Watanzania tuwe makini na vyombo vya habari vya Kibeberu. CNN wazusha kukamatwa kwa Freeman Mbowe ni amri ya Rais Samia!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,337
113,178
Wanabodi,

Wiki iliyopita nilialikwa TBC kwenye kipindi cha Mizani, kinachoendeshwa na Dr. Ayoub Rioba. Mada kwenye kipindi hicho ni "Dhima ya Vyombo vya Habari Kulinda Maslahi ya Taifa".

Kwenye mjadala kuliibuka hoja jinsi Vyombo vya habari vya nje vinavyoibagaza Africa katika ripoti zake. Kwao kuibagaza Africa ndio maslahi kwao kwa mataifa yao.

Juzi Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Freeman Mbowe amekatwa na Polisi na tuhuma za kijinai.

CNN wameripoti hivi:

Katika ripoti hiyo, kwanza CNN, hawakutafuta any authoritative source Kutoka nchini Tanzania, zaidi ya kuokoteza habari hiyo kama ilivyoripotiwa na media mbalimbali za ndani.

Kwa vile CNN ni chombo cha kibeberu, hivyo kina agenda ya kubagaza, CNN wakamtafuta Prof. Nic Cheeseman, ni Professor wa Democracy, University of Birmingham, kabla ya hapo, alikuwa Director wa African Studies Centre at Oxford University, ili kuichambua habari hiyo.

Prof. Huyo akatunga uongo wa wazi wa mchana kweupe kuwa Freeman Mbowe, amekamatwa kwa amri ya rais Samia ili ku divert attention ya vuguvugu la katiba na tozo kwenye miamala ya simu!.

Huu sio uongo wa mchana kweupe?. Yaani hata kwa akili ya kawaida tuu, yaani Rais wetu Samia atoe amri ya Kukamatwa kwa Mbowe, kisa ni vuguvugu la mjadala wa katiba mpya na tozo za miamala?!, Watanzania tusijue, aliyemkamata Mbowe, amezungumza na sababu ametoa, CNN badala ya kutafuta the reliable sources, wanatuletea wazushi na kutuletea uzushi!. Ukisikia Ajenda hasi ndio hizi!.

Kwa vile hii ni lugha ya watu, na pia naufahamu uwezo wa wengi wetu kwenye uelewa hizi lugha za watu, hivyo ili kuwasaidia wale wenzangu na mimi, sikiliza kwa makini jibu la swali la pili.
"it is a crackdown, she has launched or pretended to launch all along"

Watanzania Wazalendo lazima tuwe makini sana na Vyombo hivi, unaweza kujikuta unasambaza taarifa ya kuibagaza nchi yako, rais wako na watu wako bila kujijua.

Kipindi chote cha Mtangulizi, hizi media za nje zimekuwa zikituzushia mambo mengi tuu ya uongo na uzushi na serikali yetu imekuwa ikinyamaza bila kujibu, matokeo yake ni dunia kuaminishwa uongo, hivyo nashauri serikali yetu, awamu hii, tusinyamazie uongo na uzushi, tujibu mapigo tena kwenye vyombo vyao hivyo hivyo vya kimataifa. Tanzania tuna BBC, Reuters, DW, VOA, Blumberg, SABC, RFI, la Xhinua, tuwaite tuwaeleze ukweli, dawa ya uongo ni kuusema ukweli. Uongo ukisemwa na kuachwa kurudiwa rudiwa bila kukanushwa, sio tuu utaonekana kama ndio ukweli, bali sometimes hugeuka ukweli kabisa na kuja kutokea kwa sababu kauli nyingine huumba, kama uongo huu
Huu ulikuwa ni uongo tuu na uzushi, tukaunyamazia, ukaja kutokea kweli.

Tanzania ya Samia, tusinyamazie uongo na uzushi, wakizusha tuwaite tuwaeleze ukweli.

Uzalendo wa kweli ni kutanguliza mbele maslahi ya nchi yako, maslahi ya taifa lako, maslahi ya watu wako.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
Rejea za Mwandishi kuhusu media za Mabeberu.

Mimi naungana na hao CNN! Maana walicho lieleza kina ukweli! Kwa sababu wakati yuko kwenye ziara Morogoro, aliongelea suala hilo na kusema wanaodai Katiba Mpya wanatafuta chokochoko!

Kwa maneno hayo tu machache ni kwa nini nisiamini huyu mama ana mkono wake! Ila siyo fair! Yaani kutaka kuendesha kongamano la katiba ndiyo uonekane gaidi!

Hivi Magaidi mnawafahamu kweli nyinyi ndugu zetu wa ccm!
 
Badala uwaase wajinga wenzako huko ccm wajifunze kujibu hoja kwa hoja unakimbilia kutuhumu vyombo vya habari vinavyopigania haki na demokrasia.

Hivi ni lini hiyo njaa ya madaraka itakuisha? Lizee lizima unajidhalilisha alafu unaona kawaida tu 😏
 
Wanabodi,

Wiki iliyopita nilialikwa TBC kwenye kipindi cha Mizani, kinachoendeshwa na Dr. Ayoub Rioba. Mada kwenye kipindi hicho ni "Dhima ya Vyombo vya Habari Kulinda Maslahi ya Taifa".

Kwenye mjadala kuliibuka hoja jinsi Vyombo vya habari vya nje vinavyoibagaza Africa katika ripoti zake. Kwao kuibagaza Africa ndio maslahi kwao kwa mataifa yao.

Juzi Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Freeman Mbowe amekatwa na Polisi na tuhuma za kijinai.

CNN wameripoti hivi

Katika ripoti hiyo, kwanza CNN, hawakutafuta any authoritative source Kutoka nchini Tanzania, zaidi ya kuokoteza habari hiyo kama ilivyoripotiwa na media mbalimbali za ndani.

Kwa vile CNN ni chombo cha kibeberu, hivyo kina agenda ya kubagaza, CNN wakamtafuta Prof. wa Chuo Kikuu cha Uingereza ili kuichambua habari hiyo.

Prof. Huyo akatunga uongo wa wazi wa mchana kweupe kuwa Freeman Mbowe, amekamatwa kwa amri ya rais Samia ili ku divert attention ya vuguvugu la katiba na tozo kwenye miamala ya simu!.

Huu sio uongo wa mchana kweupe?. Yaani hata kwa akili ya kawaida tuu, yaani Rais wetu Samia atoe amri ya Kukamatwa kwa Mbowe, kisa ni vuguvugu la mjadala wa katiba mpya na tozo za miamala?!, Watanzania tusijue, aliyemkamata Mbowe, amezungumza na sababu ametoa, CNN badala ya kutafuta the reliable sources, wanatuletea wazushi na kutuletea uzushi!. Ukisikia Ajenda hasi ndio hizi!.

Watanzania Wazalendo lazima tuwe makini sana na Vyombo hivi, unaweza kujikuta unasambaza taarifa ya kuibaza nchi yako, rais wako na watu wako bila kujijua.

Uzalendo wa kweli ni kutanguliza mbele maslahi ya nchi yako, maslahi ya taifa lako, maslahi ya watu wako.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
Acha uongo wewe si ndiye ulimletea Kabendera shida kwa unafiki wako? Hakuna pahala yule professor amemu “implicate” rais Samia directly! Lakini anazifahamu siasa za Tanzania vyema kabisa. Kwani si kawaida kusikia ni “amri toka juu”?
 
Wanabodi,

Wiki iliyopita nilialikwa TBC kwenye kipindi cha Mizani, kinachoendeshwa na Dr. Ayoub Rioba. Mada kwenye kipindi hicho ni "Dhima ya Vyombo vya Habari Kulinda Maslahi ya Taifa".

Kwenye mjadala kuliibuka hoja jinsi Vyombo vya habari vya nje vinavyoibagaza Africa katika ripoti zake. Kwao kuibagaza Africa ndio maslahi kwao kwa mataifa yao.

Juzi Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Freeman Mbowe amekatwa na Polisi na tuhuma za kijinai.

CNN wameripoti hivi

Katika ripoti hiyo, kwanza CNN, hawakutafuta any authoritative source Kutoka nchini Tanzania, zaidi ya kuokoteza habari hiyo kama ilivyoripotiwa na media mbalimbali za ndani.

Kwa vile CNN ni chombo cha kibeberu, hivyo kina agenda ya kubagaza, CNN wakamtafuta Prof. wa Chuo Kikuu cha Uingereza ili kuichambua habari hiyo.

Prof. Huyo akatunga uongo wa wazi wa mchana kweupe kuwa Freeman Mbowe, amekamatwa kwa amri ya rais Samia ili ku divert attention ya vuguvugu la katiba na tozo kwenye miamala ya simu!.

Huu sio uongo wa mchana kweupe?. Yaani hata kwa akili ya kawaida tuu, yaani Rais wetu Samia atoe amri ya Kukamatwa kwa Mbowe, kisa ni vuguvugu la mjadala wa katiba mpya na tozo za miamala?!, Watanzania tusijue, aliyemkamata Mbowe, amezungumza na sababu ametoa, CNN badala ya kutafuta the reliable sources, wanatuletea wazushi na kutuletea uzushi!. Ukisikia Ajenda hasi ndio hizi!.

Watanzania Wazalendo lazima tuwe makini sana na Vyombo hivi, unaweza kujikuta unasambaza taarifa ya kuibaza nchi yako, rais wako na watu wako bila kujijua.

Uzalendo wa kweli ni kutanguliza mbele maslahi ya nchi yako, maslahi ya taifa lako, maslahi ya watu wako.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
Tangu Trump aondoke CNN wamekosa wakumtuhumu na kujipatia watazamaji Sasa wamehamia Africa

USSR
 
Badala uwaase wajinga wenzako huko ccm wajifunze kujibu hoja kwa hoja unakimbilia kutuhumu vyombo vya habari vinavyopigania haki na demokrasia.

Hivi ni lini hiyo njaa ya madaraka itakuisha? Lizee lizima unajidhalilisha alafu unaona kawaida tu
Gaidi mbowe analiwa na papasi gerezani kwa kupanga kuuwa viongozi wa kitaifa wewe unaleta siasa

USSR
 
Wanabodi,

Wiki iliyopita nilialikwa TBC kwenye kipindi cha Mizani, kinachoendeshwa na Dr. Ayoub Rioba. Mada kwenye kipindi hicho ni "Dhima ya Vyombo vya Habari Kulinda Maslahi ya Taifa".

Kwenye mjadala kuliibuka hoja jinsi Vyombo vya habari vya nje vinavyoibagaza Africa katika ripoti zake. Kwao kuibagaza Africa ndio maslahi kwao kwa mataifa yao.

Juzi Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Freeman Mbowe amekatwa na Polisi na tuhuma za kijinai.

CNN wameripoti hivi

Katika ripoti hiyo, kwanza CNN, hawakutafuta any authoritative source Kutoka nchini Tanzania, zaidi ya kuokoteza habari hiyo kama ilivyoripotiwa na media mbalimbali za ndani.

Kwa vile CNN ni chombo cha kibeberu, hivyo kina agenda ya kubagaza, CNN wakamtafuta Prof. wa Chuo Kikuu cha Uingereza ili kuichambua habari hiyo.

Prof. Huyo akatunga uongo wa wazi wa mchana kweupe kuwa Freeman Mbowe, amekamatwa kwa amri ya rais Samia ili ku divert attention ya vuguvugu la katiba na tozo kwenye miamala ya simu!.

Huu sio uongo wa mchana kweupe?. Yaani hata kwa akili ya kawaida tuu, yaani Rais wetu Samia atoe amri ya Kukamatwa kwa Mbowe, kisa ni vuguvugu la mjadala wa katiba mpya na tozo za miamala?!, Watanzania tusijue, aliyemkamata Mbowe, amezungumza na sababu ametoa, CNN badala ya kutafuta the reliable sources, wanatuletea wazushi na kutuletea uzushi!. Ukisikia Ajenda hasi ndio hizi!.

Watanzania Wazalendo lazima tuwe makini sana na Vyombo hivi, unaweza kujikuta unasambaza taarifa ya kuibaza nchi yako, rais wako na watu wako bila kujijua.

Uzalendo wa kweli ni kutanguliza mbele maslahi ya nchi yako, maslahi ya taifa lako, maslahi ya watu wako.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
Hukati tamaa na usaliti. Mpàka Kabendera kakimbia nchi bado umo tu! Sasa unaandika Nini wakati Western media zinaandika ukweli!
 
46 Reactions
Reply
Back
Top Bottom