Watanzania tusiwe wanafiki, Tozo ni muhimu kwa upana wake

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
15,316
24,181
Unafiki unatumaliza Watanzania.

Kodi zilizokuwa zikitozwa na serikali ya Awamu ya Tano kwa wafanyabiashara na wajasiria mali, wengi waliitikia wakisema mafisadi hao au wahujumu uchumi.

Kipindi cha Awamu ya Tano uonezi mwingi wa kupora, kunyang'anya, kubambika kodi na hata watu kuwekwa ndani na kufunguliwa kesi za uongo za uhujumu uchumi zilikuwepo tena nyingi sana.

Lengo lake kupata fedha kwa udi na uvuma kwa miradi ya SGR na Stiglaz Umeme na mingine mingi.

Kuna wananchi walishangilia sana uonezi uliofanywa.

Wapo viongozi walio kundi hili, Waziri Mpango wakati huo hakosekani humo.

Sasa Awamu ya Sita imerekebisha hilo ili KODI IWE KWA WATANZANIA WOTE.

Na hili linatekelezwa kwa kupitia TOZO za miamala ambazo zinamgusa kila mtu.

Hapo ndio unaona unafiki wa watu.

Hawapendi kuchangia kodi kwa maendeleo, wao wanafikiri kundi fulani tu ndio litoe kodi ili wao waneemeke.

Mshindwe, lipeni kodi Watanzania.
 
Kuna Mtanzania alikuambia hataki kulipa kodi! Au kukatwa hizo tozo? Watu wanalalamikia matumizi yake, yaliyojaa ubadhirifu mkubwa na ufisadi wa kutisha!

Lakini pia watu wanalalamikia namna wahamasishaji wenyewe wa hizo kodi/tozo kuwa mstari wa nyuma kwa kukwepa kulipa, huku wanyonge na watu wa kawaida wakiwajibishwa ipasavyo!

Mfano mzuri ni Kesi ya Mbunge wa Ukonga Jerry Silaa kulalamikia mishahara ya Wabunge kutokukatwa kodi, Mshahara wa Rais nao tunasikia haukatwi kodi, nk. Hiki kitu ndicho kinacho amsha hisia hasi kwa raia.

Ili kodi na tozo zilipwe kwa urahisi, viongozi wawe mfano wa kuigwa kwa kulipa hizo kodi, lakini pia kuzitumia kwa matumizi sahihi! Na siyo kuzitapanya, kama ilivyo sasa.
 
Kuna Mtanzania alikuambia hataki kulipa kodi! Au kukatwa hizo tozo? Watu wanalalamikia matumizi yake, yaliyojaa ubadhirifu mkubwa na ufisadi wa kutisha...
Hamkulalamika hivyo wakati wa Magufuli, kuwa fedha wanazonyang'anya wafanya biashara zinaenda wapi?

Arusha Beureu De Change zimeporwa na vyombo vya serikali, hela ilienda wapi?

Ndio maana nasema tusiwe wanafiki.
 
Sasa hizi tozo mnazokamua si ni sawa na kurudisha kodi ya kichwa vima nyie, kwa nini mnakata VAT sasa kwenye huduma na bidhaa ambazo kila mwananchi anapofanya manunuzi na kulipia bidhaa mbalimbali analipa, na zile PAYE mnazokata wafanyakazi bado haziwatoshi.

Unataka kuaminisha watu kipindi cha Magu wafanyabiashara pekee ndo walikuwa wanalipa kodi. Kimsingi hakuna mfanyabiashara anye lipa kodi zaidi ya kuwasilisha yale makato ya VAT ambayo ni mwananchi aliyelipa. Kawambie waliokutuma hii imegonga mwamba.
 
Hamkulalamika hivyo wakati wa Magufuli, kuwa fedha wanazonyang'anya wafanya biashara zinaenda wapi?..
Watu walilalamika wewe! Labda mwenzetu hukuwepo nchini. Hata sisi wafanyakazi wa serikali tulio dhulumiwa stahiki zetu kwa kigezo cha kununua ndege kwanza, tulilalamika sana humu!

Lakini tuliishia tu kukejeliwa na kudhihakiwa. Kwa hiyo siyo kweli kusema kwamba eti wakati wa magufuli watu walikuwa hawalalamiki.

Na kuhusu waliokuwa wakishangilia, hao bila shaka walikuwa ni MATAGA na Wananchi wasio na uelewa mpana wa mambo mbalimbali katika nchi! Na ambao kimsingi hawakuwa na tofauti yoyote ile na bendera fuata upepo.
 
Fanyeni yote lakini huo mpango wa tozo kwa mitandao ya kijamii muendee kwa akili na busara. Siku google, Twitter, facebook, Istergram, yahoo na wengine wakiamuu kuwazimia mitambo yao mjue mmeondolewa madarakani na nguvu ya umma.
 
Hamkulalamika hivyo wakati wa Magufuli, kuwa fedha wanazonyang'anya wafanya biashara zinaenda wapi?
Arusha Beureu De Change zimeporwa na vyombo vya serikali, hela ilienda wapi?
Ndio maana nasema tusiwe wanafiki.
Flyover unayokatisha ubungo imebeba sehemu ya hizo fedha!
 
Ishu sio tozo, ishu ni transparency!

Tumeambiwa ni tozo za uzalendo which means ni pesa yetu wananchi basi tunaomba isichezewe na kwa kuhakikisha hilo kuwe na real time system ambayo ni kama portal mwananchi anaweza kuangalia on a daily imeingia shillingi ngapi kwenye kapu na taarifa za kutolewa pesa ziwe wazi kwamba kiasi gani kimetolewa kwenye mfuko huo na kinaenda kujenga shule au barabara gani kama tulivyokubaliana.

Sio watu wanajichotea hela tu kwa siri humo na kufanya mambo yao kwa jasho la wananchi! Haifai na wala haikubaliki na kutokana na mazoea ya ufisadi wa viongozi wa chama tawala for years hatuna imani na usalama wa tozo na ndio maana tunalalamika kukatwa michango hio!
 
Wapuuzi na wanafiki ni kama wewe usiyetaka kulipo kodi ya TOZO ukitegemea mwanaume mwingine akulipie maendeleo yako.
Babu mbona ulianza vizuri ila kama unaelekea kwenye michambo sasa. Kwahiyo we unaona fair mwanaume atozwe ili bwana mwingine atambe huko na STL sio? mara ngapi ripoti za CAG zinasomwa na unaambiwa wajomba wanakwapua mizigo yakutosha na hakifanyiki kitu. We unahisi hiyo kodi wanalipa wavaa madela sio?
 
Unafiki unatumaliza Watanzania.
Kodi zilizokuwa zikitozwa na serikali ya Awamu ya Tano kwa wafanyabiashara na wajasiria mali, wengi waliitikia wakisema mafisadi hao au wahujumu uchumi.

Kipindi cha Awamu ya Tano uonezi mwingi wa kupora, kunyang'anya, kubambika kodi na hata watu kuwekwa ndani na kufunguliwa kesi za uongo za uhujumu uchumi zilikuwepo tena nyingi sana.

Lengo lake kupata fedha kwa udi na uvuma kwa miradi ya SGR na Stiglaz Umeme na mingine mingi.

Kuna wananchi walishangilia sana uonezi uliofanywa.
Wapo viongozi walio kundi hili, Waziri Mpango wakati huo hakosekani humo.

Sasa Awamu ya Sita imerekebisha hilo ili KODI IWE KWA WATANZANIA WOTE.

Na hili linatekelezwa kwa kupitia TOZO za miamala ambazo zinamgusa kila mtu.

Hapo ndio unaona unafiki wa watu.
Hawapendi kuchangia kodi kwa maendeleo, wao wanafikiri kundi fulani tu ndio litoe kodi ili wao waneemeke.

Mshindwe, lipeni kodi Watanzania.
Kwanini hatuendelezi madini chuma kule Liganga na Mchuchuma? Chuma ni utajiri
 
Hamkulalamika hivyo wakati wa Magufuli, kuwa fedha wanazonyang'anya wafanya biashara zinaenda wapi?
Arusha Beureu De Change zimeporwa na vyombo vya serikali, hela ilienda wapi?
Ndio maana nasema tusiwe wanafiki.
Unajua beureu ziliporwaa pesa kwa ajili gani?? Kama hujui kitu bora unyamaze ufiche ujinga wako! Wale watu wa beureu walikuwa wanaficha dola ili zipungue mitaani kisa dola ipandee..rais akaona wanasaliti nchi wakafanyiwa hivyo..sasa ww punguani unakurupuka huko fyoko fyoko hujui chochote..subir hizo tozo uone kama kuna jipyaa litakalofanywaa na hao wapuuzi.. akili yako itakaa sawaa..ila kwa kuwa ww n kipofuu hutajua hilo umekosa ilmu dunia..unaelimu yako ya hukooo
 
Back
Top Bottom