Watanzania tuwe makini na vyombo vya habari vya Kibeberu. CNN wazusha kukamatwa kwa Freeman Mbowe ni amri ya Rais Samia!

mafutamingi

JF-Expert Member
Feb 14, 2011
2,652
2,000
Wanabodi,

Wiki iliyopita nilialikwa TBC kwenye kipindi cha Mizani, kinachoendeshwa na Dr. Ayoub Rioba. Mada kwenye kipindi hicho ni "Dhima ya Vyombo vya Habari Kulinda Maslahi ya Taifa".

Kwenye mjadala kuliibuka hoja jinsi Vyombo vya habari vya nje vinavyoibagaza Africa katika ripoti zake. Kwao kuibagaza Africa ndio maslahi kwao kwa mataifa yao.

Juzi Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Freeman Mbowe amekatwa na Polisi na tuhuma za kijinai.

CNN wameripoti hivi:Katika ripoti hiyo, kwanza CNN, hawakutafuta any authoritative source Kutoka nchini Tanzania, zaidi ya kuokoteza habari hiyo kama ilivyoripotiwa na media mbalimbali za ndani.

Kwa vile CNN ni chombo cha kibeberu, hivyo kina agenda ya kubagaza, CNN wakamtafuta Prof. Nic Cheeseman, ni Professor wa Democracy, University of Birmingham, kabla ya hapo, alikuwa Director wa African Studies Centre at Oxford University, ili kuichambua habari hiyo.

Prof. Huyo akatunga uongo wa wazi wa mchana kweupe kuwa Freeman Mbowe, amekamatwa kwa amri ya rais Samia ili ku divert attention ya vuguvugu la katiba na tozo kwenye miamala ya simu!.

Huu sio uongo wa mchana kweupe?. Yaani hata kwa akili ya kawaida tuu, yaani Rais wetu Samia atoe amri ya Kukamatwa kwa Mbowe, kisa ni vuguvugu la mjadala wa katiba mpya na tozo za miamala?!, Watanzania tusijue, aliyemkamata Mbowe, amezungumza na sababu ametoa, CNN badala ya kutafuta the reliable sources, wanatuletea wazushi na kutuletea uzushi!. Ukisikia Ajenda hasi ndio hizi!.

Kwa vile hii ni lugha ya watu, na pia naufahamu uwezo wa wengi wetu kwenye uelewa hizi lugha za watu, hivyo ili kuwasaidia wale wenzangu na mimi, sikiliza kwa makini jibu la swali la pili.
"it is a crackdown, she has launched or pretended to launch all along"

Watanzania Wazalendo lazima tuwe makini sana na Vyombo hivi, unaweza kujikuta unasambaza taarifa ya kuibagaza nchi yako, rais wako na watu wako bila kujijua.

Kipindi chote cha Mtangulizi, hizi media za nje zimekuwa zikituzushia mambo mengi tuu ya uongo na uzushi na serikali yetu imekuwa ikinyamaza bila kujibu, matokeo yake ni dunia kuaminishwa uongo, hivyo nashauri serikali yetu, awamu hii, tusinyamazie uongo na uzushi, tujibu mapigo tena kwenye vyombo vyao hivyo hivyo vya kimataifa. Tanzania tuna BBC, Reuters, DW, VOA, Blumberg, SABC, RFI, la Xhinua, tuwaite tuwaeleze ukweli, dawa ya uongo ni kuusema ukweli. Uongo ukisemwa na kuachwa kurudiwa rudiwa bila kukanushwa, sio tuu utaonekana kama ndio ukweli, bali sometimes hugeuka ukweli kabisa na kuja kutokea kwa sababu kauli nyingine huumba, kama uongo huu
Huu ulikuwa ni uongo tuu na uzushi, tukaunyamazia, ukaja kutokea kweli.

Tanzania ya Samia, tusinyamazie uongo na uzushi, wakizusha tuwaite tuwaeleze ukweli.

Uzalendo wa kweli ni kutanguliza mbele maslahi ya nchi yako, maslahi ya taifa lako, maslahi ya watu wako.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
Rejea za Mwandishi kuhusu media za Mabeberu.

Paskali ukweli ni kwamba Mbowe asingeweza kukamatwa bila approval ya Rais. Utaanzaje kumkamata kiongozi was chama kikuu cha upinzani bila kumjulisha Rais? Na unapomjulisha lazima pia umjulishe sababu za kumkamata. Hapa ndo SSH alipoingia mkenge. Enzi za uhai wake JPM aliepelekwa igizo hili kuhusu kumkamata Mbowe akawatupilia mbali!
 
mweusi asili

JF-Expert Member
Nov 11, 2014
1,564
2,000
Shida ya mijadala ya TBC husani anayoisimamia Ryoba inakosa ile maana ya mjadala kwa sababu huwa ana Chanel hoja zilenge upande anaofikiria unafurahisha either kwake, serikali au chama ndio maana huwa natilia mashaka hata hiyo Phd yake au labda ni tumbocracy.
Maana ya mjadala ni kuwa na hoja zinazopiga kotekote Kama msumeno
kwaiyo tunategemea kuona kila
hoja pande zote.
Mfano kama hicho kipindi chake cha Mzani: Mada Dhima ya vyombo vya habari kulinda maslahi ya taifa. Kwa namna ulivyoandika kama ndivyo ilivyojadiliwa inaonekana kwamba chombo cha habari ili kionekane kinalinda maslahi ya taifa basi ni kuongelea yale mazuri tu na sio upande wa kukosoa au kuonyesha changamoto mbalimbali kitu ambacho sio sawa kwa mlengo wa kihabari ie kuelimisha, kuchambua,kutafiti,kusifia hata kukosoa kwa upande wangu naona ndio kazi ya vyombo vya habari, na viwe huru kutoa habari bila kuingiliwa na bila kuvunja sheria sasa huu utamadumi unaotaka kuimarishwa wa vyombo vya habari kulazimika kuandika habari kwa kuwafurahisha watu flani ni hatari kwa maendeleo endelevu kwa sababu habari zote ni muhimu ziwe za kusifu,kuchunguza,kukosoa au kuchambua mfano kwa iyo kesi ya Mbowe sioni tatizo kwa CNN kuripoti kwa kumtumia huyo Prof wa Oxford aliyesema Mbowe kakamatwa kwa amri ya Raisi japo kiuhalisia inaweza isiwe moja kwa amri ya Raisi lakini kupitia wasaidizi wake aliowateua itaonekana ni amri yake alafu unaposema kupata habari kwa hizo reliable/Authorative sources kwa mazingira yetu haya hususani Tanzania we mwenyewe shahidi mamlaka zetu hawapendi waandishi wa habari hasa habari iwe yeye ukakasi kwao kupata ushirikiano ni mbinde au unaweza usipate kabisa maana yake nini serikali zetu za kiafrika zinashida kuhusu utoaji na upatikanaji wa habari, wao wanataka habari za kusifu,kumpongeza au kuhamasisha kuhusu mambo yenye maslahi kwao.
Nategemea waandishi kama nyinyi ndio mpambane kuleta hiyo mizani ya habari. Tuachane na habari za kusifia tu Kuna changamoto nyingi kwenye nyanja mbalimbali zinahitaji watu kama nyinyi mzichambue,mchunguze na muhabarishe jamii bila ubaguzi(bias) ila sio kwa trend hii ya kuogopa watawala kuwa censored kwa hoja ya kulinda maslahi ya nchi kumbe mnalinda maslahi ya watu flani wachache. Mwanao akiwa huru nyumbani kukwambia suruali imetoboka matakoni ukakubali na ukabadilisha anakua kakuokoa na aibu huko nje kuliko wakakusifia halafu unafika nje ndio unaambiwa unatembea matako wazi.
 
2021mao

Member
Aug 19, 2021
43
125
Mayalla amesahau kipindi cha mwendazake alisema tutawashughulikia huku na wewe spika washughulikie humo ndani. Baada ya muda mfupi nini kilitokea kwa Lisu. Waliofanya vile wako wapi? Kwa nini tusiseme kuna mkono wa Rais? Mambo mengine mbona yapo wazi na wait wenyewe wanajinadi.
 
DaudiAiko

Senior Member
Dec 2, 2012
175
250
Wanabodi,

Wiki iliyopita nilialikwa TBC kwenye kipindi cha Mizani, kinachoendeshwa na Dr. Ayoub Rioba. Mada kwenye kipindi hicho ni "Dhima ya Vyombo vya Habari Kulinda Maslahi ya Taifa".

Kwenye mjadala kuliibuka hoja jinsi Vyombo vya habari vya nje vinavyoibagaza Africa katika ripoti zake. Kwao kuibagaza Africa ndio maslahi kwao kwa mataifa yao.

Juzi Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Freeman Mbowe amekatwa na Polisi na tuhuma za kijinai.

CNN wameripoti hivi:Katika ripoti hiyo, kwanza CNN, hawakutafuta any authoritative source Kutoka nchini Tanzania, zaidi ya kuokoteza habari hiyo kama ilivyoripotiwa na media mbalimbali za ndani.

Kwa vile CNN ni chombo cha kibeberu, hivyo kina agenda ya kubagaza, CNN wakamtafuta Prof. Nic Cheeseman, ni Professor wa Democracy, University of Birmingham, kabla ya hapo, alikuwa Director wa African Studies Centre at Oxford University, ili kuichambua habari hiyo.

Prof. Huyo akatunga uongo wa wazi wa mchana kweupe kuwa Freeman Mbowe, amekamatwa kwa amri ya rais Samia ili ku divert attention ya vuguvugu la katiba na tozo kwenye miamala ya simu!.

Huu sio uongo wa mchana kweupe?. Yaani hata kwa akili ya kawaida tuu, yaani Rais wetu Samia atoe amri ya Kukamatwa kwa Mbowe, kisa ni vuguvugu la mjadala wa katiba mpya na tozo za miamala?!, Watanzania tusijue, aliyemkamata Mbowe, amezungumza na sababu ametoa, CNN badala ya kutafuta the reliable sources, wanatuletea wazushi na kutuletea uzushi!. Ukisikia Ajenda hasi ndio hizi!.

Kwa vile hii ni lugha ya watu, na pia naufahamu uwezo wa wengi wetu kwenye uelewa hizi lugha za watu, hivyo ili kuwasaidia wale wenzangu na mimi, sikiliza kwa makini jibu la swali la pili.
"it is a crackdown, she has launched or pretended to launch all along"

Watanzania Wazalendo lazima tuwe makini sana na Vyombo hivi, unaweza kujikuta unasambaza taarifa ya kuibagaza nchi yako, rais wako na watu wako bila kujijua.

Kipindi chote cha Mtangulizi, hizi media za nje zimekuwa zikituzushia mambo mengi tuu ya uongo na uzushi na serikali yetu imekuwa ikinyamaza bila kujibu, matokeo yake ni dunia kuaminishwa uongo, hivyo nashauri serikali yetu, awamu hii, tusinyamazie uongo na uzushi, tujibu mapigo tena kwenye vyombo vyao hivyo hivyo vya kimataifa. Tanzania tuna BBC, Reuters, DW, VOA, Blumberg, SABC, RFI, la Xhinua, tuwaite tuwaeleze ukweli, dawa ya uongo ni kuusema ukweli. Uongo ukisemwa na kuachwa kurudiwa rudiwa bila kukanushwa, sio tuu utaonekana kama ndio ukweli, bali sometimes hugeuka ukweli kabisa na kuja kutokea kwa sababu kauli nyingine huumba, kama uongo huu
Huu ulikuwa ni uongo tuu na uzushi, tukaunyamazia, ukaja kutokea kweli.

Tanzania ya Samia, tusinyamazie uongo na uzushi, wakizusha tuwaite tuwaeleze ukweli.

Uzalendo wa kweli ni kutanguliza mbele maslahi ya nchi yako, maslahi ya taifa lako, maslahi ya watu wako.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
Rejea za Mwandishi kuhusu media za Mabeberu.

Jeshi la polisi ni taasisi inayo jitegemea na kwasababu hiyo sidhani kwamba wana tekeleza shughuli zao kwa kupokea maelekezo kutoka kwa Rais. Nina hisi kwamba kwa lolote wanalo fanya ni lazima wote wakubaliane na matendo yao na waamini kwamba wanafanya kitu sahihi. Cha muhimu ni kufahamu kama shughuli za siasa katika kipindi ambacho sio cha uchaguzi zina halalishwa kwa sheria zetu.
 
elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
10,700
2,000
Nchi wafadhili ni pale wanapotufadhili, nchi marafiki ni pale wanapoungana na sisi, development partners ni pale wanapochangia maendeleo, ila mabeberu, pia ndio hao hao wanapotufanyia ubeberu.
P
Nyie nchi zote za ulaya mnaziita nchi za mabeberu cha ajabu mpaka nchi ambazo hazikuwahi kutawala popote mradi ni wazungu nao mnawaita mabeberu!
Nchi kama Kanada na Marekani ubeberu wake uko wapi! Kanada ilikuwa ikitupa misaada mingi sana ila tulipoendelea kuwaita mabeberu wakanywea. Marekani hawakuwahi kututawala lakini walijikita hapa kwa kutupa misaada hasa wakati wa njaa ya Nyerere kuanzia Rais Kennedy akiwa hai, nao unawaita mabeberu, Walitutawala wapi!
Wenzenu China waliona siasa za kukalia wanalialia na mabeberu wakati hawamo nchini mwao ni siasa za kijinga, wakaamua kuachana na fikira za mwenyekiti na kuingia kwenye biashara, leo china tuliokuwa tukiwacheka wako daraja la kwanza. Indonezya, ilikuwa masikini kama sisi, wabeba mzegamzega leo hatuwaoni wametokomea matawi ya juu! Sisi tunazidi kurudi nyuma huku maisha ya miaka ya sitini yakionekana bora zaidi kuliko leo, miaka hiyo kila mtu alikuwa na uhakika wa kula milo mitatu kwa siku na kusaza, mkaja na siasa zenu za kijinga za ujamaa ndani ya watu wasiokuwa na shida, matokeo mkaleta umasikini wa kutupwa ili muendelee kututawala na kujipa sifa ya chama tawala kwa sababu ya kuupenda ukoloni mweusi! Muingereza hakututesa na tuliishi naye kwa upendo bila kubambikiana naye makesi kama ilivyo sasa chini ya chama tawala.
CNN SIYO MABEBERU.
 
issenye

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
3,537
2,000
Mkuu Akasankara , kwani ni yeye?, yaani wewe unakuwa kama hawa mabeberu?, maadam kesi inasikilizwa, nashauri tusiingilie uhuru wa mahakama, nadhani hata Mama hapendi hizo mambo.
Wewe usiwe kama wale mabeberu kudhania hiyo kesi ni mpango wa Mama.
Mimi kwa maoni yangu, hii wiki inayoanza kesho haiishi kabla DPP hajapeleka Nolle!.
P
Huyo mama yako mbona yeye aliingilia mahakama na kusema kuwa anao ushahidi wa kutosha na kuwa watuhumiwa wengine walishahukumiwa/
 
Getang'wan

JF-Expert Member
Apr 9, 2015
2,685
2,000
Mbona sasa unatuambia sisi tusiingilie mahakama, je kwani sisi sio binadamu?
Kaka huyu jamaa ana msongo mkubwa sana wa mawazo baada ya majaribio mengi ya kutafuta uteuzi lakini haonekani kwenye rada. Hivi vitu anavyoviandika wakati mwingine ni namna ya kujifariji na kuondoa stress. Tumchukulie tu kama binadamu
 
Kinoamiguu

JF-Expert Member
Nov 29, 2018
5,349
2,000
Ficha upuuzi wako bhana kuna kitu gani cha UONGO hapo? Credible source ipi wakati raisi alishasema?
Una kimbelembele wewe kujidai mzalendo kumbe babayako nae alikuwa anabambikia watu case tuu
 
sem2708

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
4,669
2,000
Mkuu Akasankara , kwani ni yeye?, yaani wewe unakuwa kama hawa mabeberu?, maadam kesi inasikilizwa, nashauri tusiingilie uhuru wa mahakama, nadhani hata Mama hapendi hizo mambo.
Wewe usiwe kama wale mabeberu kudhania hiyo kesi ni mpango wa Mama.
Mimi kwa maoni yangu, hii wiki inayoanza kesho haiishi kabla DPP hajapeleka Nolle!.
P
🤣🤣🤣🤣
 
Deceiver

JF-Expert Member
Apr 19, 2018
7,392
2,000
Nikipoona tu TBC nikaacha kuendelea kusoma.
Ni sawa na mtu akisema amehojiwa na gazeti la Uhuru.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom