Uchaguzi 2020 Watanzania, uongozi haujaribiwi. Chagua kwa ajili ya Uhuru na Amani ya Watanzania

Wagombea wote ni watanzania wazalendo!Hakuna kaburu hapo!Kila mtanzania akampigie kiongozi anayeona anafaa!
Hizi porojo nyingine tupa kule!
 
Tunamfahamu sasa vilivyo kuliko zamani. Alichowafanyia Watanzania, wengi wanafahamu. Yale tuliyoyategemea, sina haja ya kuyataja maana ni ya kawaida, na yalifanywa na watangulizi wake. Lakini yafuatayo yamekuwa dhahiri chini ya utawala wake:

1) Watu kuuawa na maiti kutupwa kwenye viroba

2) wanaomkosoa kupotezwa

3) wanamkosoa kushambuliwa kwa risasi

4) wanaomkosoa kubambakiwa kesi za uhujumu uchumi, kutakatisha fedha na madawa ya kulevya

5) sheria mbaya za kuminya uhuru wa maoni, uhuru wa vyombo vya habari, na haki mbalimbali za raia

6) kuvunja katiba na kutofuata sheria na migawanyo ya mihimili ya utawala

7) ubaguzi na upendeleo kwa misingi ya itikadi, kabila na maeneo

8) kuvuruga uchumi kwa kuendesha utawala wa kimabavu. Leo ukuaji wa uwekezaji na utalii, umeporomoka maradufu (uwekezaji toka 28% mpaka 4%; utalii toka 15% mpaka 3.6%)

9) udhalilishaji wa utu wa binadamu

10) kuvuruga chaguzi mbalimbali ukiwemo uchaguzi wa serikali za mitaa

Kumchagua tena, ina maana tunataka mambo hayo yaendelee. Nani anayeyapenda hayo? Tulimjaribisha, tumepata majibu. Majibu yamekuwa mabaya. Sasa tujaribishe mwingine.

Kwa nia ya kuokoa nafsi zetu na wenzetu, lazima tufanye mabadiliko.

Sent using Jamii Forums mobile app
Napenda nikupe majibu kwa kadiri ya uzito wa hoja zako kumi, Kama ulivyoziorodhesha.

1. Watu kuuwa na kuokotwa kwenye viroba hayakuwa matukio ya kwanza katika Tanzania na kwamba yalianza 2015. Ijapokuwa kudhibitiwa kwa uharifu na matukio ya ujambazi na ugaidi ndani ya Tanzania kumeimarika zaidi ya 90% tangu Rais John P. Magufuli aingie madarakani 2015. Kama labda waliokuwa wanauawa na kuokotwa kwenye viroba ni majambazi pengine ikasaidia, mimi sijui.

2. Wakosoaji wakubwa wa Rais Magufuli wameishi na kupatiwa hifadhi sawa Kama watanzania wengine. Wapo wakina Sheikh Ponda Issa wanaponda maisha hata Sasa, wakina Fatma Karume, Tundu Anthipas Lissu anagombea na Urais kabisa na kadhalika na kadhalika.. hoja yako ya Pili haina maana yoyote labda kama waliopotea ni kwa sababu za kiuharifu, ambapo vyombo husika vinaendelea na uchunguzi ili kubaini ukweli.

3. Matukio ya mtu au watu kushambuliwa kwa risasi hayathibitishwa kisayansi kwamba yanahusika na mambo ya kukosoana. Ila imethibitishwa pasipo kuacha shaka, kwamba waharifu hutumia silaha za kivita kushambulia mtu/watu wakiwa watekeleza matendo ya uharifu. Na ndio maana katika kila nchi, kuna vyombo vya ulinzi na usalama, vyombo vya upelelezi na usalama wa taifa ili kuwadhibiti waharifu.

4. Haijafahamika kama watumiaji wa madawa ya kulevya kwamba chanzo cha ugomvi na viongozi wao kwa sababu ya kuwakosoa ama kuwashauri. Isipokuwa imethibitishwa kisheria kuwa matumizi ya madawa ya kulevya pamoja na biashara ya madawa ya kulevya ni kosa kisheria. Kwa hiyo utakatishaji wa fedha, biashara ya madawa ya kulevya na mambo mengine yaliyozuiwa kisheria hayazuii mshauri au mkosoaji wa viongozi kushtakiwa ama kushutumiwa ikiwa Kuna viashiri vya yeye kushiriki haramu hizo.

5. Vyombo vya habari na matumizi mengine ya haki za mtu au taasisi katika mfumo wa utawala wa demokrasi, huwa unaratibiwa na kusimamiwa kwa mujibu wa Sheria za nchi. Sifa namba ya moja Sheria ni unyumbulikaji, Sheria hubadilika kuendana na nyakati na mabadiliko ya mfumo wa maisha ya watu. Lakin lengo linabaki kuwa ni kudhibiti tabia mbovu na mwenendo mbovu wa baadhi ya watu ndani ya jamii ya watu. Sheria ni kwa ajili ya uhai wa amani na utulivu wa watu ndani ya jamii. Na hakuna Sheria yo yote iliyotungwa na kupitishwa nchini pasipo wananchi kushiriki wa kupitia wawakilishi wao bungeni.

6. Sio kweli. Tanzania tumekuwa na mihimili mitatu imara ya serikali. Ipo mahakama, serikali kuu na Bunge. Na kila moja linatekeleza wajibu wake kwa misingi ya kisheria. Haijawahi kutokea Bunge kuhukumu ama kutafasiri Sheria, Mahakama kutunga au kuishauri serikali na serikali kuu kutunga Sheria au kuishauri na kuisimamia Mahakama. Bunge kwa muda mrefu imeishauri serikali ktk kutekeleza miundombinu imara ya uchumi wa nchi, pamoja kuimarisha huduma za kijamii kupitia wawakilishi wa wananchi Wabunge. Na serikali imekuwa ikikubali kushauriwa na kutekeleza. Sasa Tanzania inaonekana na imesimama kutokana na mawazo na ushauri wa wananchi.

7. Suala la ubaguzi na upendeleo kwa misingi ya itikadi, kabila na maeneo. Halina ushihidi, kwahiyo huu ni umbea wa mchana na ni ishara ya kukosekana kwa kazi ya kufanya. Hii ni sawa na ule umbea wa dikteta uchwara. Kwa hiyo madai yako hayo hayana ushihidi wa kimazingira wala kivitendo.

8. Sina haja ya kutolea majibu kwa sababu Dunia na mashirika ya kimataifa ya Fedha na Biashara imeshatoa taarifa za nchi kusini mwa Jangwa la Sahara zinazokua kiuchumi kwa kasi na ambazo zimepanda kuingia uchumi wa Kati 2020. Kwa wanaojua kusoma watakuja kukuambia humu kuwa Tanzania imeorodheshwa.

9. Udhalilishaji wa utu wa Binadamu ni kelele za mfa maji ni sawa sawa na hoja namba 7. Hizi ni hoja zenye asili ya uzushi na umbea. Haziwekujadilika kwa kuwa hazina maelezo ya kiushahidi.

10. Nchi yetu inaongozwa kwa misingi ya kisheria na kwamba ni hiari ya chama ama kishiriki au kutoshiriki. Na ni kosa la kisheria ikiwa mamlaka yo yote ile ikakishurutisha chama au taasisi kwa misingi ya kwamba kisipotekeleza chama au taasisi hiyo itafungiwa. Vyama kadhaa viliamua kutoshiriki uchaguzi ule kwa sababu viliona kuwa nafasi hizo hazina ruzuku hivyo having faida kwao kutumia pesa za chama kuwekeza katika serikali za mitaa na za vijiji.

Watanzania wengi ambao wanaelewa mambo katika uhalisia wake na kwamba sio watu wakushadadi stori za vijiweni na mabarazani yaanu umbea. Wote kwa pamoja tutaenda kumchagua Magufuli kwa miaka 5 Tena. Ili akaijenge nchi na kukuza uchumi wa watanzania.

#chaguamagufuli2020
 
Magufuli tumeiona kazi yake na akisema "nitafanya hiki" tunaweza kumuelewa kuwa atafanya kweli. Anahitaji muda kumalizia kazi alizozianza.
Kwa jinsi alivyokuwa akiwatetea bodaboda na "wanyonge" mtu asingetegemea "ushabiki mkubwa" dhidi yake. Hata kufanya kwake kweli kuhamisha makao makuu Dodoma ni matumaini yangu kuwa atapata kura nyingi za "watani" wake. Au ni kweli kuwa vijana hawana shukrani hata uwafanyie nini? Hawaoni, hawatambui?No appreciation? Tusubiri tuone.
 
Napenda nikupe majibu kwa kadiri ya uzito wa hoja zako kumi, Kama ulivyoziorodhesha.

1. Watu kuuwa na kuokotwa kwenye viroba hayakuwa matukio ya kwanza katika Tanzania na kwamba yalianza 2015. Ijapokuwa kudhibitiwa kwa uharifu na matukio ya ujambazi na ugaidi ndani ya Tanzania kumeimarika zaidi ya 90% tangu Rais John P. Magufuli aingie madarakani 2015. Kama labda waliokuwa wanauawa na kuokotwa kwenye viroba ni majambazi pengine ikasaidia, mimi sijui.

2. Wakosoaji wakubwa wa Rais Magufuli wameishi na kupatiwa hifadhi sawa Kama watanzania wengine. Wapo wakina Sheikh Ponda Issa wanaponda maisha hata Sasa, wakina Fatma Karume, Tundu Anthipas Lissu anagombea na Urais kabisa na kadhalika na kadhalika.. hoja yako ya Pili haina maana yoyote labda kama waliopotea ni kwa sababu za kiuharifu, ambapo vyombo husika vinaendelea na uchunguzi ili kubaini ukweli.

3. Matukio ya mtu au watu kushambuliwa kwa risasi hayathibitishwa kisayansi kwamba yanahusika na mambo ya kukosoana. Ila imethibitishwa pasipo kuacha shaka, kwamba waharifu hutumia silaha za kivita kushambulia mtu/watu wakiwa watekeleza matendo ya uharifu. Na ndio maana katika kila nchi, kuna vyombo vya ulinzi na usalama, vyombo vya upelelezi na usalama wa taifa ili kuwadhibiti waharifu.

4. Haijafahamika kama watumiaji wa madawa ya kulevya kwamba chanzo cha ugomvi na viongozi wao kwa sababu ya kuwakosoa ama kuwashauri. Isipokuwa imethibitishwa kisheria kuwa matumizi ya madawa ya kulevya pamoja na biashara ya madawa ya kulevya ni kosa kisheria. Kwa hiyo utakatishaji wa fedha, biashara ya madawa ya kulevya na mambo mengine yaliyozuiwa kisheria hayazuii mshauri au mkosoaji wa viongozi kushtakiwa ama kushutumiwa ikiwa Kuna viashiri vya yeye kushiriki haramu hizo.

5. Vyombo vya habari na matumizi mengine ya haki za mtu au taasisi katika mfumo wa utawala wa demokrasi, huwa unaratibiwa na kusimamiwa kwa mujibu wa Sheria za nchi. Sifa namba ya moja Sheria ni unyumbulikaji, Sheria hubadilika kuendana na nyakati na mabadiliko ya mfumo wa maisha ya watu. Lakin lengo linabaki kuwa ni kudhibiti tabia mbovu na mwenendo mbovu wa baadhi ya watu ndani ya jamii ya watu. Sheria ni kwa ajili ya uhai wa amani na utulivu wa watu ndani ya jamii. Na hakuna Sheria yo yote iliyotungwa na kupitishwa nchini pasipo wananchi kushiriki wa kupitia wawakilishi wao bungeni.

6. Sio kweli. Tanzania tumekuwa na mihimili mitatu imara ya serikali. Ipo mahakama, serikali kuu na Bunge. Na kila moja linatekeleza wajibu wake kwa misingi ya kisheria. Haijawahi kutokea Bunge kuhukumu ama kutafasiri Sheria, Mahakama kutunga au kuishauri serikali na serikali kuu kutunga Sheria au kuishauri na kuisimamia Mahakama. Bunge kwa muda mrefu imeishauri serikali ktk kutekeleza miundombinu imara ya uchumi wa nchi, pamoja kuimarisha huduma za kijamii kupitia wawakilishi wa wananchi Wabunge. Na serikali imekuwa ikikubali kushauriwa na kutekeleza. Sasa Tanzania inaonekana na imesimama kutokana na mawazo na ushauri wa wananchi.

7. Suala la ubaguzi na upendeleo kwa misingi ya itikadi, kabila na maeneo. Halina ushihidi, kwahiyo huu ni umbea wa mchana na ni ishara ya kukosekana kwa kazi ya kufanya. Hii ni sawa na ule umbea wa dikteta uchwara. Kwa hiyo madai yako hayo hayana ushihidi wa kimazingira wala kivitendo.

8. Sina haja ya kutolea majibu kwa sababu Dunia na mashirika ya kimataifa ya Fedha na Biashara imeshatoa taarifa za nchi kusini mwa Jangwa la Sahara zinazokua kiuchumi kwa kasi na ambazo zimepanda kuingia uchumi wa Kati 2020. Kwa wanaojua kusoma watakuja kukuambia humu kuwa Tanzania imeorodheshwa.

9. Udhalilishaji wa utu wa Binadamu ni kelele za mfa maji ni sawa sawa na hoja namba 7. Hizi ni hoja zenye asili ya uzushi na umbea. Haziwekujadilika kwa kuwa hazina maelezo ya kiushahidi.

10. Nchi yetu inaongozwa kwa misingi ya kisheria na kwamba ni hiari ya chama ama kishiriki au kutoshiriki. Na ni kosa la kisheria ikiwa mamlaka yo yote ile ikakishurutisha chama au taasisi kwa misingi ya kwamba kisipotekeleza chama au taasisi hiyo itafungiwa. Vyama kadhaa viliamua kutoshiriki uchaguzi ule kwa sababu viliona kuwa nafasi hizo hazina ruzuku hivyo having faida kwao kutumia pesa za chama kuwekeza katika serikali za mitaa na za vijiji.

Watanzania wengi ambao wanaelewa mambo katika uhalisia wake na kwamba sio watu wakushadadi stori za vijiweni na mabarazani yaanu umbea. Wote kwa pamoja tutaenda kumchagua Magufuli kwa miaka 5 Tena. Ili akaijenge nchi na kukuza uchumi wa watanzania.

#chaguamagufuli2020
Sina muda wa kupoteza kwa watu wanaoacha weledi nyuma, wanaamua kuongozwa na ushabiki, uwongo, na siasa za hila na hadaa.

Kwa vile Watanzania wana akili, wana macho, na ni mashuhuda wa yale yanayowazunguka, nina hakika wengi watamchagua mgombea ambaye atawatoa kwenye minyororo ya utumwa na ukoloni mpya unaofanywa na watanzania wenzao dhidi yao.

Mimi nitamchagua mtu ambaye atalinda haki ya kila mmoja, uhuru wa kila mmoja, na ataiishi falsafa ya mwasisi wa Taifa letu kuwa maendeleo ya kweli ni maendeleo ya watu. Na jweli hili, najua sipo pekee yangu bali ni mamilioni ya Watanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wagombea wote ni watanzania wazalendo!Hakuna kaburu hapo!Kila mtanzania akampigie kiongozi anayeona anafaa!
Hizi porojo nyingine tupa kule!
Sumu ni chakula, lakini haifai kuiliwa. Kwa hiyo ni wajibu wetu kutoa tahadhari kwa mustakabali chanya kwa maisha ya mlaji.
 
Habari za muda huu ndugu wanabodi wenzangu? Leo nimerudi tena baada ya takribani siku kadha zilizopita kuwa na majukumu mengine na hasa ya kiuchumi pamoja na ya kisiasa.

Tumetafuta kura za kutosha na kwa tathimini ya haraka tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuweza kuwafahamisha watanzania wengi nchini, kuhusu ilani yao pendwa na ahadi za kiongozi wao mpenzi. Na kutegemeana na matokeo ya tafiti ndogo zilizofanyika ni kwamba mgombea wetu na ilani ya chama chetu imefanikiwa kueleweka na kupokelewa vema, na hivyo upo uwezekano mkubwa wakupata idadi ya kura zaidi ya 90% ya wapiga kura watakaojitokeza.

Leo nimekuja kuendeleza kazi ile ya kutafuta kura ya ushindi wa kishindo kwa chama chetu pendwa na mgombea wetu mpendwa, chaguo la watanzania wazalendo.

Inafahamika kuwa historia ya binadamu haiwezi abadani kujitenga na historia ya amani, ya utulivu na ya uchumi. Binadamu amekuwa akitafuta amani, utulivu na uchumi tangu alipoanza kupata ufahamu kuhusu Dunia hii. Na kwa jinsi hiyo Binadamu huyu amejikuta akikutana na usaliti na utumwa wa namna zote katika akili na hali ya maisha. Waliofanikiwa katika utumwa walishindwa katika uaminifu, vivyo waliofanikiwa katika uaminifu waliushinda utumwa.

Afrika ni bara ambalo watu wake wamepitia historia ya kutisha na kuhuzunisha kwa karne nyingi, hata kabla ya kugawanywa kwake. Inasemekana biashara ya utumwa ndani ya Afrika ilianza katika karne ya 14 huko nyuma. Ni kwa sababu gani hasa..? Ukweli wa historia ya mwafrika kuingia utumwa ni kukosekana kwa uaminifu kwa baadhi ya viongozi wa makabila makubwa, ndio kusema historia ya mwafrika imegubikwa na usaliti. Kundi moja kujiona ni bora zaidi kuliko wenzao, kwamba ni wao pekee wanastahili lakini sio wengine. Hivyo kupelekea kusalitiana. Utashangaa Makaburu kuweza kuitawala Afrika kusini baada ya miaka 100 tu tangu kuingia kwake miaka ya 1400's. Ambapo wakaburu wa kwanza kukanyaga ardhi ya Mzee Madiba Mandela inakadiriwa idadi ya wazee wastaafu wasiozidi 200! Lakini ndio hao waliweza kuwatawala zaidi ya waafrika 100k ya wazawa.

Hivyo kwa sababu ya usaliti, Afrika tulitawaliwa. Lakini kwa kuwa Binadamu ameendelea kutafuta amani na utulivu ni dhahiri kuwa ilitakiwa Uhuru uwepo kwa waafrika ili mwafrika aweze kupata amani na utulivu. Na kwa jinsi hiyo ni katika karne ya 19, waafrika walianza kujitafutia Uhuru wao na kwa kweli ilitakiwa kujenga umoja na kujengeana hali ya kuaminiana kwanza ili kufanikisha kuikomboa Afrika. Hivyo basi, umoja wa waafrika na uongozi wenye uaminifu uliwezesha Afrika kujikomboa na watu wake kuwa huru. Na sasa waafrika wanawajibika na ujenzi wa uchumi wa nchi zao.

Leo Tanzania kama sehemu ya Afrika inatudai uaminifu wetu sisi waafrika watanzania katika kuhakikisha tunayaendeleza yale ambayo Afrika iliyahitaji kwa muda mrefu hata kuweza kujikomboa. Nao ni umoja wa waafrika, ndio kusema kuwa Tanzania, inatudai umoja wetu sisi watanzania.

Sasa tutawezaje kuilipa Tanzania? Kipindi tunaelekea uchaguzi mkuu, wajibu wetu ni kupiga kura kwenda kumchagua kiongozi ambaye atakuwa na misuli imara isiyotetereka katika kuwaunganisha watu pasi na kuwagawa katika misingi ya udini, ukabila wala hali zao kiuchumi. Kiongozi ambaye wajibu wake ni kwa Tanzania na Afrika, kiongozi ambaye kipaumbele chake ni kuendeleza na kukuza siasa zenye kufuata tamaduni za mwafrika na Afrika. Tukachague chama ambacho kinaamini katika ujamaa na kujitegemea kwamba usawa ndani ya jamii ndio msingi wa haki sawa kwa wananchi wote na hivyo huzaa matunda ya amani na utulivu na uaminifu baina ya Watanzania.

Siasa haiwezi kujitenga na Tanzania, na watanzania hawawezi kujitenga na siasa. Hivyo wajibu wetu ni kuwapima wanasiasa na kutambua ni wanasiasa gani wenye malengo ya kudumisha umoja, amani na utulivu wa Afrika! Kushindwa kutambua jambo hilo, ni kuiweka nchi katika hatari ya kurudi kule ilipotoka. Hivyo basi siasa haijaribiwa bali hutekelezwa kwa umakini na uangalifu mkubwa. Kwa miaka mitano sasa, wapo wanasiasa ambao kwa haiba zao, uwezo wao wa misuli, uzalendo wao kwa nchi umefunuliwa kwetu.

Tarehe 28/10/2020 siku ya jumatano, ni siku ambayo inaenda kutoa uelekeo wa Tanzania kwa miaka mitano na zaidi mbeleni. Ewe Mtanzania napenda nikukumbushe kuwa hakuna dalali ambaye aliwahi kumuacha salama mwenye mali. Yeye anasukumwa na faida zake binafsi na sio za mwenye mali. Dalali yeyote atakayeweza kuingia ikulu pale, ni hakika yangu watanzania hawatakuwa salama, Tanzania ni ya watanzania. Chagua mtanzania mzalendo mwenye kuiona Tanzania katika mioyo ya watanzania, na sio mwenye kuiona Tanzania katika mikataba ya madini iliyopo tu. Hiyo ni ishara ya udalali wa wazi kabisa. Amka asubuhi kisha fanya uamuzi wa kwenda kumchagua Rais wa nchi mzalendo na mwenye maamuzi magumu na mwenye kuamini katika misimamo yenye tija kwa ajili ya watanzania, hana msukumo wa uoga bali ni ukweli wa kitafiti, fahari ya Tanzania, kiongozi mfano wa kuigwa na Marais wa mataifa hata ya Ulaya na Asia, si mwingine ni Dkt. JOHN POMBE MAGUFULI. Leo hii mataifa wanashangaa ni jinsi gani ajabu alivyoweza kidhibiti covid-19 bila lockdown?! Walipogundua kuwa ni maombi, sasa na wao wanaitisha maombi ndani ya nchi zao.

#chaguaMagufuli2020
#chaguaCCM2020
#Magufuli5Tena

Sauti ya Mdodomia
20/10/2020.

Makala ndefu, bila haki?
 
Sina muda wa kupoteza kwa watu wanaoacha weledi nyuma, wanaamua kuongozwa na ushabiki, uwongo, na siasa za hila na hadaa.

Kwa vile Watanzania wana akili, wana macho, na ni mashuhuda wa yale yanayowazunguka, nina hakika wengi watamchagua mgombea ambaye atawatoa kwenye minyororo ya utumwa na ukoloni mpya unaofanywa na watanzania wenzao dhidi yao.

Mimi nitamchagua mtu ambaye atalinda haki ya kila mmoja, uhuru wa kila mmoja, na ataiishi falsafa ya mwasisi wa Taifa letu kuwa maendeleo ya kweli ni maendeleo ya watu. Na jweli hili, najua sipo pekee yangu bali ni mamilioni ya Watanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
Iliuweze kuyapata yote hayo, Basi amka asubuhi na mapema siku hiyo ikifika. Nenda kamchague Rais John Pombe Magufuli. Yeye atayafanya yote hayo katika uongozi wake.

#chaguamagufuli2020
 
Acheni upuuzi wenu,Tanzania ya leo wananchi wanajitambua!Hizo propaganda zenu za hovyo kaeni nazo lumumba!
Usikariri. Si kila anayeeleza mazuri ya Mh.Rais anatoka Lumumba! Ni tahadhari tu mfumbue macho au angalia kwa jicho la tatu ni kiongozi yupi atakayefaa. Uamuzi unaoongozwa na hasira au chuki mara nyingi haukupeleki kwema.Hivi hamjiulizi imekuwaje mabeberu wamekuwa na interest kubwa na uchaguzi huu?

Wao wanakufa na covid-19 sisi tunadunda! Wanafikiri "hiki kiinchi kina nini? Halafu wanashangaa "mbona hawa wanafanya haya mambo makubwa ya miundo mbinu? wanataka kufanana na sisi?". "Tuwazime vipi? Au tufanyeje waharibikiwe?". Wanapitia huko kwenye "demokrasia " na ni tahadhari tu kutokufuata upepo na kufikiri ukiongozwa na kuomba maongozi ya Mungu.

Nakumbuka taifa lilisali sana 2015 na tukapewa JPM. Hajamaliza kazi na huyu mwingine anapinga au kukosoa alichofanya. Hatutafika kama tutaongozwa na hasira au chuki au dhamira mbaya.
 
Usikariri. Si kila anayeeleza mazuri ya Mh.Rais anatoka Lumumba! Ni tahadhari tu mfumbue macho au angalia kwa jicho la tatu ni kiongozi yupi atakayefaa. Uamuzi unaoongozwa na hasira au chuki mara nyingi haukupeleki kwema.Hivi hamjiulizi imekuwaje mabeberu wamekuwa na interest kubwa na uchaguzi huu? Wao wanakufa na covid-19 sisi tunadunda! Wanafikiri "hiki kiinchi kina nini? Halafu wanashangaa "mbona hawa wanafanya haya mambo makubwa ya miundo mbinu? wanataka kufanana na sisi?". "Tuwazime vipi? Au tufanyeje waharibikiwe?". Wanapitia huko kwenye "demokrasia " na ni tahadhari tu kutokufuata upepo na kufikiri ukiongozwa na kuomba maongozi ya Mungu. Nakumbuka taifa lilisali sana 2015 na tukapewa JPM. Hajamaliza kazi na huyu mwingine anapinga au kukosoa alichofanya. Hatutafika kama tutaongozwa na hasira au chuki au dhamira mbaya.
Kwa miundombinu hata Robo kwa Kenya hatuingii!Eti USA inatuonea wivu?Mna akili timamu kweli?Hizi kweli ni propaganda za kumwambia mtu anayejitambua?

Kama ni Corona basi nchi nyingi tu Africa zimesurvive,mfano ni burundi!Wakati sisi tumefunga shule na kuzuia mikusanyiko,wao walikuwa wanafanya kampeni!

So hakuna kitu special kwa Tanzania kama mnavyoaminisha watu!!!!
 
Kwa miundombinu hata Robo kwa Kenya hatuingii!Eti USA inatuonea wivu?Mna akili timamu kweli?Hizi kweli ni propaganda za kumwambia mtu anayejitambua?Kama ni Corona basi nchi nyingi tu Africa zimesurvive,mfano ni burundi!Wakati sisi tumefunga shule na kuzuia mikusanyiko,wao walikuwa wanafanya kampeni!
So hakuna kitu special kwa Tanzania kama mnavyoaminisha watu!!!!
Ndiyo tumeanza sasa kwa kasi mpya. Angalia uwajibikaji ofisi za umma kipindi hiki! Angalia amani na utulivu na ufuataji wa sheria sasa hivi. Angalia matumizi ya kodi walau tunaona na kusikia pesa zinafanya kazi sehemu na sehemu.

Hatuwezi kulingana na kenya pengine baada ya miaka kama si miongo kadhaa mbele. Lakini kwa wenzetu ufisadi uko juu, angalia pesa zao za covid zina maneno gani. Tujivunie hatua tuliyopiga hata kama unaona ni ndogo lakini siyo ndogo.

Pengine wengine wangefurahia kusikia habari za ufisadi ambazo hazipo sasa.
 
Ndiyo tumeanza sasa kwa kasi mpya. Angalia uwajibikaji ofisi za umma kipindi hiki! Angalia amani na utulivu na ufuataji wa sheria sasa hivi. Angalia matumizi ya kodi walau tunaona na kusikia pesa zinafanya kazi sehemu na sehemu. Hatuwezi kulingana na kenya pengine baada ya miaka kama si miongo kadhaa mbele. Lakini kwa wenzetu ufisadi uko juu, angalia pesa zao za covid zina maneno gani. Tujivunie hatua tuliyopiga hata kama unaona ni ndogo lakini siyo ndogo. Pengine wengine wangefurahia kusikia habari za ufisadi ambazo hazipo sasa.
Sasa mbona hao USA ndio huwa wanahimiza uwazi na uwajibikaji wa serikali!Hata pesa wanazotoa kama misaada huwa wanafuatilia kama zimetumika kama walivyokusudia!Huwa wanasisitiza vita dhidi ya rushwa na madawa ya kukevya!Ila shida inakuja wanaposisitiza juu ya uhuru,haki na demokrasia!Hapo ndio huwa mnawaona wabaya!Mnaanza maneno ya kanga kuwa wanatuonea wivu,what a shame!!!
 
"Mnaanza maneno ya kanga kuwa wanatuonea wivu,what a shame!!!"
Unaweza ukawa na kitu cha thamani sana sana halafu kumbe wewe hujui kwa sababu ya mazoea unaona ni cha kawaida. Thamani yake utaiona kitakapokuwa hakipo. Ndiyo ubinadamu wetu ulivyo. Muda utatoa fundisho.
 
Back
Top Bottom