Watanzania tuwe na desturi ya kuwekeza katika hisa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania tuwe na desturi ya kuwekeza katika hisa

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by mseseve, Oct 6, 2011.

 1. mseseve

  mseseve JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2011
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 518
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  HAYA KWA MARA NYINGiNE TENA JAMAA WA KAMPUNI YA KIZAWA(KITANZANIA) PRECISION AIR you are why we fly ,IMETANGAZA MPANGO WA KUANZA KUUZA HISA ZAKE KWENYE SOKO LA HISA DSE ILI KUWAPA FURSA WATZ WAWEZE KUNUNUA HISA ZA KAMPUNI HIYO NA KUWA MMOJA KATI YA WAMILIKI WA KAMPUNI HIYO YA KITANZANIA INAYOJISHUGHULISHA NA SHUGHULI ZA USAFIRISHAJI ABIRIA NA MIZIGO(PARCELS) KWA NJIA YA ANGA.AKITANGAZA MPANGO HUO MWENYEKITI NA MWANZILISHI WA KAMPUNI HIYO BWANA MICHAEL SHIRIMA, ALISEMA MPANGO HUO UTAWALENGA WATANZANIA WOTE WA KIPATO CHA CHINI NA CHA JUU.

  HOFU YANGU NI JUU YA MWITIKIO WA WATANZANIA JUU YA MASWALA MAZIMA YA UNUNUZI WA HISA KAMA TUJUAVYO WATANZANIA WALIO WENGIWASOMI NA WASIO WASOMI HAWANA UELEWA JUU YA MASWLA YA HISA, HIVYO NI VIZURI KWA MAMLAKA ZINAZOHUSIKA KUTOA ELIMU JUU YA HILO.DHUMUNI LANGU NI KUONA WATANZANIA WENGI TUNAINGIA KWENYE MFUMO WA KISASA NA USHINDANI WA KIBIASHARA ILI TUWEZE KWENDA SAMBAMBA NA MABADILIKO YA KITEKNOLOJI NA MAGEUZI YA USHIRIKIANO WA KIBIASHARA KATI YETU NA WENZETU WA AFRIKA MASHARIKI.TUSIWE TUNALALAMIKA KILA SIKU TUMEZIDIWA ILI HALI NI SISI WENYEWE HATUJISHUGHULISHI.
   
 2. Mzani

  Mzani Member

  #2
  Oct 6, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 80
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu Mseseve
  Mimi ni mdau na napenda sana kuwekeza katika hisa, Tukizungumzia hisa hizi za kampuni hii inayojishughurisha na usafiri wa anga ambazo zitaanza kuunzwa kwa mara ya kwanza kesho ijumaa, kwa kiasi cha Tsh. 475 kwa hisa moja, na kiwango cha chini cha kununua ni hisa 200.

  Changamoto ninayoiona mimi ni upatikanaji wa taarifa za fedha na taarifa nyingine muhimu zitakazo weza kufanya uchambuzi wa kujua uwezo wa kampuni na mengineyo ambayo ni ya msingi.

  Wapi zinapatikana hizo taarifa?

  Nimeangalia kwenyetovuti ya precission sijapata chochote kuhusu mchanganuo wa taarifa ya fedha angalau ya miaka miwili iliyopita,
  na walisema kwamba prospectus ingepatikana kwenye tovuti kuanzia 4/10/2011 lakini mimi sijaiona.

  Yawezekana kuna taarifa ambazo zilishatolewa kwa jumuia bila mimi kufahamu, nitumiie nafasi hii kuomba uwezekano wa kupata hizo taarifa
  vinginevyo sitaweza kununua hisa ambazo sijua taarifa zake. Naamini hata wewe unafanya utafiti kwanza ndipo unawekeza, kwa kuzingatia taarifa na zinginezo za msingi
   
Loading...