Watanzania: Wachuuzi / wajasiriamali wote sasa kulipia leseni za biashara zao

Mnwele

Senior Member
Feb 4, 2010
162
100
Katika kile kilichoelezwa wakati ulee kwamba serikali inafuta utaratibu uliokuwa unawalazimisha WaTZ wafanyabiashara kulipia leseni zao za biashara katika maeneo ya mamlaka wanayoishi/kufanyia biashara husika. Hii ilielezwa itapunguza bugdha na taharuki iliyokuwa unawakumba wafanyabiashara wengi ( wamachinga na akinamama) kwa ujumla wao iliyokuwa inachagizwa na MAAFISA BIASHARA katika ngazi ya Wilaya, Miji na JIJI.

Serikali ilikaririwa ikisema kwamba uamuzi huo ungewezesha vijana wengi zaidi na waTZ kwa ujumla wao kupata fursa za kibiashara, kuinua mitaji yao na hatimaye kujikomboa katika umaskini. Hata hivyo ni jambo lilowazi kwamba uaamuzi huu ulikuwa pigo kwa Maofisa wengi katika ngazi za Halmshauri hasa kitengo cha Biashara na Afya.

Hii ilipelekea watu wengi kulazimika kulipia gharama za gizani aka RUSHWA haswa pale unapollazimishwa ukaguzi wa eneo lako la biashara na maofisa Afya/Biashara.Hivyo basi ukweli ni kwamba wafanyabiashara wengi walikuwa wanakamuliwa pesa za mitaji yao na wengine waliamua kukacha kabisa baada ya kuona mlolongo usio na lazima.

Katika bajeti hii, jambo kubwa ambalo wadau hawalizungumzii na kulitolea kauli inayostahili ni hili linalowazimisha sasa wafanyabiashara wote nchini kukata leseni za Biashara katika mamlaka za kiutawala kwa eneo husika. Katika ngazi ya Halmashauri, kila mfanyabiashara atatakiwa kwa mujibu wa sheria itakayopitishwa na Bunge hili kulipa TSH 30,000/= kwa mwaka, na katika ngazi ya MJI ni 50,000/= na nadhani JIJI itakuwa juu ya fifty.

Hili ni swala zito sana maana sasa rungu limerudi kwa maofisa wa biashara na Afya maana mapato haya ni ya kiserikali na bado mjasiriamali ataendelea kukamuliwa malipo yasiyo rasmi yaani RUSHWA.

Haapa panaibuka hoja kubwa zinazokinzana na muundo wa nje na wa kimantiki wa bajeti ya 2011/2012 pamoja na kauli-mbinu (sio kaulimbiu) ya watu toka serikalini. Hili ni pigo kwa kila mtanzania na wafanyabiashara wengi wataishia mahakama za Jiji/miji (kama zipo) na hata katika mahakama za mwanzo na Wilaya. Mbaya zaidi kamatakamata ya bidhaa za biashara ndio itashamari rasmi kuanzia Julai Mosi.

Udhia huu utawakumba watu wote na ndipo hapo tunapotakiwa sasa kuacha tofauti zetu, tuungane na watu waliojipmbanua katika kupinga bajeti hii ili kufanya ndugu zetu na shangazi zetu vijijini na kokote waliko wasi[pate shida hii. Hapa ndip mlinganyisho wa posho na vipaumbele vingine vinapojitokeza, hapa ndipo vipaumbele vya kimaendeleo ya wananchi vinapoweza kuhojiwa na hapa ndipo hoja ya kuakisi ukuaji wa uchumi tunaoelezewa wa asilimia 7 unavyoweza kutafsriwa kwa kuwafikia atu wengi zaidi.

Hali ngumu na kama Wabunge wetu...haswa wa CCM hawataacha projo zao na kupiga meza, miguu na magoti, wale wote waliowachagua hawa jamaa watasaga meno na cha mot watakiona.

Jamani tukubali, pamoja na umuhimu wa KODI katika maendeleo yetu, lakini kwa hali ya Tanzania na mazingira ya biashara, KODI YA BIASHARA ni miongoni mwa KODI ZA KERO ambazo Mh Mkapa aliamua kwa makusudi kuziondoa.

Tunaimani na wabunge wote wa Upinzani ( sina hakika na CUF) kwamba watalipigania kwa ujumla wa bajeti yenyewe kwa wao kuwa jukwaa na vipaza sauti za wanyonge wa injii hii
 
Katika kile kilichoelezwa wakati ulee kwamba serikali inafuta utaratibu uliokuwa unawalazimisha WaTZ wafanyabiashara kulipia leseni zao za biashara katika maeneo ya mamlaka wanayoishi/kufanyia biashara husika.

Jamani tukubali, pamoja na umuhimu wa KODI katika maendeleo yetu, lakini kwa hali ya Tanzania na mazingira ya biashara, KODI YA BIASHARA ni miongoni mwa KODI ZA KERO ambazo Mh Mkapa aliamua kwa makusudi kuziondoa.<br>
Tunaimani na wabunge wote wa Upinzani ( sina hakika na CUF) kwamba watalipigania kwa ujumla wa bajeti yenyewe kwa wao kuwa jukwaa na vipaza sauti za wanyonge wa injii hii

Kama ni kweli, basi mimi naunga mkono.<br>Kila mtu anatakiwa alipe kodi. Hata kama ni sh 2000, anatakiwa kuchangia kwenye pato la Taifa. Niliona Uganda, hata machinga wanaotembeza vyakula kwenye vituo vya mabasi, wanalipia kamchango kadogo.

Kumbuka kuwa kuna wafanyabiashara ndogo ndogo ambao kwa muonekano wanaonekana wamechoka sana, lakini ukipiga hesabu ya matumizi yake, yanaonesha kipato chake kikubwa tu sawa na wafanyakazi wanaokatwa kodi.

Na kwa vile huduma za barabara, afya, ulinzi na usalama, wote tunazipata kwa kutumia hela ya serikali, basi kila mtu mwenye kipato achangie kodi. Hii itapunguza tabia ya serikali ya kutegemea kodi za sigara, pombe, wafanyakazi, na wenye magari tu.

Cha muhimu kwa wabunge ni kupigania kuhakikisha kuwa pesa zinazokusanywa hazitafunwi ovyo. Kama wabunge na serikali yetu wanahisi watashindwa kudhibiti ubadhirifu, basi hamna haja ya kutoza kodi kwa hawa wafanyabiashara wadogo.
 
Nafikiri hapo sasa waTZ wengi watakataa kukata leseni za Biashara. Na zoezi hilo litawanufaisha wasimamizi wa biashara kwenye vitongoji , kata na wilaya.

Budget kweli kiboko.
 
Back
Top Bottom