Watanzania tutegemee bei ya mafuta kushuka zaidi hapa Nyumbani, baada ya Iran kushindwa kuelewana!

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,224
1,676
Bei ya mafuta yaporomoka Iran
160417152309_oil_meeting_doha_512x288_epa_nocredit.jpg
I
Bei ya mafuta imeshuka ghafla nchini Iran, baada ya wasambazaji wakuu kushindwa kukubaliana katika mipango ya kusimamisha uzalishaji ili kuweza kupunguza kasi ya usambazaji wa mafuta hayo.Ndani ya saa chache,bei ya mafuta ilishuka kwa Zaidi ya asilimia tano.

Wazalishaji wa mafuta walikuwa na matumaini ya kuongeza bei lakini maongezi hayo yalisababisha mgogoro kwa Iran ,nchi ambayo ndio soko linalotegemewa.

Saudi Arabia haikutaka kujitoa katika uzalishaji labda kama Iran itakubaliana kufanya sawa na wao ingawa Wairani wanataka kuuza mafuta Zaidi ili kunufaika Zaidi kimataifa.


Chanzo: BBC
 
Iran ni soko linalotegemewa na nani na nini kinachotegemewa? Kwani Iran wenyewe ni wazalishaji mafuta wakubwa.

Amma mleta mada hujaeleza vizuri amma huko ulikoitowa hii habari kama ulikopi na kupesti basi hawajaeleza vizuri.

Haieleweki.
 
Ni kwamba Iran wamegoma kuingia katika Jumuiya yao ya soko la pamoja la wanaochimba mafuta kwa wingi ili kuweka kupunguza kiwango cha uzalishaji kufanya bei iwe stable..yeye Iran kasema atakubaliana na hoja izo mpaka atakapofikia level ya kuzalisha pipa 4 milioni kwa siku..iyo imefanya US kushuka bei 79cent za crude oil na kuwa 37.71 kwa pipa moja...
 
ACHA OPEC WAVURUGANE NA SISI TUPUMUE , MAANA MIAKA KUMI ILIYOPITA SIKUTEGEMEA BEI KIUWA KAMA ILIVYO LEO
 
Hata ikipunguaje hio bei kwenye soko la Dunia kwetu huku ni bei ile ile kama Kawa
 
Back
Top Bottom