Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 8,935
- 6,844
Nakabiliwa na maswali machache:
a. Kwanini Watanzania wenye asili ya Uhindi au Uarabuni hawaingii kwenye vikosi vya usalama? Zamani nakumbuka tulikuwa tunawatania kuwa wao ni "watoto mayai" hawawezi kazi za shurba lakini nikagundua kuwa hata kule Uhindi na Uarabuni kuna majeshi na POlisi na wao wanapewa mafunzo ya kijeshi na kuhenyeka kama sisi. Hivyo suala la "umayai" halipo.
b. Ni juhudi gani zinafanyika kurecruit Watanzania hawa hasa kutokana na ujuzi wao wa mambo ya biashara, utaalamu wa IT, n.k n.k na hivyo kuleta vipaji ambavyo vinahitajika sana kwenye vyombo vyetu hivi?
c. NI kwa kiasi gani familia za ndugu zetu hawa zinawa encourage watoto wao kuitumikia nchi yao kwa zaidi ya siasa na biashara na kuingia kwenye utumishi wa umma. Watakuwa wanaendelea kutoa misaada tu mpaka lini.
Wahindi ni lazima wabadilike hilo halina ubishi...Wafanye tathmini wenyewe kwenye jumuiya zao waone ni kwa jinsi gani wataweza kufanya mambo ya kulisaidia Taifa na wananchi wao given the position they withhold in our society...Hilo tutalisimamia in any means neccessary....Na si kutowa misaada kwa ccm ambayo inaishia kwa mafisadi na rushwa kwenye uchaguzi ili kuendelea kuyalinda maslahi ya kibiashara nk.
Badala ya mawazo yao kuwa kwenye kuchuma na kupeleka nje na hatimaye kuhamia huko moja kwa moja...Wafikirie namna ya kuikwamua jamii ambayo imewawezesha kuupata utajiri wanaoupeleka nje ya nchi...Pia kuwa na utu na kuwathamini watu weusi na bila kuwanyanyapaa kwasababu zisizo za kimsingi.
Assimilation ni muhimu hilo halina ubishi kwetu tusiokuwa na mitizamo yoyote ya tofauti na uafrika halisi kwamba maslahi ya Afrika na mwafrika kwanza.
Katika nchi yeyote inayojidai kuwa ni demokrasia, uhuru wa raia wake kuchagua jinsi gani ya kutumikia taifa lake ni sacrosant. Mchango wowote atakaoutoa, katika nyanja yeyote ile ni lazima ithaminiwe. Tunapoanza kamchezo ka kusema kuwa utumishi katika sehemu fulani ndiyo uthaminiwe zaidi tutajiingiza kwenye matatizo. Mfanyabiashara anayewekeza na kutoa ajira kwa wanachi wake anastahili heshima sawa na mwanajeshi aliye klindoni katika mipaka ya nchi. Tusisahau kuwa utumishi katika hivi vyombo vya usalama si kila wakati ni matokeo ya uzalendo bali ni mtu kujipima uwezo wake ( shule aliyosoma, watu anaowajua n.k.) na kuona huko kuna uwezekano mkubwa wa kumpatia riziki. Vile vile mtu anayeamua kuingia katika biashara ni hivyo hivyo. Mara nyingi anafanya hivyo kutokana na sababu hizo hizo. Uwezo wake, network yake na kukosa nyenzo za kuingia sehemu nyingine. Mbona wengi tu baada ya vita vya Kagera, pamoja na kuahidiwa vyeo jeshini, tulikataa kujiunga? Utasema na sisi tulikosa uzalendo?
Kama tunaona tuna haja ya kuwa nao (kutokana na ujuzi,vipaji vyao au contact zao na si rangi yao au kabila yao) tuwatafute na kuwatongoza kujiunga na vyombo hivyo vya usalama kama vile ambavyo tunatakiwa kufanya kwa mtanzania mwengine. Rangi, uasili zitumike pale tu tunapoona kuwa hivyo vitatusaidia katika malengo yetu fulani. K.m. kama lengo letu ni kufanya espionage India basi bila shaka kuwa na mtu mwenye asili ya huko itasaidia. Au kama tunatarajia kuwa siku moja tutapigana na Oman, basi bila shaka kuwa na mtu mwenye asili ya huko kutasaidia. Lakini si vinginevyo. Kufanya vingine ni institutional racism. Kwetu sisi na sio kwa wao.
Hii institutional racism iko wazi katika tunavyojiangalia kama jamii. Kila kitu tunafanya kama vile mtanzania ni yule anayefanana na sisi. Hivi tumewahi kujiuliza ni vitu gani kati hizi institutions vinaendana tofauti na jadi zao? Wahindi wengi hawali nyama lakini katika vyombo hivi kama hauli nyama utakufa njaa! Si hicho tuu, sehemu nyingine utategemewa kushiriki katika kuchinja wanyama hawa. Mhindi leo umwambie achinje ng'ombe! Uchanganyikaji wa kijinsia katika vyombo hivyo inaweza ikawa kikwazo kingine. Si siri kuwa kama angetokeza mtoto wa Kihindi au Mwarabu wakati wetu wa JKT angegombewa na walafi kama mpira wa kona! Mzazi gani mwenye mapenzi na mtoto wake atamwachia aingie huko kama ana uwezo wa kumwepusha? Masingasinga dini yao inawakataza kukata nywele. Vyombo vyetu vya usalama, wembe ndiyo moja ya vitu vya kwanza ambavyo kichwa chako kitakutana nacho. Wanaume wote tuliopitia JKT tulinyoa mfano wa mustini! Institutional racism hii inaonekana vile na jinsi sisi tunavyowaangalia hawa jamaa kama vile wote ni matajiri na sleki. Akionekana mhindi, kitu cha kwanza kinachotuingia kichwani ni namna gani tunavyoweza kumminya ili atukatie kitu kidogo. Akitokea mhindi, mawazo yetu yote ni kuwa huyu ni lazima mkali wa hesabu na huko ndiko tunakompeleka. Katika vyama vingi vya professionals, nafasi ambazo wahindi wanapata bila matatizo mengi ni uweka hazina! hapana, wakuu, matatizo yako kwetu.
Katika dunia ya sasa hatuzungumzii asimilation bali integration. Katika assimilation unatakiwa ukane ulikotoka na uchukue identity ya nchi iliyokupokea. Katika integration, unategemewa kukubaliana na value za msingi lakini kubakia na tamaduni na lugha (yako ya asili na hiyo ya ugenini) n.k. Kwa wenzetu wanachukua hizi tofauti kama resources na si kikwazo. Canada wachina wa Vancouver wameiwezesha nchi yao mpya kupata biashara kibao na China n.k. Sisi kwetu tunaona mtu kupenda asili yao ni kukosa uzalendo. Leo tunamshangilia Obama ambae hafanyi siri ya kuwa na mapenzi makubwa na ukoo wa baba yake. Baba aliye mtelekeza.
Matumizi yetu ya majina kama mhindi, mwarabu, tukimzungumzia mtu ambae kwa generations amekuweko kwetu ni moja ya dalili ya kutowakubali hao. Wenzetu wanawatofautisha wananchi wao wenye asili ya nje kwa kutumia hyphens, African-Americans, Irish-Americans, Asian-Americans, Black-Britons n.k. Ni lini tutamwona mtanzania mwenye asili ya bara lingine na rangi iliyo tofauti na sisi kuwa anahaki sawasawa na sisi watengo? Haki hiyo ikiwa ni pamoja na kujichagulia wapi atakapotoa mchango wake kwa taifa lake!
Sisi tulio majority katika nchi hii. Inatubidi sisi tuwape nafasi na kuwahakikishia kuwa tunawathamini kama tunavyomthamini mtu mwingine. Ishara ya kuthamini huko ni jinsi tutakavyoheshimu utamaduni na imani zao kama vile tunavyoheshimu za wadengereko wenzetu.
Amandlaa........