Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,435
- 113,444
Wanabodi,
Hili ni bandiko la swali la kisiasa, kiuchumi na kijamii. Kuna watu unawapa kazi halafu kupitia mambo madogo madogo tuu wanaonyesha wameshindwa, hivi unapowapa mambo makubwa zaidi, unategemea nini?. Tuendelee kujifunza kwa makosa au tukiona tuu dalili tujipange tusisubiri washindwe ndipo tutafute ufumbuzi.
Kabla sijasekwenda zaidi nianze kwa kutoa pongezi kwa serikali yetu awamu ya 5 kuyafanyia uchechemuzi mkubwa sekta ya usafiri na usafirishaji kuanzia kuifufua ATC, kujenga meli, kutandaza mabarabara nchi nzima, flyovers, kujenga SGR etc ambayo yote ni mambo makubwa mazuri japo in my opinion, bado naamini we are not very right in setting our priorities kwenye maendeleo ya vitu badala ya maendeleo ya watu na mfano mzuri ni money spent on display project ya kununua midege kwa cash ili kuifufua ATC ambayo ni tegemeo la wachache, the few and the rich ambao pia wanajengewa daraja la Agha Khan, if such monies were injected on agricultural sector ambayo ndio tegemeo la walio wengi, where we would have more multiplied effects;
Kuna msemo usemao usiposhukuru kwa madogo hutapewa makubwa. Tuwashukuru TRL kurejesha route ya Moshi, wataja rejesha na route ya Tanga na route ya Moshi Arusha.
Swali hili ni kuhusu utendaji wa TRL kwenye vitu vidogo vidogo tuu!. Ndio Maana Ninauliza Jee Sisi Watanzania Tutaendelea Kujifunza Kwa Makosa Hadi Lini?!. Hivi TRC Hawa Hawa Wanaoshindwa Vitu Vidogo Vidogo Kama Hivi!, Wataweza Kweli Kuja KuiRun SGR Yetu Effectively na Efficiently?
Mimi ni mmoja wa Watanzania wanaopenda leisure kama mfuko unaruhusu, I love travelling tena upate muda wa kutosha kuenjoy safari, ndio maana ukipanda Dreamliner ile inapaa tu hata kabla huja enjoy in less than 1-hour mnatangaziwa mjiandae for landing!. Naamini tuna Watanzania wengi they love travelling and adventures, hivyo nikiwaambia nilipata ajali mbaya ya pikipiki when travelling Dar -Dodoma with a big bike, wapenda rides watanielewa, na naamini hali yetu ya uchumi ingekuwa nzuri, Watanzania wengi tungekuwa tunasafiri sana for leisure na tunatembelea vivutio vyetu vya utalii.
Japo kikabila mimi sio Mchagga ila Moshi inanihusu hivyo kila Desemba around Christmas nami na familia yangu huwa tunaunga tela kwenda Moshi kuamkua jamaa, kwa kawaida huwa navurumisha mashine na kiukweli Moshi town na Mgombani during Christmas time is fun, utaenjoy tuu, hata "kuria hapo kidogo mbee" ni raha.
Mwaka huu niliposikia kuna gari moshi la kwenda Moshi, nikaamua mwaka huu nitafanya a leisure trip ya Moshi kwa gari moshi.
Hatua ya kwanza ni kutembelea website ya TRC kucheki bookings, huwezi amini, kwenye website ya TRC, hakuna hiyo route ya Moshi!
Nikapiga simu ya maulizo iliyopo kwenye website yao +255222110599
simu hii haijawahigi kupokelewa hadi kesho!, sijui wana operator mmoja tuu na kaenda likizo ya Christmas, hivyo akirudi ndio simu zitaanza kupokelewa tena.
Kunapokuwa hakuna taarifa zozote na hakuna mawasiliano yoyote, mtu analazimika kutoka hapo alipo hadi TRC kuulizia usafiri.
Nikaenda siku ya Jumamosi last week nikaelezwa nirudi leo J3 asubuhi.
Leo nimerudi ndio nikachoka kabisa!. Kwanza tuu utaratibu wa kukata tiketi ni utaratibu wa kijima kabisa!. Eti mtu anatakiwa kuwahi kufika na kupanga foleni dirishani on first come first served basis, hivyo ili kuwahi foleni, watu wamekuja usiku na kulala hapo ili asubuhi wawe wa kwanza, dirisha la malipo linafunguliwa saa 2:00.
Hilo zogo la hapo ni usipime!. Mtanisamehe sikuthubutu hata kunyanyua simu kupiga japo kapicha ni kuwadhalilisha tuu watu waliolala hapo usiku kucha kugombea tikeketi.
Kuna madirisha matatu ya tiketi, Dirisha la Gari Moshi la Kigoma, gari Moshi la Mwanza na gari Moshi la Moshi. Kwa mujibu wa kumbukumbu zangu za enzi zile, kwa kila route kulikuwa na madirisha matatu, watu wa 1st Class walikuwa na dirisha lao, 2nd Class dirisha lao na kule kajamba nani nao na dirisha lao. Sasa ni dirisha moja, na ili kuzuia mtu asiingilie na kujipenyeza kwenye foleni, watu mnasogeleana hadi kugusana!. Mambo gani haya?!.
Kiukweli hali niliyoiona hapa eneo la kukatia tiketi ya gari moshi la kwenda Moshi ni hali mbaya ya kukatisha tamaa hata ya leisure yenyewe basi tu.
Kutokana na hali hii, nimeanza kujiuliza hivi hawa TRC wenyewe ndio hawa tunao wategemea waje kutuendeshea gari moshi umeme la SGR?!. Watu wanashindwa vitu vidogo vidogo tuu kama hivi halafu ndio uje uwape vitu vikubwa vya kisasa kama SGR, wataweza kweli?. Au tusubiri tuu hadi hiyo SGR ije, tuwajaribishe kama wakishindwa ndipo tutafute watu!.
Sisi Watanzania tatizo ni nini mbona mambo madogo tuu haya yako hovyo hovyo, makubwa tutaweza?.
Sasa tuna mifumo mingi ya malipo na kuna online applications nyingi za bookings na kulipa online, kwanini hawa TRC wanatesa watu kiasi hiki?. Yaani mpaka leo kwenye ulimwengu huu wa sayansi na teke linalokujia, bado taasisi ya umma inayojiandaa kuendesha reli ya kisasa ya SGR, bado inaendesha mambo yake kijima hivi, tutegemee nini kwa uendeshaji wa SGR yetu, au tuendelee tuu na mtindo ule ule, hata tukiona dalili za wazi kabisa za watu walioshindwa kazi, bado tunaendelea kuwajaribu hadi washindwe ndipo tutafute dawa ya kutibu tatizo?
Watu wanajidai wako up to date hadi wana hot lines 24/7, lakini kwenye website yao wameweka landline number moja tuu tena haipokelewi!. Wameanzisha route mpya ya Moshi lakini there is no any info za route hiyo kwenye website yao?
Kaka yangu Masanja Kadogosa, you are doing good job lakini baadhi ya watu wako wanakuangusha kwa vitu vidogo vidogo tuu kama hivi vinapokuwa kero, hata kujua tuu ni lini na lini gari Moshi la wapi lipo, huwezi kujua hadi ufunge safari kuja kituoni?
Sisi vyombo vya habari kama jicho la umma, tunakunyooshea wewe kidole halafu na wewe banana na watu wako wa ndani.
Nawatakia Krismasi Njema.
Paskali