Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,684
- 149,887
Watanzania wapenda mabadiliko tunawajibu wa kuwaunga mkono wabunge wa UKAWA Kwa kuwachangia fedha zitakazowasaidia kuendesha mikutano yao nchi nzima iwapo CHADEMA watashinda kesi dhidi yal polisi na wao kuendelea na mikutano yao kama walivyopanga.
Vile vile kama wale wabunge wa UKAWA waliobaki Dodoma hawalipwa hata perdiem, fedha itakayopatikana itumike pia kuwarudishia fedha walizotumia kukaa Bungeni mpaka sasa maana hawabaki Dodoma kwa masilahi yao bali ni katika kutupigania sisi watanzania masikini. Tunaambiwa hivi sasa wanaendesha vikao vyao katika ukumbi wa Msekwa huko Bungeni.
Watanzania hatuna budi kuwaunga mkono wabunge hawa na si kuwaacha peke yao kwani mzigo wanaoubeba si wao bali wanaubeba kwa niaba yetu.
Naomba uandaliwe utaratibu naamini wengi watakuwa tayari kuchangia.Hatupaswi kuwaacha wabunge hawa bila msaada.
Michango ya aina hii itakuwa ni kielelezo tosha cha nguvu ya umma katika kutafuta haki na usawa kwa wote.
NB:
Bora sisi wenye utamaduni wa kuchangishana fedha kugharamia shughuli za chama kuliko wanaotumia mamlaka yao kukwapua mafungu ya fedha kugharamia kampeni za chama chao na kuendesha shughuli nyingine za chama.
Naona kuna watu povu linawatoka.Kama wewe ni mvaa pampasi hii mada elewa haikuhusu bali inahusu wapenda mabadiliko kama inavyojieleza. Sisi hatukwapui,tunachangisha na hatujaanza leo.