beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Hassan Abbas amehimiza Watanzania kujitokeza kwa wingi kuaga mwili wa Rais mstaafu, Benjamini Mkapa leo.
Aliwataka mawaziri na manaibu wao, wakuu wa mikoa na watumishi wote wa umma, sekta binafsi na wananchi wengine waende kumuaga Mkapa leo kwa kuwa kesho muda hautatosha.
Akizungumza na vyombo vya habari kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Dk Abbas alisema ni vema wananchi wakajitokeza leo kwa kuwa ratiba ya kesho Jumanne itakuwa ngumu kwao kupata nafasi kutokana na muda.
Hii inatokana na ratiba inayoonesha kwamba Rais John Magufuli ataongoza waombolezaji wa kitaifa na kimataifa kuaga mwili wa mzee Mkapa na baadaye mwili utasafirishwa mchana kupelekwa kijijini Lupaso, Mtwara kwa ajili ya maziko.
Dk Abbasi alisema serikali inaendelea kupokea salamu za rambirambi na pole na kwamba viongozi wa kimataifa wamethibitisha kuja kuaga na hivyo kutokana na ratiba hiyo inawezekana muda usiwe rafiki kwa viongozi na wananchi wote kupata nafasi siku hiyo.
“Nirudie tena kusema bado tunaendelea kupokea salamu za pole kutoka ndani na nje ya nchi, tunategemea kupata wawakilishi na viongozi wa kimataifa watakaoshiriki kuaga hiyo kesho, sasa muda hautakuwa rafiki kwa sababu baadaye siku hiyo, mwili wa mzee wetu utasafirishwa kwenda Lupaso kwa mazishi,” alisema Dk Abbasi.
Chanzo: Habari Leo