Msambichaka Mkinga
JF-Expert Member
- Oct 22, 2015
- 1,649
- 2,911
Mtu mvivu na mjinga ni lazima awe maskini, na mtu maskini siku zote hufikiria umaskini wake umesababishwa na mtu mwerevu, mwenye bidii na tajiri.
Watanzania tumekuwa watu wa kulaumu kupita kiasi. Tunawalaumu wazungu kuwa wanatunyonya. Tunashindwa kufahamu kuwa kukubali kunyonywa ni dalili ya uvivu na ujinga. Mtu mwerevu na mwenye akili hawezi kunyonywa, ukinyonywa itakuwa kwa muda tu.
Kwa waafrika huko tunakokuita kunyonywa kunaonekana kuwa na faida zaidi kuliko tukaachwa bila kunyonywa. Tunalalamika kuwa tunanyonywa kwenye uchimbaji wa madini lakini katika huo tunaouita unyonywaji angalao tunaambulia kodi na fedha za kigeni, tusiponyonywa hatuwezi kuchimba madini, na hata tukichimba hakuna kungine kwa kuyapeleka zaidi ya huko huko tunakokuita kwa wanyonyaji.
Lakini tunavyofanyiwa sisi leo, na mataifa mengine ya huko Ulaya na Amerika yalifanyiwa hivyo hivyo. Ni Waingereza ndiyo waliochimba madini ya Marekani na Canada. Ni Wakanada ndiyo waliochimba madini ya Australia, ni Waustralia, Wamarekani na Wakanada leo ndiyo wanaochimba madini ya China. Mbona hayo mataifa mengine walikuwa na wawekezaji wa mataifa mengine na bado kwa kupitia uwekezaji wa nje waliweza kuyajenga mataifa yao kiuchumi na kiteknolojia? Kwa nini Afrika inashindikana?
Mataifa kama Marekani, Kanada na Australia yaliwahi kupokea misaada toka Uingereza. Ujerumani iliwahi kupokea misaada toka Marekani. Ni misaada hiyo hiyo ndiyo iliwapa nguvu ya kusonga mbele. Sisi kwa nini misaada tunayoipokea haitotoi mahali tulipo? Tatizo ni watoa misaada au tunaopewa misaada?
Tunasema hii misaada inawanufaisha wazungu watoa misaada. Kijiji kwetu tuna mradi wa maji na umeme tuliosaidiwa na Wajerumani kwa kupitia kanisa. Baada ya kukamilika miradi hiyo tukakabidhiwa. Baada ya miaka 10, umeme na maji vyote havitoshelezi mahitaji yetu, tumeanza kuomba tena. Hivi huu mradi unawapa faida gani Wajerumani? Kwa nini tumeshindwa hata kuuendeleza ili uendane na ongezeko la watu?
Watanzania ni walalamikaji hata kwa mambo ya kipuuzi kabisa. Wazungu wanasaidia kutujengea barabara halafu utamsikia mswahili kuwa humo wanamochimba siyo bure, wanachukua madini yetu. Ujinga mkubwa! Hivi madini yanachimbwa kama kokoto za kujengea? Kama ni rahisi kiasi hicho kwa nini usiende kuchimba na wewe?
Matatizo makubwa ya Afrika ni ya Waafrika wenyewe.
Mataifa mengi ya Afrika yana viongozi ovyo kabisa. Yana viongozi wabinafsi, wachoyo, walaghai, wasio wabunifu, ma wasio na upendo kwa watu wao.
Mataifa ya Afrika yana tawala zisizo na demokrasia na zinazofurahia udikteta. Ndiyo maana siyo ajabu kiongozi wa Afrika bila aibu anasimama na kusema, 'mimi nitatawala mpaka nitakapoacha mwenyewe, chama chetu kitatawala milele, n.k.', huo ndiyo uongozi wa Afrika usio na tija kwa waafrika.
Waafrika ni wavivu, hawana ubunifu, ni mabingwa wa kulalamika. Ukitaka kuona matatizo ya Waafrika, safiri hata na basi tu kuelekea mikoani, dereva anasimamisha gari pembeni ya barabara, na abiria wanasambaa vichakani kujisaidia, mpaka leo mwafrika hajui wapi anatakiwa kuweka kinyesi chake! Kipindupindu kikija anasema magonjwa haya yamesababishwa na wazungu ili watengeneze dawa wapate hela.
Ukitaka kuona roho mbaya ya mtu mweusi, angalia tu hata barabarani wanavyoendesha magari. Dereva anahangaika kuhakikisha mwenzie aliye pembeni asipate nafasi ya kuingia barabarani, au wanaoingia barabara kuu wakipata nafasi hawataki watoe nafasi kwa waliowapa nafasi na wenyewe wapate nafasi kwenye barabara ambayo wote wanatakiwa kuitumia. Angalia mtu kapiga suti yake, na digrii mbili kichwani anavyokunywa maji na kurusha chupa barabarani, akiulizwa atakuambia kuna wafagiaji wanaolipwa.
Angalia Polisi wasivyo na upendo kwa raia wenzao. Mtuhumiwa, na wakati fulani kwa kuonewa tu, anaenda kukamatwa, hajakataa, polisi anaanza kumtandika, kamkwida nyuma kwenye suruali anamtembeza kwa vidole, n.k.
Waafrika wanapigana wenyewe kwa wenyewe. Wakianza kuuana wanaanza kulalamika kuwa jamii ya kimataifa kwa nini haikuzuia mauaji? Na sisi Waafrika kwani ni nani aliyesema tupigane? Mara utasikia hivi vita vinachochewa na mataifa yanayotengeneza silaha. Ina maana sisi hatuna akili? Ikitokea mtu anatengeneza mikuki, akanishaishi ninunue, nikinunua nikaenda kumwua ndugu yangu, wa kulaumiwa ni anayetengeneza mikuki au mimi kwa uwendawazimu wangu niliyeenda kununua mkuki kwaajili ya kumwulia ndugu yangu?
Watanzania kama tunataka kupata maendeleo, kabla ya kuwalaumu wazungu, tuangalie zaidi udhaifu wetu. Sisi tuna matatizo mengi sana yanayosababishwa na uroho wa madaraka, ubinafsi, uchoyo na uvivu.