Watanzania, Waingereza na Warusi ni ndugu moja?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,864
155,822
Balozi wa Uingereza kwanini anatutafuta hivi? Ni nchi ngapi za Afrika zimelaani kitendo kinachosemekana kuwa ni Urusi kujaribu kuua wakala wake bwana Sergei Skripal na bintiye Yulia kwa sumu iitwayo "novichok"? Swali refu eeh? Bado sikumalizia sehemu ya tukio lilipotokea huko Salisbury Uingereza.
Sasa balozi anatutaka Tanzania tuungane nao kulaani hilo,nashangaa inaonyesha Uingereza in a balozi mmoja Afrika nzima naye ni huyu wa Tanzania. Au inaonekana Tanzania ndiyo Afrika yenyewe,ukisema Tanzania unasema Afrika. Tanzania tupo juu sana basi. Sijasikia nchi yoyote ya kiafrika ikilaani hilo,sisi tunatakiwa tufanye hivyo,wakati wao walishindwa hata kusema chochote tulipogwaya kuongea chochote na kudai haki za ndugu yetu Dokta Shika ambaye mimi kwa mtazamo wangu naona ni kweli alidhurumiwa na warusi biashara yake na pesa zake.Mtu anayetoka kwenye nchi masikini mno,ambayo ni mwanachama wa jumuiya ya madola ya Uingereza. Hawakutusaidia kwenye hilo dogo wanataka sisi tulaani mambo yao wanayofanyiziana huko hii si fair...
Sisi watanzania kama binadamu wa walivyo hatukubaliani na vitendo vyovyote vya dhuruma ya uhai wa mtu yoyote yule,na ndiyo maana hata mauaji mbalimbali yaliyosikika sehemu mbalimbali hapa nchini ambayo hatujui nani wanayafanya yamekuwa yakipingwa na kupigiwa kelele,hata ajali za barabarani za kizembe tu zinazogharimu maisha ya watu tunazipinga na kulaani vikali tu,kwa hiyo hata hiyo ajue tu hatukubaliani nalo,ila asitutake tutoke tuanze kulaani Urusi kwa hilo,huku wakiwa bado wanavutana na warusi ambao nao wanakana kuhusika(japo natia shaka,ile mijamaa ya ovyo mno). Wasitake kutupambanisha kwenye hilo.
Nani kati yenu ninyi wadau mtakaopitia hapa kusoma mumesikia nchi yoyote ya kiafrika imeilaani Urusi kwenye hilo suala wanalohusishwa nalo? Waingereza wajue tu tunawaunga mkono lakini wasitutake tutoe tamko.
 
Uingereza wapuuzi wanajua nguvu ya Tanzania na pia uhusiano wake na urusi ndio maana wametoa kauli hiyo

Pia , naona vita ya cold war imeisha sasa inakuja vita ya live , ndio maana chokochoko zinazidi kwa kasi

Sisi misimamo wetu ni ileile NAM (Non Alignment Movement)
 
Wakati anataka tuwaseme Urusi amwambie PM wake atekeleze agizo alilopewa n Putin la kupeleka hiyo sample Urusi wakaifanyie uchunguzi ndio waone kama wao kama Urusi wana la kujieleza ama la.
Pia amkumbushe kuwa ile deadline aliyompa Putin ilishapia hivyo afanye yale aliyomtishia.

Akishajibiwa ndio aje mara ya pili na current story.
 
Tanzania sio Bendera, wapambane na hali yao tu.....
 
Back
Top Bottom