Watanzania Wadaiwa Kushikwa na Heroin Japan | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania Wadaiwa Kushikwa na Heroin Japan

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by X-PASTER, Dec 1, 2010.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Dec 1, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Watanzania Wadaiwa Kushikwa na Heroin Japan

  Polisi wa Yokohama katika mkoa wa Kanagawa wametoa taarifa rasmi kuhusiana na taarifa za kukamatwa kwa watanzania na madawa ya kulevya . Wamesema kuwa wamewakamata watanzania wawili baada ya kuthibitika kuwa walimeza dawa za kulevya aina ya Heroin katika matumbo yao.Wakwanza aliyetajwa kuanguka kwenye mikono ya wajapani ni Machenga Machenga Ally mwenye umri wa miaka 33 na Ally Mohamed Husein (37) ambao wanadaiwa kumeza kilogram 1.3 za heroin zenye thamani ya fedha za Japani zipatazo Millioni 78 kulingana na Polisi wa mkoa wa Kanagawa.


  Polisi hao wa Mkoa wa Kanagawa walisema kuwa Watanzania hao walikamatwa jumanne iliyopita ya Nov.23 wakiwa na kapsuli 5 kila mmoja zikiwa na gramu 13 za heroin zikiwa nyuma ya gari walilokuwemo. Awali Machenga Ally alimeza Kapsuli( capsules) 25 zenye ukubwa unaofanana na huo na tarehe 24 siku ya jumatano walilazwa hospitalini ambapo Machenga Ally alivitoa kwa njia ya haja kubwa kapsuli 10 na Husein kapsuli 40 Polisi wamesema kuwa watuhumiwa hao ambao wamekiri makosa yao waliondoka Tanzania tarehe 19 Novemba siku ya Ijumaa na kuingia Japani Novemba 22. Kilichowaponza kulingana na maelezo ya Polisi ni kuwa wenyeji wao katika eneo walilofikia alitoa taarifa Polisi katika mkoa huo wa Kanagawa kuwa jamaa zake walikuwa wakilalamika kuwa wanaumwa sana tumbo jambo liliwatia mashaka, hatimaye kila kitu kikawa hadharani.

  Hata hivyo kuhusika ama kutohusika kwao kutafahamika pale watakapofikishwa mahakamani na ukweli ukabainika. Kwa sasa wanabakia kuwa watuhumiwa... Magazeti mengi ya Japani hii leo yamekuwa yakitoa fursa watu kutoa maoni yao na mmoja alikuwa akiulizia Tanzania iko wapi....!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #2
  Dec 1, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Sasa tutajuulikana tuko wapi kama tulikuwa hatujuulikani. Duh hatari
   
 3. Deodat

  Deodat JF-Expert Member

  #3
  Dec 1, 2010
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 1,279
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hao jamaa nao vilaza, yaani wamekula ng'ombe mzima wameshindwa kumalizia mkia? kweli za mwizi 40. Wameweza kuvuka viunzi vya airport zote hizo wakashindwa kumalizia kuutoa mzigo.
   
 4. Deodat

  Deodat JF-Expert Member

  #4
  Dec 1, 2010
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 1,279
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Jamani mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, Siye (Tanzania) tulivyo mabingwa wa kununua magari ya mitumba (al-maarufu used cars) kutoka Japan, leo hata hawatujui tuko location gani? haya basi, Rais wetu anasafiri sana nje na huwa anatuambia anaenda kuitangaza nchi yetu, leo wanasema hawaijui Tanzania? Kweli maskini hata afanye juhudi gani, hawezi kujulikana!
   
 5. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #5
  Dec 1, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Hawaijui bwana. Rais wenu huwa anaenda kukutana na viongozi wa nchi za nje kwenye mahoteli makubwa kubwa, raia wa chini hajui hata Tanzania iko wapi seuzi rais wake ni nani.
   
Loading...