Watanzania tuwe wamoja katika kipindi hiki kigumu

Naona nchi hii sasa imegawanyika vibaya mno kisa siasa.

Nachotaka kusema hapa uchaguzi umepita na ulikuwa na machungu mengi maumivu mengi kisa tu chama fulani wabaki madarakani, yote na yote tumeyaona.

Ila naomba tusameheane tuendelee kuijenga nchi yetu maana kwa sasa naona kwa hatua tuliofikia ni rahisi sana maadui kuipiga Tanzania maana mikoa yote ya mipakani imevurugwa na huu uchaguzi watu wana vidonda moyoni.

Ila tukumbuke Tanzania ni yetu wote sisi masikini hatuna uwezo hata wa kukimbilia nchi nyingine na ndio tulio wengi chonde chonde tuipende nchi yetu yaliyo tokea tuyasamehe tu na maisha yaendelee siasa zisitufanye tuchukiane.

Naona watu wanashangilia Bunge la Ulaya kupendekeza misaada kukatwa nchini naomba niseme tusifurahie haya mambo yatakuwa magumu sana.

Tuipende nchi yetu kwa vizazi vyetu
INAELEKEA WEWE NI MMOJA WAO WA WALE WALIO NUFAIKA NA UCHAGUZI , UMEPATA NAFASI YA UONGOZI , HUNA NDUGU AMBAYE AMEPIGWA RISASI AU KUUAWA. UCHAGUZI HUU UMEICHAFUA TANZANIA NDANI NA NJE YA NCHI . KITUGANI KITATUFANYA TUWE WAMOJA
 
Back
Top Bottom