Watanzania tuungane kupinga ajira za undugu TRA, BOT, TBC, EWURA

Mwita Maranya hii secretariat inakinzana na sheria zingine za uanzishwaji wa taasisi za serikali. Kuna taasisi ambazo sheria zake zinasema kwamba mkuu wa taasisi ndiye ana uwezo wa kuajiri na kufukuza. Lakini sasa kuna hii sheria ya hiyo secretariat inasema yenyewe ndio inatakiwa kuinterview watu na kuwapost kwenye taasisi. Hivyo unakuta watu wanapelekwa kwenye taasisi huku hawana uwezo"

Wapo katika mchakato wa ajira zilizotangazwa hivi karibuni zikiwamo za Makatibu kata, wahadhiri- Mwl JK nyerere, CBE, Chuo cha Miponago Dodoma. Kinachoendelea huko ni vimemeo na undugu tu! tusibiri matokeo!
 
Namba tano mi nimeanza kuifanyia kazi,,,nimeshabadili KABILA
Kutokana na hali ilivyo, kwenyemijadala ya namna hii, Great Thinkers, je iwe:

1. Marufuku tasisisi ya umma (au hata binafsi?) kuwa na watumishi zaidi ya mmoja wanaotoka ama mkoa mmoja, au wilaya moja, au hata kabila moja?

2. Ni Marufuku kwa mtu yeyote kuomba kazi kwenye taasisi ambayo tayari kuna mtu wa kabila lake?

3. Katika CV, lazima kiwepo kipengele kinachoulizia kabila (kama ilivyo kwa dini?

4. Kabila la mtu liingizwe kwenye vitambulisho vya taifa vinavyokaribia kutoka?

5. Kuwe na uwezekano wa kubadilisha kabila, ili hata makabila mengine yafaidi?

6. .....

7.......
 
Mmh hapo TRA,BoT,TBC,na Ewura lazima uwe muhaya hata kama huna elimu kazi utapata tu cha msingi uwe na ndugu

Siku hizi Tanzania haina kabila mashuhuri au lenye nguvu, kwa hiyo ukabila hauna nafasi tena. Kilicho na nafasi ni tabaka la wenyenacho na wasiokuwa nacho. Achana na chuki zisizokuwa na maana kwa kulishwa ujinga ambao hauwezi kuutetea. Mtoto wa Balozi Kagasheki kuolewa/kuoa mtoto wa Mwinyi hakutokani na makabila yao bali ukaribu wao. Mtoto wa Mramba kuolewa na mtoto wa Msiba hautokani na makabila yao bali ukaribu wao. Fikiria mazingira yaliyokuzunguka utaona ukweli ninao ueleza. Achana na kabila, achana na dini!
 
taanzania tanzania nakupenda kwa moyo wooote nji yangu tanzqania jinalako ni tamu saaaana
niamkapo nakuwaza wewe nilalapo ni heri mama weeeeee


Niliitwa B.O.T kufanya interview IT department nilijuta kumbe nilienda kuuza sura kwenye vile viyoyozi maana ilikua ni stress interview kwa wengi wetu undugu unafanyika waziwazi mtu anamleta mtoto wake au ndugu yake bila aibu hawasubiri utaatibu wa kuingia kwa kuitwa wao wanapitiliza na kuondoka sie kina kayumba tuliwekwa hadi jioni
 
haya mambo ya kupata ajira kwa memo/kujuana ndo yametufikisha hapa tulipo watu maofisi hawafanyi kazi na hakuna wa kuwawajibisha kwakweli taifa letu linapitia katika hali tete sna mm ushauri wangu kwa vijna waliomaliza elimu ya juu ni kujaribu kujiajili najua mwanzo ni mgumu sna na vjna wengi hatuna ujasiri wa kujiajili achilia mbali mtaji wa kukuwezesha kujiajili nasema hya kwasababu nimepitia huko mpka nikaamua kujiajili mwenyewe kwa kufungua kampuni za ujenzi moja nikiwa partner nyingine nikiwa peke yangu,yote kwa yote hakuna lisiloshindikana,vjna wasomi ndio wawe waanzisha mwendo katika kufungua soko la ajira tusikae kusubiri kuajiliwa tu siku hzi hta mwanasheria anakuwa bank teller sasa ww uliyesoma mambo ya fedha cjui utaenda wap ni changamoto kwakweli
 
Hii ndio Tanzania yetu ya sasa.Tunakoelekea ni kubaya sana.Ajira za serikali na mashirika yake zipo mifukoni mwa wanamtandaoni flani hivi hapa nchini.Mtandao huo ni wa wale wenye kipato cha juu ambao wanadhani kuwa kila kitu kizuri hapa dunian ni kwaajili yao na familia zao,jamaa na marafiki zao.ndio maana zikitangazwa nafasi 20 wao huwa tayar wameshachukua 10 mpaka 15 zinazobaki na za makabwela wanaoshinda barabarani wakizunguka bila ma Godfather.

Huu ni mtandao unaoanzia ktk watu kupata mikopo ya elimu ya juu.serikali inadai mara nyingi tu kuwa hawana pesa za kutosha kukopesha wanafunz wote wa elimu ya juu lakin cha ajabu wanaopata mikopo hiyo weng wao ni wale ambao familia zao zinajitosheleza kwa kila kitu wangeweza kujilipia na bas hcho kidogo cha serikali wakakopeshwa maskini ambao nadhan ndio walengwa.Cha kushangaza vijana hawa wa WANAMTANDAO ndio wakipata pesa za mkopo ushinda kwenye mabaa na starehe kwakuwa wanajua hata hiyo pesa ikiisha basi wazazi wao wanawaongezea maradufu za kutumia.

wengi wa hawa vijana wa wanamtandao uwa hawafaulu kwa kiwango cha juu chuoni maana muda mwingi wanautumia kwenye starehe na mengineyo,na roho zao uwa haziwasuti hata kidogo.

wakimaliza vyuo upewa nafas ktk makampuni ya familia zao au jamaa wa familia zao,wakati huohuo wakitafutiwa nafasi katika serikali na familia zao kwa kushirikiana na jamaa,ndugu na marafiki wa familia zao.

hili la kusema udini,undugu na ukabila uangukia hapa japo uwa si lazima likawa linafanyika intentionally.kama mtu ni mchaga,obvious rafiki wengi wa familia yake ni wachaga tena wakristu wanaosali kanisa moja.kama mtu ni muislamu rafiki weng wa familia yake ni waislamu ambao usali pamoja na hata kualikana wakati wa mfungo wa Ramadhani.hili halina ubaya but ndio network yenyewe ambayo wanasaidiana katika mambo mengi.

sasa suala linalojitokeza ni pale ambapo wanaombeana kusaidia watoto wao waliomaliza vyuo,lazima itaangukia ktk sura hiz za udin,ukabila na urafiki.Maskini asiekuwepo ktk mtandao huu lazima AUMIE hata kama tu.
 
kweli hizi idara zina mizengwe ile mbaya kweli na huku ndiko kwenye vyeti fake kila kukicha kama wanabisha waanze kuchunguza vyeti TRA ndio utaona kuna madudu yakufa mtu
 
Jamani wacheni kutuponda wenye wenye GPA za 2.5 Mimi nina haiyo GPA na nimefanya kazi ya kuajiliwa miaka mitatu na nimekuwa the best employee zaidi ya hao wenye GPA za 4, na nikaingia kwenye kujiajili ndani ya miaka minne nika perfom na sasa nina kampuni tatu kubwa nimeajili wazu zaidi ya ishirini na tano kama wafanya kazi wa moja kwa moja
 
jamani acheni kugeneralize mambo, mimi binafsi niliomba kazi BoT na nikapata kazi bila hata ya kumjua mtu yoyote
 
Mtu wa tabaka la chini ni ngumu sana kuassociate moja kwa moja na kundi hili la tabaka la juu maarufu WANAMTANDAO maana limejaa watawala,maboss wa mashirika ya kiserikali na vyombo vya dola.kundi ambalo kwa kias kikubwa linakwamisha maendeleo ya nchi maana wao wanajali zaid matumbo yao.

Sasa kwa mfano zikitangazwa nafasi za kazi 30 wao wanalink fasta na unakuta nafas kama 15 hiv wameshazibeba,wengne hawafanyi hata interview na wanakua tayar wameshajiassociate na shirika husika eti wanavolunteer au wapo kwa mikataba mifupi(ambayo maskin haimuhusu maana uwa haitangazwi popote maarufu km fall vacancy).Na hata interview zinapofanyika,maana yake ni kuwa tayar nafas zinazogombaniwa zimeshapungua hapo.

Kwahiyo hapa tatizo kubwa uwa ni mambo ya kujuana ambayo yanabeba sura za udin na ukabila lakin chanzo chake ni tabaka la watawala na watawaliwa.na kibaya zaid watawala ndio wenye nacho zaid maana wao ni wabadhilifu na wez wa mali za umma kwa njia tofauti tofauti.

maskin akipata nafas ktk mashirika hayo ni pale ambapo kapewa msaada na mtu wa tabaka la juu au kagombea tunafas tuwili tutatu tulitobakia.

maskin mwenye GPA ndogo si rahis kupata kazi lakin wa tabaka la juu na GPA yake ndogo ni rahis kupata ajira.MAskin mwenye GPA kubwa si rahisi pia kupata ajira,lakin tajir mwenye GPA ya juu ni rahis kama kumsukuma mlevi.

Tabaka hilo linaumiza wengi kwani ndilp limejimilikisha mali za umma,na pia linamiliki makampuni binafsi ambayo pia hayaajiri watu yasiowafahamu.Kibaya zaid ndilo linainfluence hata ajira ya kampuni za kigeni maana uwa yamewapatia 10%.ndio tabaka linalofanya biashara haramu na kujihusisha na pesa haramu.Maskin kabanwa kila kona

TRA mara nyingi wamekuwa wakioutsource NBAA kuendesha zoez la usahili,lakin Mkurugenz wa NBAA ameshasema mara nyingi TRA hawaajiri watu ambao wameshinda intetview hizo,kisa hawako free ktk recruitment wanaingiliwa sana na maboss wa serikali kuu.

TANZANIA NCHI YANGU!
 
Sasa ufisadi wa kupandishwa vieo ndio balaa kwa makapuki waliopata ajira kwenye taasisi hizi kwa bahati mbya.Simba na tembo huishi kingdom family tofauti na nyumbu.
 
Back
Top Bottom