Watanzania tuungane kupinga ajira za undugu TRA, BOT, TBC, EWURA

Nenda pale TRA ukaone ina maana wenye uwezo na waliosoma ni wachaga tuu, karibu kila nafasi imeshikwa na mchaga katika hali ya kawaida huwezi kusema wao ndiyo wana uwezo tu utaona matangazo lakini utashangaa. pale TRA kuna nafasi za kazi za ndani lakini utashangaa anatolewa mtu nje mchaga aje kujaza nafasi. Kwa kweli panahitaji kuchunguzwa kwa umakini vinginevyo ile taasisi ni ya kabila moja UCHAGAAA tuuuu.
 
Mwita Maranya hii secretariat inakinzana na sheria zingine za uanzishwaji wa taasisi za serikali. Kuna taasisi ambazo sheria zake zinasema kwamba mkuu wa taasisi ndiye ana uwezo wa kuajiri na kufukuza. Lakini sasa kuna hii sheria ya hiyo secretariat inasema yenyewe ndio inatakiwa kuinterview watu na kuwapost kwenye taasisi. Hivyo unakuta watu wanapelekwa kwenye taasisi huku hawana uwezo.

Kimbunga,
Nakubaliana na wewe lakini ufahamu kwamba sekretarieti inainterview watu na kuwapeleka sehemu baada ya kupata maombi ya taasisi/idara husika.
Kilichonisikitisha ni kupeleka watu sehemu kazini, wakifika huko wanakataliwa na wakirudi sekretarieti wanashindwa kuwasaidia, wakati huo kule walikokataliwa wanaajiri watu wengine wanaowataka (ndugu zao) bila kupitia sekretarieti lakini hakuna hatua zozote zinazochukuliwa.
 
Last edited by a moderator:
Hali ni hiyohiyo UwT, Polisi, Magereza, juzi nilikwenda pale bodi ya mikopo ya wanafunzi WAJALUO kibao, DAWASCO unaweza kukuta baba, mama, mtoto, mkwe,..., wote wameajiriwa pale! Kwa kweli nchi inarudi kwa kasi ya ajabu kwenye ukabila, udini, ukoo, hasa kwenye ajira.
Zamani waajiri walikuwa wanawasiliana na vyuo ili kupata wafanyakazi wapya na ajira kubwa zilitangazwa kwa uwazi. Tumeacha haya. Sasa hivi ni vimemo kwa kwenda mbele.

WildCard kumbe Omela Nyatega nae ameshaanza kufanya mambo?
Kweli nchi hii tumeanza kuhamasisha udini, ukabila na kujuanazation kwa kasi ya ajabu.
 
Last edited by a moderator:
WATANZANIA tuache kulalama, moja uwe na shule ya kweli katika tasisi hizi especially BoT na EWURA kwani vigezo vya kuingia katika post nyingi 90% lazima uwe na masters, pale EWURA mchemsha chai ni Form Six ambaye kwa sasa anasomea degree ya Sheria, kuna undugu hapo? Matatizo yetu tumekuwa tukilalama tu! kinachokupeleka sio undugu bali shule ya mtu. Kwa mfano EWURA ina wafanyakazi 99 kati ya hao 80 wana Masters ya maeneo husika na wanaobaki wana degree na qualification nyingine! kwa maana hivyo, usije ukasoma kadiploma ukategemea kupata kazi EWURA- Regualation is a new field that needs highly specialized personalities.

isaiah nina kila sababu ya kuamini kwamba utakuwa ni mnufaika wa mfumo mbovu wa ajira ya kupendeleana unaolalamikiwa.
Unadhani kwamba hawa wanaolalamika hawana hizo sifa unazotaja? Kwanini taasisi moja ijae wat wa kabila moja? Au mkoa mmoja? Au au wale wale ambao baba/mama zao wako humo humo serikalini?
Hii nchi sasa inageuzwa kuwa ya watu wachache ni lazima tukemee hali hiyo!
 
Last edited by a moderator:
WildCard kumbe Omela Nyatega nae ameshaanza kufanya mambo?
Kweli nchi hii tumeanza kuhamasisha udini, ukabila na kujuanazation kwa kasi ya ajabu.
Hata yule ofisa uhusiano wake ni MJALUO! Hawatumii majina ya Onyango, Otieno, Ogolla,...Shida tulionayo ni nafasi hizi kubwa mtu anaweza kukaa nayo kwa zaidi ya miaka kumi. Anaigeuza taasisi anayoiongoza inakuwa mali yake kabisa. Anaajiri na kufukuza anavyotaka. Yule Kilaghane wa TPDC kakaa pale zaidi miaka 20 sasa. Vivyo hivyo Mutalemwa wa DAWASA. Nyatega pale bodi ya mikopo naye amedumu pale. Wakuu wa Taasisi hizi ndio chanzo cha yote haya. Wangepewa vipindi viwili tu vya miaka mitanomitano.
 
Kutokana na hali ilivyo, kwenyemijadala ya namna hii, Great Thinkers, je iwe:

1. Marufuku tasisisi ya umma (au hata binafsi?) kuwa na watumishi zaidi ya mmoja wanaotoka ama mkoa mmoja, au wilaya moja, au hata kabila moja?

2. Ni Marufuku kwa mtu yeyote kuomba kazi kwenye taasisi ambayo tayari kuna mtu wa kabila lake?

3. Katika CV, lazima kiwepo kipengele kinachoulizia kabila (kama ilivyo kwa dini?

4. Kabila la mtu liingizwe kwenye vitambulisho vya taifa vinavyokaribia kutoka?

5. Kuwe na uwezekano wa kubadilisha kabila, ili hata makabila mengine yafaidi?

6. .....

7.......
 
Tume ya Ajira utumishi wa UMMA ivunjwe; Unaweza kwenda fanya interview harafu ukiambiwa vile unaacademic transcript tu ambazo ni original huwezi kupata kazi mpaka uje na certificate; unafukuzwa baadala ya kukufanyia interview na kama unafanikiwa wakuombe upeleke certificate ili kuanza kazi; Sasa mazingira haya ni rushwa tupu, kwani cheti kile cha chuo chenye jina lako na digrii ulomaliza ni cha muhimu kuliko academic transcript yenye GPA na dgrii yako ulosemea??? Ni kama mbinu mbinu hivi ktk ajira.

RUSHWA RUSHWA inatumaliza
 
Kutokana na hali ilivyo, kwenyemijadala ya namna hii, Great Thinkers, je iwe:

1. Marufuku tasisisi ya umma (au hata binafsi?) kuwa na watumishi zaidi ya mmoja wanaotoka ama mkoa mmoja, au wilaya moja, au hata kabila moja?

2. Ni Marufuku kwa mtu yeyote kuomba kazi kwenye taasisi ambayo tayari kuna mtu wa kabila lake?

3. Katika CV, lazima kiwepo kipengele kinachoulizia kabila (kama ilivyo kwa dini?

4. Kabila la mtu liingizwe kwenye vitambulisho vya taifa vinavyokaribia kutoka?

5. Kuwe na uwezekano wa kubadilisha kabila, ili hata makabila mengine yafaidi?

6. .....

7.......
Suala la ajira kwenye taasisi za UMMA na serikalini liratibiwe vema na kufanyika kama ifuatavyo:
-Kuwepo na TUME moja ya ajira ambako maombi yoote ya nafasi za kazi yatapitia huko toka kwa waajiri na waajiriwa.
-Viongozi wakuu wa taasisi za umma waajiriwe kwa vipindi viwili vya miaka mitano kila kimoja basi.
-Udahili na usaili uwe wa wazi kwa nafasi kubwa za taasisi za umma na vyombo vya Dola.
-Nafasi zote za kazi isipokuwa za KISIASA zitangazwe kwa uwazi.
-Watu wasiongezwe mikataba muda kustaafu unapofika. Tunao WATANZANIA wa kutosha sasa wenye sifa.
 
[h=2]sio undugu tu, kuna udini, urafiki, ukabila, uchama na rushwa za aina zote[/h]
 
Hata yule ofisa uhusiano wake ni MJALUO! Hawatumii majina ya Onyango, Otieno, Ogolla,...Shida tulionayo ni nafasi hizi kubwa mtu anaweza kukaa nayo kwa zaidi ya miaka kumi. Anaigeuza taasisi anayoiongoza inakuwa mali yake kabisa. Anaajiri na kufukuza anavyotaka. Yule Kilaghane wa TPDC kakaa pale zaidi miaka 20 sasa. Vivyo hivyo Mutalemwa wa DAWASA. Nyatega pale bodi ya mikopo naye amedumu pale. Wakuu wa Taasisi hizi ndio chanzo cha yote haya. Wangepewa vipindi viwili tu vya miaka mitanomitano.

umesahau TRA
 
Suala la ajira kwenye taasisi za UMMA na serikalini liratibiwe vema na kufanyika kama ifuatavyo:
-Kuwepo na TUME moja ya ajira ambako maombi yoote ya nafasi za kazi yatapitia huko toka kwa waajiri na waajiriwa.
-Viongozi wakuu wa taasisi za umma waajiriwe kwa vipindi viwili vya miaka mitano kila kimoja basi.
-Udahili na usaili uwe wa wazi kwa nafasi kubwa za taasisi za umma na vyombo vya Dola.
-Nafasi zote za kazi isipokuwa za KISIASA zitangazwe kwa uwazi.
-Watu wasiongezwe mikataba muda kustaafu unapofika. Tunao WATANZANIA wa kutosha sasa wenye sifa.

Mkuu Wildcard, shukran.

-Hiyo Tume (Secretariat ya Ajira) si ndiyo inalalamikiwa pia? Watumishi wa tume hawana makabila?
-Kuna taasisi nazifahamu ma CEO wake ni mikataba ya miaka mitano mitano na hao pia wanalalamikiwa.
-Kisheria, taasisi zote za umma (na nyingi za binafsi) zinatangaza nafasi za kazi, lakini ndo hii sasa malalamaiko yanasema matokeo yanapangwa, ku favour watu "wa makabila yao." Tufanyeje?
Nakubaliana nawe kuwa nyongeza za mikataba kwa wastaafu haaina tija kwa waajiriwa watarajiwa.
 
acha kulalamika, ajira zinatangazwa wenzako wanaomba wanapata ajira we unakataa kuomba kwa hisia potofu kuwa watu wamekwishaajiriwa utabaki unachonga saaana wenzako wanapeta na vigezo vyao

Acha na wewe kuwa na hisia potofu. Unajuaje kuwa hakuomba?
 
Mmh hapo TRA,BoT,TBC,na Ewura lazima uwe muhaya hata kama huna elimu kazi utapata tu cha msingi uwe na ndugu

Hapo ilikuwa ZAMANI, tokea ameingia Ndulu mambo yamebadilika sana sana, yule mtu ameibadili BoT kwa kiasi kikubwa, mimi binafsi nafurahia na nampongeza kwa hilo. Zamani BoT walikuwa wafujaji wakubwa wa pesa ukiachia ajira kwa watoto wa wakubwa, lakini sasa hivi hata ukienda kwenye workshops na seminars zao ni kazi tu! watakwambia seminar inaanza saa tatu asubuhi mpaka saa sita mchana, na unapewa korosho , maji na jiuce , or wanakwambia mkutani ni saa moja na nusu na inamaanisha hivo na si vingine, wakati zamani workshop ya kufanyika masaa mawili inafanywa bagamoyo au Mwanza tena kwa wiki tatu loh! ila sasa hivi Ndulu amejitahidi kuondoa ufisadi kuanzia ajira, hata kama ipo basi ni kwa uchache sana sana !

HApo sikubaliana na wewe !
 
Limekuwa jambo la kawaida kwa mashirika tajwa hapo juu kutoa matangazo ya kaz kutimiza tu matakwa ya sheria lakin tayari huwa wanakuwa na watu wao. Watoto wa vigogo ndo wamekuwa wakinufaika huko walalahoi na vyet vyao vizur wakisaga lami

Sina shaka hili ni tatizo la kitaifa kwani hivi sasa kwenye na makampuni walala hoi wamekuwa wakiacha kazi na kwenda kufanya mambo yao binafsi ya ujasilia mali kwani uonevu na upendeleo kwa watu fulani umezidi na hii ni changa moto wizara ya utumishi na wizara ya kazi. Watapaki na watumishi vihiyo na wanandugu watupu na shirika kufa kabisa maana serikali imeshindwa kuliona hilo.
 
acha kulalamika, ajira zinatangazwa wenzako wanaomba wanapata ajira we unakataa kuomba kwa hisia potofu kuwa watu wamekwishaajiriwa utabaki unachonga saaana wenzako wanapeta na vigezo vyao

wewe uliajiriwa mwaka gani?
 
Limekuwa jambo la kawaida kwa mashirika tajwa hapo juu kutoa matangazo ya kaz kutimiza tu matakwa ya sheria lakin tayari huwa wanakuwa na watu wao. Watoto wa vigogo ndo wamekuwa wakinufaika huko walalahoi na vyet vyao vizur wakisaga lami

kama hawajui haya ndio mambo yanayowakasirisha waTZ wengi kwasbb kama vyeti vya shule sote tunavyo ila sehem nzuri waTZ wa kawaida hawapati utasikia ni mtt/ndg wa rais,wazir,balozi,chama,jeshi na other big shots. at last wanafanya cold chuki
jamani wasiasa tuwe makin na hili kwani siku chama kikianguka. mhhhhhhhhhhhhhh kama unavyofikiria ww kitakacho tokea...
kila mTZ anapenda awe na kipato stahili na hicho kinapatikana kwenye mashirika/vitengo fulani,
 
Back
Top Bottom