Watanzania tutazidi kutiana aibu mpaka lini ndugu zangu!!!ebu angalieni aibu hii inayotujia jtatu

nderingosha

JF-Expert Member
Mar 20, 2011
4,208
3,097
Ikiwa imebaki siku moja tu kufanyika kwa shindano la Miss Universe kule Brazil (J'tatu) imenibidi nikate tamaa kwa mwakilishi wetu kule (yaani Nelly Kamwelu).

Nikiwa mmoja wa mdau na mkereketwa wa sifa nzuri kwa taifa letu ambaye nimekuwa nikifatilia maandalizi haya kule Brazil kwa kweli imenisikitisha baada ya kumfatilia mwakilishi wetu kule miss Nelly Kamwelu.

Nimekuwa nikimfatilia yeye na wawakilishi wetu wa africa haswa majirani zetu Angola na Botswana ambao kwa kweli wamepeleka vitu vya uhakika wajameni.

Kwanza sijui ilikuwaje watanzania tukampeleka mrusi kutuwakilisha, hivi kweli tumekosa mweusi mwenzetu jamani??

Nawaambia safari hii tena TZ imefanya kama walivopeleka muhindi Richa kipindi kile, tena safari hii ni mbaya zaidi kwani huyu mdada Nelly anaonekana kuiwakilisha urusi na wala si tz, hii ni fedheha kubwa jamani.

Kilichonifanya niumie sana ni kuona kuwa katika kuwakilisha vazi la taifa, wengine wote wamewakilisha mavazi yao kama waafrica wengine wamevaa nguo zao za taifa lakini cha ajabu huyu Nelly kapiga picha ya ajabu nawawekea hapa, hili vazi wanavaaga urusi na wala halina hadhi ya ki nchi ni aibu kubwa...yaani hata nguo za kanga wameshindwa kumpa huyu akavaa angalau kuonyesha anatoka Africa (Tanzani)? Hata Richa kipindi kile alivaa nguo za vitenge, huyu mrusi safari hii ametuua kabisa wajameni.

Pia hana mvuto hata chembe ukilingalisha na wadada toka majirani zetu hapa Angola na Botswana ni vitu adimu vya nguvu, safari hii kweli sitashangaa kusikia miss Angola au Botswana kashinda kwani ni watoto adimu na wakali kiyama.

Kwa kuwaonyesha tu picha ebu angalieni hizi picha za huyu mrusi wetu Nelly alafu tumlingalishe na wenzake Leila (miss Angola) na Larona (miss Botswana) alafu muone aibu tuliyopeleka kule.

Fuatilieni link hii kujua zaidi kinachojili kule miss universe Brazil.(Angalia pdf attachment ushangae anaebeba bendera yetu)

http://www.missuniverse.com/members/profile/599558/year:2011
 

BinMgen

JF-Expert Member
Jun 18, 2008
1,845
245
Ashindwe ashindwe mara milioni, Maluuni mkubwa huyo! wala haniwakilishi kitu, tena nataka ajinyee jukwaani hasa.
 

NIMIMI

Senior Member
Apr 2, 2011
170
16
Hakuna maana yeyote ile. Hakuna faida bora yafutwe kwani kutubomolea maadili ya nchi ye2 na bara kwa ujumla.
 

Danniair

JF-Expert Member
Feb 18, 2011
360
65
Sijawahi kuiona siku ambayo wanawake wa ki Tz walishindwa kuzaa watoto wa kike. Au kwa kuwa urusi ina historia ya kufaulu ktk mashindano kama haya? Ama alikosekana m-TZ wa kutoa hongo ili aende huko/?
 

Nish

JF-Expert Member
Jul 22, 2011
730
111
tanzania ingejitoa kabisa kwenye haya mashindano ya kipumbavu tangu nakua sijaona faida yake
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom