Watanzania tutajifunza kwa makosa hadi lini? Hivi TRC hawa wanaoshindwa vitu vidogo hivi wataweza ku-run SGR yetu effectively & efficiently?

Route ya kigoma imekuwepo muda wote,wamewaka mfumo wa ICT?
Paschal bwana, Sasa hata mabehewa yenyewe wanayahamisha from one route to another on a trial and error basis Unadhani kwa muda huu mfupi waliozindua hiyo route yao watakuwa tayari kuincorporate ICT systems kwa ajili ya booking?.

Kusimika mifumo ya ICT plus booking bado inahitaji muda.

ROMA haikujengwa siku moja

Unanikumbusha wale waliokuwa wakimbeza JK kujenga shule za kata wakati hakuna walimu wa kutosha, Sasa hivi kuna walimu kibao hadi kazi hawana!

Maendeleo ni hatua, cha msingi tuombe hatua zipigwe harakaharaka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nadhani wadau hawajamwelewa Paschal Mayala,tafadhali someni kwa kina ndio mje na majibu. tatizo alilolisema mleta mada huo ndio uhalisia wa sasa katika nchi yetu.Kuna mdau ameelezea Hospitali kule Sinza na maeneo mengine,mimi nasema hata katika mbuga zetu za Wanyama namba wanazo zitangaza waweza piga mwezi mzima simu haijawahi kupokelewa.
 
Mashirika mengi ya uma bado yanajiendesha kwa mazoea. Kuna vijana smart sana kama wangeajiruwa kwenye mashiraka haya hasa TRC na TTCL nadhani mambo yangekuwa poa. Ben Mwanantala ni mmoja wa kijana anayefanya vizuri sana, sasa sijui kama ndiyo yeye anahusika kwenye website za TRC. Hakuna kitu kina nikera kama kupanga foleni mda mrefu kwa ajili ya kusubiri huduma yaani huwa tunapoteza muda mwingi sana.
Issue ni ile ile wanajua wakirahisisha mambo watapigia wapi wanataka wapewe pesa dirishani wabaki na chenji, au wapunguze, mh mkapa alipo binafsisha mashirika ya umma tulimuona wa ajabu ila sisi ndio wa ajabu zaidi kwa mambo kama haya
 
Angalizo zuri sana hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
Angali hapa kwa ss 2na jikaza kisabun kulifanya Taifa hili kua na viwangoo ( Elim, utali, Afya ) Ila 2na sahau vyanzoo vidogo na muhimuu kwa maendeleo , hapa Baba usafirishaji ktk kila sector ni muhimuu kama 2navyo sisimua uchumi wa vyiwanda bila yakua na enough accessibility of electricity,. Uncle you have to work hard

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[Raisi Magufuli abahabgaika kuwapa Soko Lakini hawajiongezi .Serikali iwaondoe wafanyakazi wote iajiri vijana washike nagasi zao
 
Issue ni ile ile wanajua wakirahisisha mambo watapigia wapi wanataka wapewe pesa dirishani wabaki na chenji, au wapunguze, mh mkapa alipo binafsisha mashirika ya umma tulimuona wa ajabu ila sisi ndio wa ajabu zaidi kwa mambo kama haya
Nadhani Bora watangaze tenda ya uendeshaji ipewe kampuni private iendeshe shirika.Wenyewe hawajajipanga
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali la kisiasa, kiuchumi na kijamii. Kuna watu unawapa kazi halafu kupitia mambo madogo madogo tuu wanaonyesha wameshindwa, hivi unapowapa mambo makubwa zaidi, unategemea nini?. Tuendelee kujifunza kwa makosa au tukiona tuu dalili tujipange tusisubiri washindwe ndipo tutafute ufumbuzi.

Kabla sijasekwenda zaidi nianze kwa kutoa pongezi kwa serikali yetu awamu ya 5 kuyafanyia uchechemuzi mkubwa sekta ya usafiri na usafirishaji kuanzia kuifufua ATC, kujenga meli, kutandaza mabarabara nchi nzima, flyovers, kujenga SGR etc ambayo yote ni mambo makubwa mazuri japo in my opinion, bado naamini we are not very right in setting our priorities kwenye maendeleo ya vitu badala ya maendeleo ya watu na mfano mzuri ni money spent on display project ya kununua midege kwa cash ili kuifufua ATC ambayo ni tegemeo la wachache, the few and the rich ambao pia wanajengewa daraja la Agha Khan, if such monies were injected on agricultural sector ambayo ndio tegemeo la walio wengi, where we would have more multiplied effects

Kuna msemo usemao usiposhukuru kwa madogo hutapewa makubwa. Tuwashukuru TRL kurejesha route ya Moshi, wataja rejesha na route ya Tanga na route ya Moshi Arusha.

Swali hili ni kuhusu utendaji wa TRL kwenye vitu vidogo vidogo tuu!. Ndio Maana Ninauliza Jee Sisi Watanzania Tutaendelea Kujifunza Kwa Makosa Hadi Lini?!. Hivi TRC Hawa Hawa Wanaoshindwa Vitu Vidogo Vidogo Kama Hivi!, Wataweza Kweli Kuja KuiRun SGR Yetu Effectively na Efficiently?.

Mimi ni mmoja wa Watanzania wanaopenda leisure kama mfuko unaruhusu, I love travelling tena upate muda wa kutosha kuenjoy safari, ndio maana ukipanda Dreamliner ile inapaa tuu hata kabla huja enjoy in less than 1-hour mnatangaziwa mjiandae for landing!. Naamini tuna Watanzania wengi they love travelling and adventures, hivyo nikiwaambia nilipata ajali mbaya ya pikipiki when travelling Dar -Dodoma with a big bike, wapenda rides watanielewa, na naamini hali yetu ya uchumi ingekuwa nzuri, Watanzania wengi tungekuwa tunasafiri sana for leisure na tunatembelea vivutio vyetu vya utalii.

Japo kikabila mimi sio Mchagga ila Moshi inanihusu hivyo kila Desemba around Christmas nami na familia yangu huwa tunaunga tela kwenda Moshi kuamkua jamaa, kwa kawaida huwa navurumisha mashine na kiukweli Moshi town na Mgombani during Christmas time is fun, utaenjoy tuu, hata "kuria hapo kidogo mbee" ni raha.

Mwaka huu niliposikia kuna gari moshi la kwenda Moshi, nikaamua mwaka huu nitafanya a leisure trip ya Moshi kwa gari moshi.

Hatua ya kwanza ni kutembelea website ya TRC kucheki bookings, huwezi amini, kwenye website ya TRC, hakuna hiyo route ya Moshi!.

Nikapiga simu ya maulizo iliyopo kwenye website yao +255222110599
simu hii haijawahigi kupokelewa hadi kesho!, sijui wana operator mmoja tuu na kaenda likizo ya Christmas!, hivyo akirudi ndio simu zitaanza kupokelewa tena.

Kunapokuwa hakuna taarifa zozote na hakuna mawasiliano yoyote, mtu analazimika kutoka hapo alipo hadi TRC kuulizia usafiri.

Nikaenda siku ya Jumamosi last week nikaelezwa nirudi leo J.3 asubuhi.
Leo nimerudi ndio nikachoka kabisa!. Kwanza tuu utaratibu wa kukata tiketi ni utaratibu wa kijima kabisa!. Eti mtu anatakiwa kuwahi kufika na kupanga foleni dirishani on first come first served basis, hivyo ili kuwahi foleni, watu wamekuja usiku na kulala hapo ili asubuhi wawe wa kwanza, dirisha la malipo linafunguliwa saa 2:00.

Hilo zogo la hapo ni usipime!. Mtanisamehe sikuthubutu hata kunyanyua simu kupiga japo kapicha ni kuwadhalilisha tuu watu waliolala hapo usiku kucha kugombea tikeketi.

Kuna madirisha matatu ya tiketi, Dirisha la Gari Moshi la Kigoma, gari Moshi la Mwanza na gari Moshi la Moshi. Kwa mujibu wa kumbukumbu zangu za enzi zile, kwa kila route kulikuwa na madirisha matatu, watu wa 1st Class walikuwa na dirisha lao, 2nd Class dirisha lao na kule kajamba nani nao na dirisha lao. Sasa ni dirisha moja, na ili kuzuia mtu asiingilie na kujipenyeza kwenye foleni, watu mnasogeleana hadi kugusana!. Mambo gani haya?!.

Kiukweli hali niliyoiona hapa eneo la kukatia tiketi ya gari moshi la kwenda Moshi ni hali mbaya ya kukatisha tamaa hata ya leisure yenyewe basi tuu.

Kutokana na hali hii, nimeanza kujiuliza hivi hawa TRC wenyewe ndio hawa tunao wategemea waje kutuendeshea gari moshi umeme la SGR?!. Watu wanashindwa vitu vidogo vidogo tuu kama hivi halafu ndio uje uwape vitu vikubwa vya kisasa kama SGR, wataweza kweli?. Au tusubiri tuu hadi hiyo SGR ije, tuwajaribishe kama wakishindwa ndipo tutafute watu!.
Sisi Watanzania tatizo ni nini mbona mambo madogo tuu haya yako hovyo hovyo, makubwa tutaweza?.

Sasa tuna mifumo mingi ya malipo na kuna online applications nyingi za bookings na kulipa online, kwanini hawa TRC wanatesa watu kiasi hiki?. Yaani mpaka leo kwenye ulimwengu huu wa sayansi na teke linalokujia, bado taasisi ya umma inayojiandaa kuendesha reli ya kisasa ya SGR, bado inaendesha mambo yake kijima hivi, tutegemee nini kwa uendeshaji wa SGR yetu, au tuendelee tuu na mtindo ule ule, hata tukiona dalili za wazi kabisa za watu walioshindwa kazi, bado tunaendelea kuwajaribu hadi washindwe ndipo tutafute dawa ya kutibu tatizo?.

Watu wanajidai wako up to date hadi wana hot lines 24/7, lakini kwenye website yao wameweka landline number moja tuu tena haipokelewi!. Wameanzisha route mpya ya Moshi lakini there is no any info za route hiyo kwenye website yao?.

Kaka yangu Masanja Kadogosa, you are doing good job lakini baadhi ya watu wako wanakuangusha kwa vitu vidogo vidogo tuu kama hivi vinapokuwa kero, hata kujua tuu ni lini na lini gari Moshi la wapi lipo, huwezi kujua hadi ufunge safari kuja kituoni?.

Sisi vyombo vya habari kama jicho la umma, tunakunyooshea wewe kidole halafu na wewe banana na watu wako wa ndani.

Nawatakia Krismasi Njema.

Paskali
Ni kweli kabisa TRL mnatakiwa kubadilika. Mbona ni applications ndogo sana za kufanya booking? Kwanza mfumo wa malip ya taslim sio mzuri sana kiusalama. Anzeni mabadiliko
 
Huwa nashangaa sana mtu anavyosema kuwa eti pesa zinanunua ndege ama kujenga miundo mbinu zingeelekezwa kwenye kilimo. Hivi wewe Pascal Mayalla kwa akili yako tukiendeleza kilimo bila miundo mbinu hayo mazao unayasafirisha na nini?

Je unajua kuwa Kenya inatushinda kuuza bidhaa za chakuka nje? Unajua ni kwa nini?

Ulikuwa na hoja nzuri ila umeongeza na ushabiki ama mihemuko

God save us
 
Pascal nakumbuka ulizungumzia suala la matumizi ya barabara na hasa inapotokea kuna misafara ya viongozi huko Ulaya and Sweden in particular, nilijifunza kuwa watendaji wengi wa serikali yetu wakienda nje jambo la kwanza kwao ni shopping hawaendi kujifunza na kama watajifunza mafunzo hayatakuwa na tija hapa kwetu kwasababu wanatumikia interest binafsi, naamini kama wangekuwa wanajifunza kwa dhati tungekuwa na mabadiliko chanya mengi.

Leo limetokea hilo la TRC, sidhani Kadogosa hajatembelea nje akaona utendaji wa mashirika ya reli huko, anafahamu sana kinachofanyika kwa wenzetu.

Hapa kwetu kuna shida yawezekana kuna team ya viongozi wa juu wasiopenda digitization kwakuwa ajira nyingi zitafutwa, lakini hawafikirii kuwa wanaweza kutengeneza ajira nyingi zaidi kwa kuboresha huduma ambazo sasa zinafanywa manually.

Niliwahi kutoa ushauri humu kuwa ni vema sana taasisi zote za serikali na binafsi zinazotoa hudumabkwa jamii zikaweka platforms za kupokelea mawazo mapya na malalamiko, hata kuwashirikisha wananchi kwenye initial design za miradi badala ya watu kujifungia na kufanya designing yenye mtazamo wao peke yao huku mradi unakwenda kuwahudumia wananchi wengi, natolea mfano stand mpya ya mabasi Iringa ambayo haikuzingatia kabisa mahitaji ya watumiaji.

Ipo haja Kadogosa akawachukua watu wenye exposure kama wewe P na wengineo waliozunguka duniani akawakalisha mkatengeneza mapendekezo ya maboresho ya huduma za shirika tajwa kwakuwa nina uhakika hajawahi kupeleka watu wake nje kujifunza, kwahiyo kuepuka gharama ya kupeleka watu wake kujifunza basi awatumie mliopo tayari na itasaidia kuja na mtazamo mpya wa utendaji wa shirika.

Shirika likiboreshwa, litavuta wateja wengi, mapato yataongezeka, masilahi ya watumishi wa shirika yataongezeka, lakini hali uliyokutana nayo ya ukataji tickets manually inaendekezwa kwasababu ya kutafuta virushwa na wizi mdogomdogo kwakuwa watumishi wenyewe wana njaa.

Ifahamike wazi kuwa hapa kwetu Tanzania watumishi wananeemeka kupitia uduni wa huduma zinazotolewa.
Wiki moja iliyopita misafara miwili tofauti Morogoro na Zanzibar iliua watu wawili, mmoja Morogoro na mwingine Zanzibar.
 
Kaka yangu Masanja Kadogosa, you are doing good job lakini baadhi ya watu wako wanakuangusha kwa vitu vidogo vidogo tuu kama hivi vinapokuwa kero, hata kujua tuu ni lini na lini gari Moshi la wapi lipo, huwezi kujua hadi ufunge safari kuja kituoni?.

Nadhani hili la kukosoa na kusifia ndio linalowachanganya hao wenye nafasi za kufanya mabadiliko.

Kama kuna watu chini yake hawafanyi yanayotakiwa, yeye hawezi kuwa anafanya vizuri...na maanisha overall perfomance/average inakula hata juhudi za wachache waliofanya kwa kupitiliza. Na kwa level ya shirika, kama limeyumba, aliyepewa dhamana hiyo ametumba tu.

Mengine ni majukumu yake ya kazi, asifiwe akienda extra mile....alaumiwe kila wakati
 
Mkurugenzi wa TRC anabeba hizilawama kwa asilimia mia.

Mkurugenzi ameahindwa kazi that's the simply word to say.

Miniliwatafuta kwenye website yao sikuwaelewa nikaulizia nikaambiwa ticket zinapatikana pale kamata, nilipofika nilichoona nikatukana nikaondokazangu.

Magufuli bado anakazi kubwa sana kwenye hii nchi hadi namuoneaga huruma.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli mkuu halafu anakuja mtu, anakwambia eti sisi ni third world country kwa hiyo kufanya mambo bila utaratibu unaoeleweka eti ndio desturi yetu hii ni fikira ya hovyo kabisa.

Ni kiri kabisa mimi namkubali sana Mh. Magufuli kwa kweli huyu baba hajawahi kupewa nafasi yoyote ya utumishi akafail, kila wizara aliyopita hakukuwa na uzembe uzembe watu walichapa kazi kwa kumuhofia, hata sasa nafasi aliyonayo ya Uraisi anafanya vuzuri , shida naiona bado ipo kwa wasaidizi wake ni kama bado hawaendani na kasi yake kabisa japo kuna baadhi wanajaribu.
 
Mkuu katika mambo mengine unaweza kuwa na hoja ya msingi lakini katika hili nakupinga. Kwa Tz ya sasa ambayo angalau asilimia kubwa imepata elimu ya shule ya kata ujinga na umasikini haiwezi kuwa sababu kwenye hili. Tatizo ni usimamizi.

Makampuni ya simu yanahudumia WaTz hawa hawa lakini yanaendesha mambo yao yote kwa mtandao. Pamoja na umasikini wake ila kwa sasa angalau kila kaya ina simu; wananunua vocha, wanaweka, wanajiunga vifurushi n.k mbona haya wanayaweza? Watashindwa nini kukata tiketi kwa mtandao?

WaTz hawahawa masikini hadi wanaopelekewa umeme wa REA wameweza kununua umeme kwa LUKU kupitia simu zao au wanaenda kwenye vituo vya mauzo. Watashindwa tiketi za treni?

Baadhi makampuni ya mabasi kama Dar lux na Shabiby wanakatisha tiket online. Mifano ni mingi.
Hawa TRL wamekosa usimamizi. Business as usual.
Mimi sijalenga eneo moja tu la ukataji wa tiketi, mimi naongelea huduma kwa ujumla.

Ukisoma baadhi ya comment kuna walioainisha maeneo kadha wa kadha ambako wamekuwa wanakutana na kero za huduma, kuna mmoja alitoa mfano wa Zahanati yao ya kata....na akasema kabisa usiombe Mkeo apate ujauzito...hivi kama una uwezo utafuata nini kwenye hiyo Zahanati ili hali kuna Aga khan?

Hivi unadhani mradi kama wa DART wakiachiwa uhuru wa kuhudumia wanavyotamani wao na wahakikishe huduma zinakuwa daraja la kwanza nauli zitakuwa kiasi gani? utasema kudemadema kwa ule mradi ni usimamizi au pesa hazitoshi? usimamizi ni mgumu bila pesa/mapato? na ni vigumu kuwa na mapato kutoka kwa Wananchi wasio na uwezo...au wewe una jibu tofauti na hilo?

Leo basi TRC wajenge jengo kama lile la pale JKNA, kwani nani hataki huduma za hali ya juu? lakini Wahusika watakuuliza tujenge ili tuwahudumie kina nani?

Pointi yangu ni kuwa ubora huambatana na gharama.

Ndio maana nimetoa mfano wa Mchechu na NHC, yalivyomfika kwa kutaka kujenga nyumba za kisasa na ziuzwe kwa Wananchi "Masikini" kwa milioni hamsini.
 
Hivi kwani vyuo vyetu vikuu hasa UDSM wameshindwa kuja na utafiti wa kusaidia namna bora ya kuendesha haya mashirika ya uma kwa faida huku, wakitoa huduma bora.
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali la kisiasa, kiuchumi na kijamii. Kuna watu unawapa kazi halafu kupitia mambo madogo madogo tuu wanaonyesha wameshindwa, hivi unapowapa mambo makubwa zaidi, unategemea nini?. Tuendelee kujifunza kwa makosa au tukiona tuu dalili tujipange tusisubiri washindwe ndipo tutafute ufumbuzi.

Kabla sijasekwenda zaidi nianze kwa kutoa pongezi kwa serikali yetu awamu ya 5 kuyafanyia uchechemuzi mkubwa sekta ya usafiri na usafirishaji kuanzia kuifufua ATC, kujenga meli, kutandaza mabarabara nchi nzima, flyovers, kujenga SGR etc ambayo yote ni mambo makubwa mazuri japo in my opinion, bado naamini we are not very right in setting our priorities kwenye maendeleo ya vitu badala ya maendeleo ya watu na mfano mzuri ni money spent on display project ya kununua midege kwa cash ili kuifufua ATC ambayo ni tegemeo la wachache, the few and the rich ambao pia wanajengewa daraja la Agha Khan, if such monies were injected on agricultural sector ambayo ndio tegemeo la walio wengi, where we would have more multiplied effects

Kuna msemo usemao usiposhukuru kwa madogo hutapewa makubwa. Tuwashukuru TRL kurejesha route ya Moshi, wataja rejesha na route ya Tanga na route ya Moshi Arusha.

Swali hili ni kuhusu utendaji wa TRL kwenye vitu vidogo vidogo tuu!. Ndio Maana Ninauliza Jee Sisi Watanzania Tutaendelea Kujifunza Kwa Makosa Hadi Lini?!. Hivi TRC Hawa Hawa Wanaoshindwa Vitu Vidogo Vidogo Kama Hivi!, Wataweza Kweli Kuja KuiRun SGR Yetu Effectively na Efficiently?.

Mimi ni mmoja wa Watanzania wanaopenda leisure kama mfuko unaruhusu, I love travelling tena upate muda wa kutosha kuenjoy safari, ndio maana ukipanda Dreamliner ile inapaa tuu hata kabla huja enjoy in less than 1-hour mnatangaziwa mjiandae for landing!. Naamini tuna Watanzania wengi they love travelling and adventures, hivyo nikiwaambia nilipata ajali mbaya ya pikipiki when travelling Dar -Dodoma with a big bike, wapenda rides watanielewa, na naamini hali yetu ya uchumi ingekuwa nzuri, Watanzania wengi tungekuwa tunasafiri sana for leisure na tunatembelea vivutio vyetu vya utalii.

Japo kikabila mimi sio Mchagga ila Moshi inanihusu hivyo kila Desemba around Christmas nami na familia yangu huwa tunaunga tela kwenda Moshi kuamkua jamaa, kwa kawaida huwa navurumisha mashine na kiukweli Moshi town na Mgombani during Christmas time is fun, utaenjoy tuu, hata "kuria hapo kidogo mbee" ni raha.

Mwaka huu niliposikia kuna gari moshi la kwenda Moshi, nikaamua mwaka huu nitafanya a leisure trip ya Moshi kwa gari moshi.

Hatua ya kwanza ni kutembelea website ya TRC kucheki bookings, huwezi amini, kwenye website ya TRC, hakuna hiyo route ya Moshi!.

Nikapiga simu ya maulizo iliyopo kwenye website yao +255222110599
simu hii haijawahigi kupokelewa hadi kesho!, sijui wana operator mmoja tuu na kaenda likizo ya Christmas!, hivyo akirudi ndio simu zitaanza kupokelewa tena.

Kunapokuwa hakuna taarifa zozote na hakuna mawasiliano yoyote, mtu analazimika kutoka hapo alipo hadi TRC kuulizia usafiri.

Nikaenda siku ya Jumamosi last week nikaelezwa nirudi leo J.3 asubuhi.
Leo nimerudi ndio nikachoka kabisa!. Kwanza tuu utaratibu wa kukata tiketi ni utaratibu wa kijima kabisa!. Eti mtu anatakiwa kuwahi kufika na kupanga foleni dirishani on first come first served basis, hivyo ili kuwahi foleni, watu wamekuja usiku na kulala hapo ili asubuhi wawe wa kwanza, dirisha la malipo linafunguliwa saa 2:00.

Hilo zogo la hapo ni usipime!. Mtanisamehe sikuthubutu hata kunyanyua simu kupiga japo kapicha ni kuwadhalilisha tuu watu waliolala hapo usiku kucha kugombea tikeketi.

Kuna madirisha matatu ya tiketi, Dirisha la Gari Moshi la Kigoma, gari Moshi la Mwanza na gari Moshi la Moshi. Kwa mujibu wa kumbukumbu zangu za enzi zile, kwa kila route kulikuwa na madirisha matatu, watu wa 1st Class walikuwa na dirisha lao, 2nd Class dirisha lao na kule kajamba nani nao na dirisha lao. Sasa ni dirisha moja, na ili kuzuia mtu asiingilie na kujipenyeza kwenye foleni, watu mnasogeleana hadi kugusana!. Mambo gani haya?!.

Kiukweli hali niliyoiona hapa eneo la kukatia tiketi ya gari moshi la kwenda Moshi ni hali mbaya ya kukatisha tamaa hata ya leisure yenyewe basi tuu.

Kutokana na hali hii, nimeanza kujiuliza hivi hawa TRC wenyewe ndio hawa tunao wategemea waje kutuendeshea gari moshi umeme la SGR?!. Watu wanashindwa vitu vidogo vidogo tuu kama hivi halafu ndio uje uwape vitu vikubwa vya kisasa kama SGR, wataweza kweli?. Au tusubiri tuu hadi hiyo SGR ije, tuwajaribishe kama wakishindwa ndipo tutafute watu!.
Sisi Watanzania tatizo ni nini mbona mambo madogo tuu haya yako hovyo hovyo, makubwa tutaweza?.

Sasa tuna mifumo mingi ya malipo na kuna online applications nyingi za bookings na kulipa online, kwanini hawa TRC wanatesa watu kiasi hiki?. Yaani mpaka leo kwenye ulimwengu huu wa sayansi na teke linalokujia, bado taasisi ya umma inayojiandaa kuendesha reli ya kisasa ya SGR, bado inaendesha mambo yake kijima hivi, tutegemee nini kwa uendeshaji wa SGR yetu, au tuendelee tuu na mtindo ule ule, hata tukiona dalili za wazi kabisa za watu walioshindwa kazi, bado tunaendelea kuwajaribu hadi washindwe ndipo tutafute dawa ya kutibu tatizo?.

Watu wanajidai wako up to date hadi wana hot lines 24/7, lakini kwenye website yao wameweka landline number moja tuu tena haipokelewi!. Wameanzisha route mpya ya Moshi lakini there is no any info za route hiyo kwenye website yao?.

Kaka yangu Masanja Kadogosa, you are doing good job lakini baadhi ya watu wako wanakuangusha kwa vitu vidogo vidogo tuu kama hivi vinapokuwa kero, hata kujua tuu ni lini na lini gari Moshi la wapi lipo, huwezi kujua hadi ufunge safari kuja kituoni?.

Sisi vyombo vya habari kama jicho la umma, tunakunyooshea wewe kidole halafu na wewe banana na watu wako wa ndani.

Nawatakia Krismasi Njema.

Paskali
Nakuuna mkono poti hapo TRC ni kero ya kutiisha, yaani inatisha sana tu. Yaani tiketi kwa nini isifanyike kwa mtandao bana. Kila kitu KAMATA.
 
Back
Top Bottom