jumuiya nzima.

  Ni jumuiya itakayowaunganisha watanzania waishio Urusi na asasi za Serikali na taasisi Binafsi nchini Tanzania na Afrika kwa Ujumla.
  Lengo na madhumuni ya TANCORU pamoja na mambo mengine ni Kuyapa kipaumbele mambo muhimu yanayohusu maendeleo ya nchi yetu katika nyanja mbalimbali kama vile Elimu, Afya,Uwekezaji,Utalii,na Ustawi wa jamii ya watanzania .

  Katika majadiliano hayo, wajumbe wa kamati hiyo, wamekubaliana kuipitisha rasimu ya awali ya Uanzilishi wa Jumuiya na Muundo wa Uongozi wake.
  Wajumbe wameafikiana uwepo wa mawasiliano na watanzania wote kupitia mtandao wa jamii wa facebook na email ili kuendelea kukusanya maoni ya wadau katika kuboresha Rasimu ya Uanzilishi wa Jumuiya ya TANCORU.

  Mwisho kamati maalumu ya Uanzilishi inatarajia kufanya Mazungumzo na Mheshimiwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Urusi Kapten Mstaafu JAKA MWAMBI mapema juma lijalo kwa lengo la utambulisho wa Jumuiya ya TANCORU ,na majadiliano ya mchakato wa Uzinduzi unaokusudiwa kufanyika katika kilele cha miaka ya 50 ya uhuru wa Tanzania bara.

  Imetolewa na:
  Kurugenzi ya Mawasiliano,
  TANCORU. 144 leninskii Praspect . Email: tancoru@yahoo.com. MOSCOW–RUSSIA.
  27 Novemba, 2011.
   
 2. m

  magesa jr Member

  #2
  Nov 30, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Doh! Sielewi mliwasiliana vp na watz nje ya moscow. Si tunasoma ryazan, mwendo wa 2hrs kwa gari toka moscow lkn hatukupata hii news.
   
 3. T

  Tanzania Russia New Member

  #3
  Nov 30, 2011
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  swala la mawasiliano ni muhimu , !! wasiliana na kurugenzi ya mawasiliano kwa email hii tancoru@yahoo.com or kwenye facebook search Tanzania Russia, na jiunge ktk fb group THE TANZANIAN COMMUNITY IN RUSSIA(TANCORU) . Nafikili tunahitaji kufahamu zaidi mko wangapi na majina kamili ili tuwapatie further details ;
   
 4. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #4
  Nov 30, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Pamoja sana, Harashoo. Sasa ni kwenda kujichana Vodka na Kalubasa kwa saaana tu mara baada ya kufungua. Na zdrove, SPASIBA :)
   
 5. M

  Marytina JF-Expert Member

  #5
  Dec 1, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  wengi wenu ni pro-ccm hamna maana
   
Loading...