Watanzania tuwe makini,hali ya nchi kiusalama nafuu ya jana

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Watanzania tuwe makini,hali ya nchi kiusalama nafuu ya jana. Roho zetu zina tishwa kwa kusema ukweli na kuisimamia haki itendeke na haki siku zote haiombwi ila hunyakuliwa. Tumeruhusu sisi wenyewe kimakosa kuruhusu udikitekta ututawale kwa kukubali kujaribiwa,matokeo yake tuna uishi udikitekta mubashara bila chenga.

Watanzania mliambiwa msimpangie lakini akasahau kuwa urais haukupata kama ndoto, nanyi mkaa kimya,akapiga marufuku siasa mpaka 2020,ili atekeleze ilani ya chama chake,kwa kuwa ilani ya chama ni zaidi ya katiba,sheria na kanuni,nanyi mkalegea. Akathubutu kuzuia michango ya rambi rambi za matukio ya tetemeko kwa kejeri na dharau kubwa,lakini si bunge wala taasisi yoyote ya asasi za kiraia iliyo thubutu kumnyooshea kidole. Sasa leo tuna lia nini, wakati mchelea mwana kulia hulia yeye.

Ibara ya13.-(1) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano inasema wazi kuwa"watu wote ni sawa mbele ya sheria,na wanayo haki ,bila ya ubaguzi wowote,kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria.

(2)- ni marufuku kwa sheria yoyote iliyo tungwan na mamlaka yoyote katika Jamhuri ya Muungano kuweka sharti lolote ambalo ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake.

Vifingu vyote viwili vya ibara ya 13 vimesema bila kificho kuwa,watu wote ni sawa mbele ya sheria na wana haki sawa, iweje leo tubaguliwe kwa itikadi na kutweza utu wetu kwa kuwa baadhi yetu ni wapinzani? Kwani vyama hivi havipo kisheria na kama vipo kisheria kwa nini Watanzania tuna ruhusu serikali kuikanyaga katiba itakavyo nasi tupo kimya!!!

Watanzania wangapi leo hii wanafunguliwa kesi za kijinai kwa makosa ya kuionya na kukemea uovu wa serikali,lakini hakuna taasisi yoyote,au asasi za kiraia zilizo paza sauti zao na kufungua kesi za kikatiba kumtaka mtawala Magufuli aongoze kwa kufuata katiba,sheria na kanuni.

Alipo tangaza baraza lake la mawaziri,hakutoa instruments kwa mawaziri, wala hakutangaza kwenye gazeti la serikali,bunge lilipiga kelele,waziri mkuu aliahidi kufuatilia, lakini hakuna mrejesho uliorudi ndo maana mpaka kesho serikali inaendeleza double standard,kwa kuwa haiendeshwi kwa kufuata mwongozo bali utashi na mihemuko ya mtawala.

Makosa makubwa ni bunge la wananchi kugeuzwa idara ya serikali,kwa kutekeleza wajibu wake kwa mwongozo wa serikali na kukubali kuwa,bunge sehemu ya serikali, badala ya Rais kuwa sehemu ya bunge.

Ukandamizwaji wa bunge kupitia kiti cha spika,umeruhusu naibu wake kutoka serikalini,kulifanya bunge kukosa meno,na bunge kuwa sehemu ya kuhukumu wabunge wanao onekana mwiba kwa serikali. Hali hiyo imemjengea kiburi cha kimamlaka mtawala Magufuli, kwa kukiagiza kiti cha spika kitende kwa matakwa ya serikali na kuligeuza bunge kuwa mtetezi wa serikali.

Matokeo ya rafu hizo,serikali imekuwa ikilitumia jeshi la polisi kuwaburuza wabunge wa kambi ya upinzani bungeni, watakavyo bila bunge kupewa taarifa. Hadhi ya bunge imeshuka na kulifanya bunge la wananchi kuwa sehemu ya manyanyaso ya wawakilishi hao.

Tumeona hoja binafsi zikizuiliwa, kwa kuwa zina igusa serikali moja kwa moja,na kwa kuwa kiti cha spika kipo chini ya chama cha rais ,ambaye ndiye mwenyekiti wa chama anacho toka Spika,kiti kinashindwa kutekeleza majukumu yake,kwa kumuogopa mwenyekiti anaye pitisha majina ya wagombea ubunge ndani ya chama hicho.

Kushindwa kwa bunge kuisimamia na kuishauri serikali,kuna vunja nguvu mamlaka ya kibunge kusimamia sheria zitakazo Linda haki za binadamu na kuruhusu utekaji,mauaji yenye sura ya kisiasa na ukamatwaji wa watu wenye mawazo mbadala yanayo kinzana na serikali ya Mtawala.

Udhaifu huu na ulevi wa madaraka ni viashiria chanya ,kwa nia ya makusudi kuliangamiza taifa,kwa kuwa kundi linalo onewa likichoka uvumilivu hali ya nchi itakuwa tete.

Kuwakamata viongozi wa vyama vya siasa kwa maagizo toka juu,hakuifanyi nchi kuwa salama,kuwajengea hofu na uoga wananchi hakuipi CCM tiketi ya kutawala daima,zaidi zaidi kuna jenga chuki ya kiitikadi na kuwachochea wananchi waichukia serikali yao,kwa kuwa umewageuka na kuwa tishio la usalama wao. Wakisha ichukia nchi yao kinacho fuata ni kuihasi serikali.

Serikali isijione shujaa,kwa kunyamazia matendo ya uvunjifu wa amani,ugandamizaji katiba,ukiukwaji wa sheria na uvunjaji makubaliano ya mkataba wa amani wa Geneva,kwa kuwaona watawaliwa(wananchi) kuwa wajinga,nguvu ya umma ikisimama,bunduki zenu mlizo zinunua kwa kodi yetu kujilinda kwa ajili ya kutunyanyasa zitakuwa si kitu.,wala hazitatosha kutuangamiza wote.

Kwa kuwa Tanzania ni nchi yetu sote,serikali itafute muafaka wa kitaifa juu ya mustakabali wa amani ya taifa, kwani mchelea mwana kulia,hulia yeye.
 
Huyu yeye anaona ujenzi wa reli na barabara ni justification ya kukanyaga haki na uhuru wa watu wengine. Kama ni reli na barabara hata mkoloni alijenga. Tunataka utu wa watu urudi kuheshimiwa.
 
Tunataka umoja na mshikamano wa kitaifa,kutugawa ili mtutawale hakuna wafanya mfikie malengo yenu,tusiruhusu upanga utawale
 
Back
Top Bottom