Uchaguzi 2020 Watanzania tuwe makini: Viongozi wengi hupenda kugawa "vitu" badala ya "akili" ya kuvipata vitu hivyo

Kididimo

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
3,791
3,360
Ni aibu karne ya leo kupokea baiskeli, chumvi, T-shirt kama kichocheo cha kutoa kura yako.

Tumesikia Wabunge kadhaa tena wa Chama chetu Tawala wakishikiliwa na Takukuru kisa ni kutoa rushwa.

Ni aibu vilevile Kiongozi kujinadi kuwa amejenga barabara za vijijini hivyo tumpe Kura.

Je, niwaulize wapiga kura wenzangu, unapopewa baiskeli na Mbunge kwa nini usijiulize kuwa yeye kavipataje? Katumia mbinu gani kupata uwezo wa kununua hiyo baiskeli anayokuhonga?

Kama alilima akafanikiwa, ni nini kinamuwia ugumu kukupa huo utaalamu wa Kilimo ili nawe unufaike zaidi ya hako ka phonix?

Ukienda kwenye Suala mfano la barabara au maji ni vivyo hivyo. Siamini kama Wanakijiji wenye uwezo mzuri wa kiuchumi watashindwa kuchimba visima vya maji au kujenga barabara zao nk.
 
Back
Top Bottom