Watanzania tuunganishe nguvu kumdai Rais Kikwete haki yetu!

kindafu

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
1,346
1,676
Watanzania wenzangu mie nafikiri kwa hali ilivyo tete kuhusu mgomo wa madaktari, tuna haki na sababu ya msingi ya kumbana Rais Kikwete atuhakikishie usalama wetu na hatma ya afya zetu. Yeye mwenyewe kwa hiari yake alitupigia magoti akatuomba tumchague kuongoza serikali na akatuahidi maisha bora kwetu sote. Hata kama hatukumchagua sote au kama isemwavyo kwamba alichachua matokeo ila pia alikula kiapo cha kutimiza hayo. Na ili kumwezesha yeye kutuletea hayo maisha bora sisi Watanzania tunamlipa kodi.
Katika hili la mgomo Raisi Kikwete ndo mdaiwa wetu kwani ndo tuna mkataba naye na sio madaktari!

Nawasilisha wakuu!
 
unaongea na mfu,afya yako nayo imechakachuliwa,pole sana kwani wagagagigikoko hawatakulewa wamezoeshwa shida
 
Natafakari pa kuanzia kudai haki yetu kwa hii serikali ya Jk, bado sipaoni. Kinachonipa hofu zaidi ni pale ninapokumbuka watu wenye majina makubwa nchini kama Mwakyembe kutosikilizwa madai yake ya kuuwawa pamoja na kuwakilisha ushahidi wa kimaandishi kwa wakuu wa nchi. Sasa sisi walalahoi tutaonekana wapi? Labda suluhisho ni kufanya yaliyofanywa huko Tunisia, Misri, Libya na sasa Yemen/Syria?
.
 
Kwa taarifa yako watanzania wenye elimu ya urai nikiwepo mimi tutakuelewa nini unasema na kwamba hilo kwa rais sio ombi bali ni jukumu lake. Lakini kwa walio wengi na tena ambao hawajui elimu ya urai na bahati mbaya kabisa hawafiki jukwaa hili la kijamii, hilo haliwezekani maana wanajua rais ni Mungu na mambo kama hayo atayafanya akipenda. Hebu hapo ulipo elimisha watu 10 na hao 10 uwaombe wawaeleweshe wengine 10@ hapo tutaweza la sivyo wao wataendelea kuamini sisi ni taifa changa na umasikini ni jadi yetu. Hali ambayo itaendelea kuwafanya kuwaita viongozi waheshimiwa hata kama hawatekelizi wajibu wao.
 
Kuwepo kwa serikali ya magamba madarakani, walah waTZ tumepaka wanja wa pilipili. Yewomiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!
 
Back
Top Bottom