Watanzania tuwe makini tunapojadili mustakabali wa Taifa letu, tusiruhusu hisia mbaya zitutawale

In Summary iko hivi:

Mawaziri wanawake 4 sawa na 17%, Wanaume 83% ( a good lesson to Ndugai's rants about Chadema gender biasness)......

Waislam ni 3 sawa na 13%, Wengine 87% (na assume waliobaki wote ni Wakristu)

Zaidi ya 50% wanatoka kanda ya ziwa

Hii ni just highlight ya hali ya Baraza ilivyo na wala siyo watu wanalisema vibaya maana hamna cha uongo wanachokisema. Labda kama haupendi Maths & Statistics

Sisi tunaliombea badaza li-delivery kadri ya matamanio ya mteuaji na chama tawala
Mkuu mambo ya takwimu na hesabu yamekatazwa
 
Wewe changu acha kelele. Wahi ikulu kabla makombo hayajatolewa mezani pa bwana wako. Lunch time ndiyo inaishia.
 
Nyinyi wajinga was kipenyo msituletee hoja za hovyo humu. Mna andika mareeeefu ambayo ni uharo tu. Akili zenu zimeishia kwenye siasa tu usalama, uchumi etc zero. Hakuna legitimacy kwenye uteuzi wa mawaziri period.
Hujanielewa na huta nielewa mana unawaza kwa mrengo mmoja tu wa uteuzi wa kidini.

Hivi kama pangekua na Sheria Kali inayosimamia Katiba yetu ya kijamaa na maadili ya uongozi nani angelimbilia hizo teuzi eti kabila au dini!!

Hebu jiulize mtu anateuliwa kuwa waziri baada ya miaka miwili anaona aibu kutangaza Mali zake mana hazina idadi.

MTU anakua Rais baada ya miaka kumi hakuna tume inayohoji Mali zake.

Anaingia kwenye uteuzi au uchaguzi hakuna anayehoji Mali zake.
Anatumbuliwa kwa wizi hakuna anayehoji Mali zake.
Wewe unaona hiyo in sawa kwa sababu tu ametoa wazo mtu asiyesifia Dini au chama au kabila.
Mana Mimi sijaongelea kabila wala Dini ya mtu kama sifa.

Ila ni vyema tuondoe yale yanayosababisha watu wanapendeleana kidini au kikabila.
Sijakata kuwa hakuna udini au ukabila. Nilichozungumzia ni visabishi na vinavyolea hayo mambo ambayo ni kimyume kabisa na Katiba.

Na nakuhakikishia kuwa tusipowafunga Brake watawala kwa kuboresha zaidi Katiba na kuweka madili na kupunguza madaraka ya mtu mmoja kuna siku inchi hii itatawaliwa kidini kabisa kabisa kabisa na dalili ya mvua ni mawingu.

Mimi hua napenda kushauri zaidi ndio maana situkani mtu kama nyie wengine Mnaodhani nguvu ya hoja ni matusi na kejeli. Matokeo yake hakuna mwenye akili anayetishwa na matusi zaidi ya kumtafuta mtukanaji na kumfumua fumua tu. Tena uchaguzi umeisha na baraza tayari hatutaki matusi tena tunataka hoja za mana na ushauri wenye kufikirisha au kuwa kwa pembeni lakini sio matusi ambayo hayajenge chochote zaidi ya kutengeneza makosa ya kimtandao.

Sio jambo la kiungwana kulaumu tuu wakati unajua wazi kuwa madaraka ndiyo yanayotoa mwanya huo na hakuna wa kuhoji zaidi ya kupiga tu kelele bila jukumu La kisheria.
Angefanya hivyo wa upande mwingine wa Dini bila shaka matamko yangekua ni mengi na nyaraka nyingi . Je, huoni kuwa mfumo ndio unaotoa mwanya wa watu kupendeleana na kupeana ulaji!?

Hivi huoni kuwa akitokea mtu mkaidi na kuamua kuiendesha nchi kwa misingi ya kabila au Dini yake anaweza kabisa kutokana na umaskini na madaraka makubwa anayokua nayo mtu ya kuamua nani ale na kusaza na nani akalie gerezani ?
Hivi mtu akaamua kuwaweka watu wa upande wake tuu kwenye idara zote na wakatumia madaraka yao kuwatisha wengine si atafanikiwa !!
Nani atahiji wakati anayehoji naye kapewa nafasi ili ale aondoe umaskini.

Kwa mfano wabunge wa sasa na madiwani asilimia kubwa wamepata nafasi kwa sababu zisizo rasmi na wengine wamepata uwaziri na unaibu na wengine wameteuliwa. Kwa hali ya kawaida na fursa za madaraka zilizopo wanaona wazi kuwa maisha yao yanaelekea kuwa bora sana . Je, wataweza kuhoji jambo lolote kinyume cha Katiba.?
Wanasema mtu akila asiwe anaongea ndio mila za kiafrika.

Katiba yetu haijataja sifa za Mawaziri kuwa zitapatikana kutoka kwenye Imani za dini. Sasa utatumia kigezo gani kulalamika kama sio kulalamika kwa sababu ya kutafuta msosi tu mana hakuna kingine. Kama tungesema kuwa Cheo ni dhamana nadhani kila mtu angeogopa madaraka.

Mimi binafsi hua sionagi shida kuona watu wa dini nyingine kuongoza. Shida yangu ni kile kinachopelekea watu kukimbilia madaraka.
Mtu akipata uwaziri basi hafuati tena sheria za ajira anajaza watu wa familia yake kila mahali penye fursa za kipato. Na haya ndiyo wanayoyapigania kwa migongo ya dini ,vyama ,ukabila ,urafiki ,undugu na kila aina ya upendeleo.
Angefungwa waziri au mstaafu mmoja mkubwa aliyetumia madaraka yake vibaya nadhani kila mmoja angejipima kabla ya kutamani mtu wa dini yake awe kiongozi.
 
Umeandika insha ndefu, kumbe wewe ni Lumumba fc!
Linapokuja suala la kufyeka maslahi hua CCM na wapinzani wanaungana kupinga mana wote ni wanasiasa wanaotumia siasa kama biashara.

Maslahi yanaweza yakamfanya mtu akawaza madaraka tu.

Ndio maana Afrika hatuwezi kuungana na kuwa nchi moja kubwa yenye nguvu ya kiuchumi kwa sababu kila mtu anawaza kuwa nani atakua rais na atatoka wapi ,ukanda upi, dini gani na kila aina ya sifa za ajabu ajabu.

Kama mtu amejitoa kweli kwa ajili ya watu nadhani suala la dini hailina tija sana.
Lakini kama ni kupeana ulaji basi nadhani kila mtu anahitaji mtu wake au yeye mwenyewe kupata mana njaa haina baunsa.

Piganieni Katiba bora kabisa inayowabana sana watawala wawapo mdarakani na wanapotoka madarakani na teuzi zao zibanwe ili wakiingia waweke wazi mali zao na walivyozipata.
Wakitoka wahojiwe tana juu ya Mali zao. Mishahara yao tuwape kulingana na uchumi wetu na uwiane na watu wengine wanaotumikia taifa hili kwa uzalendo na wao wana familia pia. Lakini pia kuna ambao hawana fungu lolote kwenye utajiri ulioumbwa na Mungu kwenye mataifa haya ya Kiafrika nao piwa wanafaidika vipi mana hata maji wananunua bado tu kulipia mvua na Jua.

Sijaona Chama chenye mfumo mbadala zaidi ya kutamani kuingia ili nao wale na kujiwekea kinga ya kutoshitakiwa na kufungwa gerezani na hata kufilisiwa na kunyongwa kwa makosa wanayofanya.

Kuna mengine mwenyekiti tu anaogopwa kuliko mungu na hahojiwi wala kukosolewa zaidi ya kupigiwa magoti ndani ya vyama .
 
Nani awe careful????! Ni kuku ama yai??!???
Nani anatakiwa awe makini zaidi???
Ni kiongozi ama ni aliyeonewa???
Please use your brains to think!!!
 
Back
Top Bottom